Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,438
Nilikuwa kwenye basi ni kutokea kwetu mkoa I juridical Dar risalama kibaruani. Pembeni yangu alikaa dada mmoja ana msambwanda mpaka nilimkumbuka shemeji yangu Behaviourist Kwakweki sikutaka kuongea kwani nilichoka sikupata usingizi vizuri. Tulipofika Segera alitaka machungwa kwakua nilikaa dirishani ilibidi tuvunje ukimya ndipo tuliopanza kuongea.
Alineleza jina lake akanieleza alivyotokea kunipenda tu. Aliniita dada.na alinipa story yake ya Maisha. Alipomaliza shule kuna Baba wa miaka 50+ alimtolea posa akaolewa. Baada ya harusi kufika kwa mume kila akibeba mimba ikifika miezi 6,7, au 8 zinaporomoka. Utajiri wa mume wake unaongezeka. Alijenga nyumba kwa Dar alikuwa na nyumba zaidi ya 20 anapangisha.
Baada ya miaka mitano ya ndoa bila mtoto, Shangazi yake alistuka. Alikwenda kwa wataalamu wa satellite kuangalia ndoa ya mwanae. Huko aliambiwa yule Baba anatoa watoto kafara ili utajiri wake uendelee. Kwakuwa mke wake alishakuwa mtu mzina, ilibidi mzee aoe damu changa ili aweze kutoa kafara yenye damu yake.
Kutoka kwa mune ilikuwa ni shughuli. Walikaa miaka miwili wakipigana makonbora. Mpaka mume amepata stroke ndiyo imekuwa nafuu yake kwani anajitibu yeye kwanza. Yule binti ameolewa na kijana mwenzake na wana watoto wawili. Biashara yake anapika mama lishe kwa sasa na ana furaha.