Tambua thamani yako.

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,627
154,987
Kuna bwana mmoja alikuwa hana ajira kwa muda mrefu licha ya kuwa alikuwa na elimu ya chuo kikuu.
Ili maisha yaendelee ilibidi ajishikize kwenye ajira ya udereva wa taxi.
Bahati nzuri kulikuwa na ndugu yake aliyekuwa masomoni nje, akamuunganisha na dada mmoja mwenye kampuni kubwa ya clearing and forwarding ili jamaa akaajiriwe kama meneja wa masoko kwenye kampuni hiyo.
Siku ya kukutana na mkurugenzi kwa ajili ya kwenda kufahamiana na kuanza kazi jamaa akaanzia kwenye kijiwe chake cha taxi. Akiwa kijiweni hapo akapita dada mmoja mwenye bonge la wowowo, akiwa anafanya mazoezi ya matembezi ya asubuhi. Taxi dereva msomi akaanza kupiga miluzi na kumfanyia kila aina ya dhihaka yule dada, dada akampuuza na kuendelea na mazoezi yake.
Muda ukafika, jamaa akawasha taxi yake na kuelekea kwenye miadi ya kazi .
Akafika kwenye hiyo ofisi na akaomba kuonana na mkurugenzi. Sekretari akamkaribisha ndani kwa mkurugenzi,. Kwa jinsi alivyokuwa amevalia na kwa kuwa ameketi, jammaa hakumkumbuka yule dada kuwa ndiye aliye mfanyia dhihaka asubuhi, lakini yule dada alimkumbuka vizuri.

Baada ya maongezi, yule dada akamuuliza ukimuona mwanamke mwenye makalio kama yangu huwa una behave vipi?
Dada akainuka na kugeka, jamaa bado hakupata picha.
Dada akamkumbusha mkasa wa asubuhi na kumweleze kuwa ame disqualify hiyo post ya umeneja, kwa hiyo aondoke.
Jamaa akatoka na aibu.
Jamani UHUNI HAULIPI.
 
Ni ndefu, haichoshi, inasisimua na inafundisha. Mshikaji naona ameachiwa kilema cha maisha kwenye akili yake
 
Ndio wakome, ukimuona tu mdada mnaanza kupiga miruzi, hayo ndio malipo yake
 
kumcheka mwanadamu mwenzio ni sawa na kumkosoa muumba na pia elimu yake haimsaidii. kuheshimu kila mtu kuwatumia watu vizuri ndiyo siri ya mafanikio.wadau kazi kwenu
 
Back
Top Bottom