rose mzalendo
Member
- Mar 5, 2019
- 71
- 114
Nimeikuta mahala Fulani. Soma nawe ujifunze
Nilikua nikiamini kuwa mwanamke sio mtu wa kuamini, kila nikiangalia mapenzi namna watu wanavyoumizwa na kutapeliwa niliamua kumuamini tu Mama yangu hivyo kila kitu nilichokua nikikichuma niliandika majina yake.
Nilikua nikimshirikisha Mama na kumuambia mambo yangu kila siku, naye pia alikua akinisikiliza na alikua akiniunga mkono, nadhani kwa kiasi kukubwa alikua anafurahia nilivyokua najitambua kwa kutukumuamini mke wangu.
Mpaka Mama yangu anafariki Dunia kila kitu kilikua kwa jina lake, hakuna kitu hata kimoja nilichochoma katika maisha yangu kilikua na jina langu. Mke wangu hakujua na ndugu zangu hawakujua, hata Baba yangu sikumuambia kwani mimi nilikua ni mtoto wa Mama. Kutokana na usiri ule hata nyaraka sikuziweka nyumbani, niliweka nyumbani kwa Mama na yeye peke yake ndiyo alikua anajua.
Najua mnaweza kujiuliza ni kwanini nilikua nikimuamini Mama na si Baba? Hiyo ilitokana na tabia za Baba yangu kipindi tukiwa wadogo, alikua akimnyanyasa sana Mama, akimpiga na kuna kipindi walitengana Baba akaenda kuoa mwanamke mwingine lakini mwishoni Baba aliugua sukari, nguvu zikamuishia akaomba msamaha na ingawa sisi tulimuambia Mama hakuna kurudiana naye lakini alimrudia, kwa bahati mbaya Mama ndiyoa liwahi kufariki pamoja na afya yake kuwa nzuri.
Baada ya Mama kufariki ghafla, hakua akiumwa alikua kalala na asubuhi hakuamka, tulimaliza msiba na kila mtu kurejea kwake, Baba alibaki mwenyewe na kwakua watoto wote tulikua tukimchukia hakuna aliyejali zaidi ya ndugu zake ambao walikua wakimpa misaada misaada. Lakini kabla ya mimi kuondoka nyumbani kwa Mama nilianza kutafuta nyraka ambazo nilimpa Mama, nilikua natafuta kimya kimya kwani sikutaka mtu ajue, niihangaika kutwa nzima bila kuzipata.
Kusema kweli nilichanganyikiwa, niliondoka kimya nikiwa na mawazo sana, usiku wake Baba alinipigia simu. Nilihisi kaziona nayeye ndiyo kazificha, niliwasha gari na kurudi nyumbani kuonana na Baba.
“Mama yako amekufa na mimi sina muda nitakufa…” Baba alianza kuniambia, nilimsikiliza huku kichwa changu kikiwaza kuhusu nyaraka zangu, yeye alikua akiniangalia tu na hakunipa muda wa kuzungumza.
“Najua mnanichukia na mlitamani nianze kufa mimi, lakini mwanangu hivi unajua ni kwanini mnanichukia?” Aliniuliza, nilizuga kuwa simchukii lakini alicheka, aliniambia anajua na hata baada ya Mama kufariki matumizi hatutatoa, aliniuliza kama najua kuwa ni kwanini tunamchukia.
Nilimuangalia kwa hasira na kumuambia mambo yote mabaya ambayo alikua anamfanyia Mama, namna alivyokua akimnyanyasa, hamjali na jinsi ambavyo alikua anabadilisha wanawake bila kujali kuwa anamuumiza Mama.
Alicheka kwa dharau kitu ambcho kiliniumiza zaidi.
“Sasa wewe ilikua inakuuma nini? Mama yako si alikua ni mke wangu, naweza kumfanya chochote kile ninachotaka?” Aliongea kwa dharau, hasira zilinipanda na kweli nilitamani hata kumtandika makofi lakini nilijizuia, mtu mwenyewe alishachoka na kama ni kupigwa ulimwengu ulishampiga.
