Taliban hivi sasa wanaushambulia Mji Mkuu Kabul toka pande zote

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
7,312
10,493
Ni suala la muda tu, Kabul itakuwa chini ya udhibiti wa Taliban. Kinachoendelea ni mashambulizi makali kutoka kila upande wa mji. Kiongozi wa Taliban anasisitiza kuwa hataki umwagaji wa damu na anawaomba askari wajisalimishe. Majeshi ya Serikali kibao yanasalimu amri. Rais Ghan kabaki kutoa matamko ya kishujaa yasiyo na tija, kifupi anachezea kichapo!

Anga la mji limetapakaa helikopta za USA katikati ya moshi wa mizinga zikiwawahisha watu wake Uwanja wa ndege wa Kabul ambapo wanapakiwa kwa ndege then wanahama nchi.

NB: America Hana perment friend wala permanent enemy, akishachukua anachokitafuta anakuacha ujifie katikati ya maharamia!!!

FB_IMG_16290172751492400.jpg


Update: Serikali imesema wananchi wawe na Amani, mazungumzo yapo pazuri... Taliban wapo getini, wameambiwa wasishambulie bila ulazima

Update: Taliban wameukamata Uwanja mkubwa wa Ndege wa Bagram na gereza lenye wafungwa 5000

Taliban wameahidi kuwasamehe viongozi wote wa Serikali.

Bado askari wa Taliban wameamriwa kukaa getini mwa mji, wasiingie mjini mpk waambie.

Wanawake wameombwa na Taliban kwenda kujificha mahali salama.

Wanaotaka kuondoka Kabul wameruhusiwa kuondoka anytime bila bugudha.
 
Ni suala la muda tu, Kabul itakuwa chini ya udhibiti wa Taleban. Kinachoendelea ni mashambulizi makali kutoka kila upande wa mji. Kiongozi wa Taleban anasisitiza kuwa hataki umwagaji wa damu na anawaomba askari wajisalimishe. Majeshi ya Serikali kibao yanasalimu amri. Rais Ghan kabaki kutoa matamko ya kishujaa yasiyo na tija, kifupi anachezea kichapo!

Anga la mji limetapakaa helikopta za USA katikati ya moshi wa mizinga zikiwawahisha watu wake Uwanja wa ndege wa Kabul ambapo wanapakiwa kwa ndege then wanahama nchi.

NB: America Hana perment friend wala permanent enemy, akishachukua anachokitafuta anakuacha ujifie katikati ya maharamia!!! View attachment 1892975
US alikuwa anachukua kipi hapo Afghan!!
 
Ukweli mchungu ni kwamba kama Taleban itaichukua Afrighastan Marekani haipo salama.Afrighastan itakuwa ni makao makuu ya magaidi wote duniani.

Kwenye hili democratic wamefeli sana.Urusi ameshaizidi nguvu marekani.Republic wana kazi kubwa sana ya kuja kufanya katika foreign policy.
 
US alikuwa anachukua kipi hapo Afghan!

Hakukua na chochote alichochukua ilikuwa hasira tu ya ndege na balozi zake kupigwa. Siyo kila raia alipenda uwepo wa marekani sababu marekani naye aliua raia wengi sana kwa sababu tu za kisingizio cha taliban. Shida ni kuwa dunia haitakuwa salama kwa sababu dunia haitakuwa salama kwa sababu Afghanistan tayari ni makao ya magaidi i.e. ISIS, na wengine
 
Inasemekana Taliban wapo kwenye meza ya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa kijeshi ili wakabidhi mji kwa amani,pasipo umwagaji damu.tayari ndege ya kumbeba Raisi Ashraf Ghani ipo tayari na muda wowote kuanzia sasa ataondoka kwenye ardhi ya Afghanistan.

Baadhi ya viongozi wengine wakiwepo mawaziri washaondoka Afghanistan,wamekimbilia Pakistan.kwa iyo siku ya leo haiwezi kuisha pasipo Taliban kutangaza ushindi wa kuchukua Nchi.
 
Back
Top Bottom