Tamaduni za kabila la wazinza zikoje

Masikio Masikio

JF-Expert Member
Apr 12, 2023
1,840
3,378
Kabila la wazinza lipo sengerema, geita na sehemu mbali mbali za kanda ya ziwa
Ambaye anazijua tamadun za kabila la wazinza naomba anijuze

Note: wale watukanaji na wale wenye stress huu sio uzi wa kumalizia stress zenu
 
Wazinza ni kabila la watu kutoka eneo la kusini-magharibi kwa Ziwa Viktoria na visiwa vya jirani, nchini Tanzania.

Mwaka 1987 idadi ya Wazinza ilikadiriwa kuwa 138,000 [1].

Lugha yao ni Kizinza.

Kazi yao ilikuwa uvuvi, ufugaji na uwindaji pamoja na kilimo. Kwa sasa wamejikita katika anga la wasomi maana wametapakaa kila taaluma na kila mahali.

Vyakula asilia wanavyovipenda[hariri | hariri chanzo]​

Wazinza walio wengi hupenda kula ugali wa mhogo, ndizi, samaki (hasa sato, sangara, mumi, kamongo, dagaa, mbete, nshonzi) na nyama.

Lakini pia kutokana na uhaba wa vyakula hivyo na mgawanyo wa makazi na kazi, Wazinza wamekuwa wakila vyakula vya aina nyingine nyingi. Mfano ni wali, ugali wa mtama, ugali wa mahindi, mboga za majani kama vile msusa, kisamvu, mchicha, n.k.

Vyakula asilia kama maboga, viazi vitamu, mihogo mitamu, kunde, maharage ni miongoni mwa vyakula muhimu sana kwa Wazinza

KWA HISANI YA WIKIPIDIA
 
Back
Top Bottom