Tambua kisha Thamini watu wa karibu na wa muhimu zaidi msimu huu.

WeedLiquorz

JF-Expert Member
May 30, 2022
3,273
5,441
Mzuka wana jf, Ahsanteni kwa hivi vimaua vyeupe mfano wa falling snow vimenishawishi kutupia bandiko.

Huu ndo ule msimu utatamani ujigawe mara kadhaa hautoweza...
Huu ndo ule msimu utajua unawaganda rafiki wenye rafiki zao hapa mjini.....
Huu ndo ule msimu utachagua kubaki town ule bata na wachumba wakati unategemea kuomba ada/msaada kijijini.
Huu ndo ule wakati mchepuko atakushika akili wakati mke na watoto wanabaki wapweke nyumbani.
Huu ndo ule msimu utajua unagongea demu ya wenyewe kwani hautozingatiwa.
Huu ndo ule wakati utamalizia pesa kidimbwi ukidai nakula mtaji nitajuaga kesho...

Asee nikwambie tu kesho siyo mbali, utavunja uaminifu kwa watu wa muhim ndani ya muda mchache sana wakati umejikaza mwaka mzima.

Ni msimu muhim sana ukichagua familia, ndugu wa karibu na watu wenye msaada mkubwa maishani mwako utoandoa lawama na aibu ndogo ndogo baada ya sikukuu hizi kuisha, hatujachelewa turudi nyumbani wazee.
 
Merry Xmas.
 

Attachments

  • Justin Bieber - Mistletoe (Official Music Video) ( 256kbps cbr ).mp3
    5.6 MB
Back
Top Bottom