Tz boy 4tino
JF-Expert Member
- Sep 14, 2014
- 1,598
- 1,816
Wakati Watu wengi wakiamini sababu kuu ya vita Ethiopia ni ukabila, Jambo hilo siyo kweli.
Sababu kuu ya vita ya Ethiopia ni maslahi mapana ya mabeberu. Hii ni baada ya kutishika na msimamo wa Ethiopia haswa katika utekelezwaji wa miradi ya maendeleo.
Je, ni vipi Ethiopia inatishia maslahi mapana ya mabeberu?
Katika miaka ya karibuni Ethiopia imekuwa ikitekeleza miradi mikubwa ya maendeleo yenye malengo ya kunyanyua watu wake kiuchumi na kuwaondoa katika dimbwi la umasikini.
Baadhi ya miradi hiyo ni kama vile The Grand Renaissance Ethiopia Dam “Bwawa kubwa zaidi barani Afrika , na mabwawa mengine makubwa matatu ambayo yakikamilika yataifanya nchi hiyo kuwa na zaidi ya Mega Watts elfu kumi ( 10,000 MegaWatts ). Kwa lengo la ufafanuzi tu, Mega Watts 10,000 ni zaidi ya umeme unaozalishwa jumuiya ya Afrika Mashariki nzima.
Miradi mengine inayoendelea Ethiopia, ni uboreshaji wa miundombinu, special economic zones n.k.
Je ni vipi miradi hii inahatarisha maslahi ya mabeberu?
- Miradi hii itaenda kufanya asilimia mia ya wananchi wa Ethiopia kuwa na umeme, itaondoa utegemezi wa Ethiopia kwa nchi Za magharibi kwa kiwango kikubwa, unaenda kuifanya Ethiopia kuifanya Ethiopia kuwa huba ya viwanda vya kuongeza thamani hivyo kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu.
- Mbali na hayo jambo kubwa linalowaogopesha zaidi nchi za magharibi. Ni namna bwawa kubwa la Ethiopia linavyoweza kuwa msingi wa mapinduzi ya mikataba ya kinyonyaji iliyowekwa na wakoloni , ambayo iliwekwa kwa lengo la kuhakikisha nchi za kusini mwa jangwa la Sahara ( nchi za watu weusi) zinabaki masikini kwa kipindi kirefu.
Miongoni mwa mikataba hiyo ni mkataba wa matumizi ya Mto Nile, kwa muda mrefu nchi Za magharibi zimekuwa zikitumia mkataba huo kuhujumu miradi ya maendeleo katika nchi za Afrika Mashariki haswa inayohusiana na usambazwaji wa Maji na umeme.
Ushindi wa Ethiopia unaonekana waweza kuwa chachu ya mkataba huo kuvunjwa. Kwa ufupi mkataba huo unaipa haki Misri katika upangaji wa matumizi ya mto Nile pamoja na vyanzo vyake vyote jambo ambalo halina mantiki yoyote .
- Sababu kuu ya tatu ni namna utekelezwaji wa miradi mikubwa ya maendeleo nchini Ethiopia inavyotekelezwa. Wakati nchi nyingi Za Afrika hujikuta ikiingia mikataba isiyokuwa na tija, katika utekelezwaji wa miradi ya maendeleo. Mengine ikipelekea hata uuzwaji wa rasilimali muhimu katika mataifa yao. Hali ipo tofauti nchini Ethiopia, kwani nchini humo miradi mingi inamilikiwa na serikali ya nchi hiyo kwa kiwango kikubwa.
Kwa Ethiopia kutekeleza miradi mikubwa ya kiwango kile na mabeberu kutokuwa na chao katika miradi hiyo, ni jambo linalowakwaza sana na linaenda tofauti na maslahi yao mapana ambayo ni kuhakikisha wana udhibiti na nafasi katika miradi mikubwa ya maendeleo inayoendelea katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.
Tunapozungumzia nchi za Magharibi hapa tunamaanisha zote na haziishii kwa nchi zilizowahi kuwa na makoloni Afrika kama Uingereza, Ufaransa n.k. bali ni nchi zote za magharibi zina obligation ya kutekeleza hii ajenda.
Swala la nchi za magharibi kuhujumu maendeleo ya nchi kusini mwa jangwa la Sahara wala siyo siri na huko nyuma kabla ya maendeleo ya sayansi na teknolojia, hiyo mikakati walikuwa wakijadili wazi kwenye mabunge yao Ulaya.
Hizi ni baadhi tu ya sababu kwa nini ile vita ni zaidi ya wengi wafikiriavyo. Kwa ufupi tu , yote yanayoendelea nchini Ethiopia ni kutokana na tishiyo la maslahi mapana ya mabeberu, hamna swala ukabila/uonevu, wala bwawa la Ethiopia kutishia janga la upatikanaji wa maji nchini Misri. Zote ni propaganda.