Tamasha la 18 la wiki ya usomaji na maonesho ya vitabu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamasha la 18 la wiki ya usomaji na maonesho ya vitabu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Gudboy, Oct 8, 2009.

 1. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  TAMASHA LA 18 LA WIKI YA USOMAJI NA MAONESHO YA VITABU
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Baraza la Maendeleo ya Vitabu Tanzania (BAMVITA) likishirikaiana na wadau mbali mbali hapa nchini na nje ya nchi limeandaa Tamasha na wiki ya usomaji wa vitabu kuanzia tarehe 13 hadi 17 Oktoba 2009. Tamasha hili litafanyika katika mikoa yote ya Tanzania. Kitaifa tamasha hili litafanyika katika jengo la “Ubungo Plaza”, mkabala na kituo kikuuu cha Ubungo cha mabasi yaendayo nje ya Dar es Salaam.


  Lengo kubwa la Tamasha ni kuhamasisha wananchi wa rika zote na hali zote za maisha kupenda kujisomea vitabu na kujenga utamaduni huo miongoni mwa jamii yetu. Kauli mbiu ya tamasha la wiki ya usomaji vitabu mwaka huu ni SOMA VITABU, UJIENDELEZE, UJIKOMBOE, na mwaka huu msisistizo ni kwa vitabu vya watoto.


  Inakubalika kote duniani kuwa nchi yoyote haiwezi kujikomboa wala kuendelea kama wananchi wake hawajengi tabia ya kujisomea vitabu kwa lengo la kuboresha maisha yao. Ukuaji wa haraka wa uchumi unatokana na kasi ya wananchi kuwa na tabia ya kujisomea, kupata elimu mpya na stadi mpya za kuwawezesha kumaliza shida zao. Inaeleweka kisayansi kuwa tabia ya kupenda kujisomea vitabu hujengeka nyumbani na shuleni, hasa watoto wakiwa bado na umri mdogo; na ndiyo maana mwaka huu tukaamua kuweka msisitizo kwenye vitabu vya watoto.


  Baadhi ya shughuli zilizoandaliwa kwa ajili ya tamasha hili ni Mahema ya Watoto na ya Watu Wazima ya kusomea vitabu; semina mbalimbali zitakazohusu masuala ya kuendeleza usomaji; mafunzo ya ukutubi kwa waalimu hamsini kutoka katika shule za msingi za Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, pamoja na kutoa zawadi za vitabu kwa shule hamsini pia za wilaya hiyo hiyo ya Mvomero. Pia kutakuwepo na maonesho ya vitabu yatakayofanyika katika jengo la Ubungo Plaza. Washiriki katika maonesho hayo ni wachapishaji na wauzaji vitabu toka Tanzania na nje ya nchi. Kutakuwapo pia matukio ya burdani kwa wale wote watakaohudhuria maonesho hayo.


  Taarifa hii ni kuwajulisha wamiliki na watendaji katika vyombo vya habari kuhusu Tamasha hilo la 18 la Usomaji wa Vitabu. Pia ni kuwataka wamiliki wa vyombo vya habari, wahariri na waandishi, kushiriki kikamilifu katika kutangaza tamasha hili na kuchochea wananchi waishio jijini Dar es salaam kwenda Ubungo Plaza kutazama vitabu na kushiriki katika matukio mengine yaliyoandaliwa kwa ajili yao. Tunaamini kwamba vyombo vya habari ni wadau muhimu katika kufanikisha azma ya tamasha hili. Tunaamini pia kwamba ni wajibu wa vyombo vya habari kushiriki katika kufanikisha tamasha hili kwani suala la usomaji linavihusu sana. Lengo ni kufanya suala la usomaji liwe la kitaifa na taasisi zote zenye vyombo vinavyoweza kuhamasisha usomaji zijipange vizuri na kulichukulia suala hili kama lao.


  Kwa kupitia kwenu na jitihada zingine zinazofanywa tutawafikia na kuwashirikisha viongozi wote wa wizara na idara za serikali, idara zinazojitegemea, taasisi zote za umma, asasi zote zisizo za kiserikali, mashirika ya dini, vyama vya wafanya kazi, vyama vya ushirika, vyama vya wafanyabiashara na mashirika ya misaada kutoka ndani na nje ya nchi katika kujenga taifa la watu wanaopenda kujisomea vitabu.


  Ni matumaini yetu kwamba vyombo vya habari vitatuunga mkono katika kufanikisha suala hili la kitaifa. Uongozi wa BAMVITA pamoja na wadau wote wanaounda baraza hilo wapo tayari kushirikiana nanyi ikiwa ni pamoja na kutoa maelezo ya ziada kama yatahitajika. Wakati wote tutakuwa tayari kushiriki katika kuandaa vipindi na makala mbalimbali pale tutakapotakiwa kufanya hivyo.


  Kwa mawasiliano na Kamati ya Maandalizi wapigie simu wajumbe wafuatao. Pia kwa maelezo zaidi nenda kwenye tovuti ya BAMVITA.


  Bi. Levina Oloo – Katibu Mtendaji BAMVITA 0762551649
  Bi. Hobokera Magale – Mratibu wa Tamasha 0754283866
  Bw. Abdallah Hassan – Mwenyekiti wa Tamasha 0754 263390 / 0715 263390


  Imetolewa na:


  Walter Bgoya
  Mwenyekiti, Baraza la Maendeleo ya Vitabu Tanzania (BAMVITA)
  Simu: 0784457457


   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Catch me some Agoro Anduru, if at all they are still in print.
   
Loading...