“Mbona wewe mke wako nayeye unamuona kama takataka, humjali unajifanya unampenda Mama yako lakini mkeo unamnyanyasa au hujui kuwa Mke wako ndiyo Mama wa watoto wako na hujui kuwa jinsi unavyonichikia mimi ndiyo hivyo hivyo wanao watakuchukia.”
Aliongea maneno amayo yalinichoma na kuamua kumjibu, nilimuambia kuwa mimi si kama yeye, simpigi mke wangu, sichepuki na wala simnyanyasi nampa kila kitu.
“Unampa kila kitu lakini humuamini? Unampa kila kitu lakini mali zote umemuandika Mama yako? Unafikiri ukifa leo mke wako atapata nini? Unafikiri hizo mali zako zitakua na faida gaani kwa wanao kama Mama yao hazijui na kuzisimamia?” Aliniuliza, nilishtuka kujua kuwa anajua kila kitu kuhusu mali zangu, nikiwa nashangaa shangaa alitoa nyaraka zote na kunionyesha.
Mwanangu kisheria hizi mali ni za kwangu, mimi ndiyo mume halali wa Mama yako na ndiyo natakiwa kuzichukua, lakini pia ndugu zako wanaweza kuzirithi kwani ni Mali za Mama yao na si zako.” Aliongea huku akiniangalia. Nilishikwa na butwaa nikimuangalia.
Chukua mali zako, badilsiha majina na weka majina ya wanao kama humuamini basi mke wako, ndugu zako wakija kujua kuwa Mama yao aliacha mali hawatakuacha, unapoficha mali kwa mke wako basi jua kuwa unaficha mali kwa wanao kwani ukifa yeye ndiyo atawalea na si Bibi yao.”
Alinikabidhi nyaaka zangu zote na kuniambia niondoke, niliondoka huku nikiwa na mawazo, nilijisikia vibaya kumuacha baba yangu katika hali ile, alikua mpwkee kachanganyikia, alikua na mawazo, kakonda na alikua kakata tamaa. Nilirudi nyumbani lakini usiku sikulala, nilimuamsha mke wangu na kumuambia kuwa tunatakiwa kumchukua Baba kwani hali yake ni mbaya, mke wangu alikubali na kuniambia nilale asubuhi tukamchukue.
Asubuhi naamka kitu cha kwanza ilikua ni kujiandaa kwenda kwa Baba, niliwahsa gari, nilifika na kuanza kugonga Baba hakusikia, nilijaribu kufungua milango ilikua haijafungwa. Niliingia na kufika sebuleni nilimkuta Baba kakaa kwenye kochi kajinyoosha, nilimuita sana lakini hakushtuka, alikua ashapoa, Baba yangu alikua kafariki dunia. Niliangalia pembeni na kukuta kikaratasi. “Nilishakufa muda mrefu Mama yenu ndiyo alikua ananiweka hai tu, naumwa sana nitakua mzigo kwenu, siwezi kuishi bila Mama yenu kwaherini bora niondoke.”
Baba alikua amejiua, nilijisikia vibaya sana kwani jana yake nilikua naye, nilitakiwa kuona namna alivyokua mpweke na kumchukua.
Ndugu zangu hakuna aliyejali hata hawakuumia sana walisikitika kidogo lakini mwishyo kila mmoja aliendelea na maisha yake, nilijisikia vibaya zaidi kwani pamoja na kuwa sikua nikimnyanyasa mke wangu lakini nilikua namfanya kama mgeni, sikusikiliza mawazo yake na sikumshirikisha katika mambo ya maendeleo, niliumia sana na tangu siku hiyo niliamua kumfanya mke wangu kama mshirika wa ndoa yangu na si kama mgeni mtu wa kupita tu.