Tambua familia bora inavyoishi

Marconho

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
288
444
1. Kwanza Baba ndiye kiongozi wa familia si babamkwe wala mamamkwe. Familia bora baba ndiye mwenye kauli ya mwisho si mama wala watoto. Kwenye familia bora baba anaheshimika na akiwa na heshima inavyostahiki pia familia hiyo inaheshimika na watu wote.

2. Pili familia bora mapato na matumizi ya familia hupangwa pamoja na hutumika vizuri kukidhi mahitaji ya familia.

3.Upendo na heshima ndio nguzo kuu katika familia bora maana kila mwanafamilia anatambua umuhimu wa yeye kuwepo kwenye familia hiyo.

4. Kila mwanafamilia anajua wajibu wake na majukumu yake ya kila siku. Baba kazini, mama kazini, watoto shuleni na house girl kupika, kufua na usafi wa nyumba na vyombo.
Nb. Waheshimuni sana na kuwalipa vizuri wasaidizi wa nyumbani maana na wao ni wanafamilia.

5. Ulinzi kwa watoto ni jambo la mhimu sana katika familia bora, na hii ni pamoja na kutambua mahitaji ya watoto na mazingira hatarishi kwa watoto.
Nb. Watoto huiga tabia za watu wanaokuwa nao karibu hivyo kuwa makini sana.

6. Afya na Usafi wa mwili pamoja na mazingira ndicho kitu kinachufuatia baada ya chakula bora katika familia.

7.Familia bora hupanga mipango ya maendeleo sio kuzua shida na matatizo kwa watu wengine na hujitahidi kuleta suluhu mapema kabla mzozo haujawa mkubwa na kwenda mbali.
 
Watu wengi walikuwa wanajua familia bora ni ile inayokula wali nazi,pilau au mboga saba kumbe kipato chochote kina kinafaa kuifanya familia iwe bora.
Namba moja kwangu imepwaya mke wangu anapenda kumsikiliza mama yake sana kuliko mimi.
 
Watu wengi walikuwa wanajua familia bora ni ile inayokula wali nazi,pilau au mboga saba kumbe kipato chochote kina kinafaa kuifanya familia iwe bora.
Namba moja kwangu imepwaya mke wangu anapenda kumsikiliza mama yake sana kuliko mimi.

Kweli kabisa
 
Back
Top Bottom