`Talaka zisizotambuliwa na mahakama hazivunji ndoa` | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

`Talaka zisizotambuliwa na mahakama hazivunji ndoa`

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by paesulta, Feb 27, 2010.

 1. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Na Muhibu Said
  26th February 2010

  Serikali imesema talaka ambazo hazitambuliwi na mahakama, hazivunji ndoa iliyofungwa kwa vile chombo pekee chenye mamlaka ya kuvunja ndoa Tanzania Bara ni mahakama.

  Kaimu Meneja Msajili wa Ndoa na Talaka wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (Rita), Julien Mafuru, aliyasema hayo alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu Talaka katika semina ya mafunzo ya ndoa na talaka kwa viongozi wa dini na makatibu tawala, iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.

  Mafuru alisema miongoni mwa talaka, ambazo hazivunji ndoa iliyofungwa chini ya Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971, ni pamoja na “Talaka” zinazotolewa kwa msingi wa dini ya Kiislamu, ambazo kisheria zinaangaliwa kama ni nia ya kutoa Talaka.
  “Chombo chenye mamlaka ya kuvunja ndoa katika Tanzania Bara ni mahakama pekee. Baada ya kuvunja ndoa kisheria mahakama inatakiwa kuwasilisha nakala ya uamuzi ya kuvunja ndoa au kubatilishwa kwa ndoa kwa Msajili Mkuu wa Ndoa na Talaka kwa ajili ya kusajiliwa kwenye Daftari la Talaka na kutoa Hati ya Talaka au ubatilisho wa ndoa ambayo ni uthibitisho wa kuvunjika kwa ndoa,” alisema Mafuru.

  “Kwa waumini wa Kiislamu, Talak zitolewazo kwa msingi wa dini ya Kiislamu huwa hazivunji ndoa iliyofungwa chini ya sheria ya ndoa. Talaka za jinsi hii kisheria zinaangaliwa kama ni nia ya kutoa Talaka.

  Hiyo mhusika hutakiwa kufungua dai lake la kuomba talaka mahakamani na kutumia “Talaka” aliyopewa kama ushahidi wa kuthibitisha kuwa ndoa inayohusika imevunjika pasipo kurekebishika. Mahakama hupokea ushahidi huu na kutamka kuvunjika kwa ndoa,” aliongeza.

  Hata hivyo, alisema pamoja na matakwa ya sheria, mahakama zimekuwa haziwasilishi nakala za maamuzi ya kuvunjika kwa ndoa au kubatilishwa kwa ndoa kwa Msajili Mkuu wa Ndoa na Talaka.

  Alisema hali hiyo imekuwa ikiwalazimu wahusika wao wenyewe kuwasilisha nakala za kuvunjika kwa ndoa, hasa pale wanapokuwa na wana madai ya haki fulani, kama vile wanapotaka kufunga ndoa nyingine na wenzi wao.

  “Hii imechangia kukosa kumbukumbu sahihi kwa ndoa zilizovunjika/batilishwa, kwa sababu si wanandoa wote ambao ndoa zao zimevunjwa huwasilisha nakala za uamuzi wa kuvunjika ndoa zao kwa Msajili Mkuu wa Ndoa na Talaka,” alisema Mafuru.

  Alisema baadaye mahakama itatoa uamuzi, ambao mhusika atatumia kusajili maamuzi ya kuvunjika kwa ndoa yake kwa Msajili Mkuu wa Ndoa na Talaka wa Rita, ambapo huo ndio utakuwa mwisho wa ndoa husika.

  Alielezea hatua za kufuata wakati wa kuomba Talaka na kusema kwamba, mwenye nia ya kuomba ndoa yake ivunjwe anatakiwa kupeleka malalamiko ya matatizo yake ya ndoa kwenye Baraza la Usuluhishi wa Ndoa la Kamishna wa Ustawi wa Jamii au Baraza la Ndoa lingine lolote linalotambulika kisheria, kama vile Baraza la Kata, kanisani au Bakwata.

  Kaimu Meneja Msajili wa Ndoa na Talaka wa Rita alisema Baraza la Usuluhishi la Ndoa litasikiliza malalamiko husika na kama litashindwa kuwasuluhisha wanandoa husika, litaandika hati maalum kwenda mahakamani likielezea mgogoro huo kwa ufupi na kutoa maoni yake kuhusu suala walilosikiliza.

  Mafuru alisema walalamikaji/mlalamikaji atapeleka hati hiyo mahakamani kwa ajili ya kufungua shauri lake la kuomba ndo ivunjwe kisheria na haki zake nyinginezo kutamkwa mahakamani.

  Alitaja faida ya kusajili Talaka kuwa ni pamoja na kuwezesha kupata hati ya Talaka, ambayo ni uthibitisho wa hali ya ndoa ya mhusika, kumwezesha mtalikiwa kupata haki ya kuoa au kuolewa tena na mtu mwingine, kuwezesha umma kujua kuwa ndoa imevunjika, kulinda mali ya mtalikiwa endapo atafariki mwenzie wa zamani kutaka kudai urithi na kupata takwimu za ndoa zinazovunjika na wapi zinatokea.

  Awali, Msajili Msaidizi Mkuu wa Ndoa na Talaka wa Rita, Theophil Rugonzibwa, akiwasilisha mada ya ndoa katika semina hiyo, alisema kisheria ndoa haifungishwi nyumbani, bali katika sehemu za wazi, kama vile makanisani na misikitini na kwamba, anayetaka kufungisha nyumbani, lazima apate kibali cha serikali.

  Pia, alisema Rita “ndoa” ya mwanamke na mwanaume wanaodaiwa kuwa ni mume na mke kwa vile tu wameishi pamoja kwa kipindi cha miaka miwili.

  “Hata waishi miaka mia moja, huwa si ndoa hiyo na wala hatuisajili. Ndoa ni ile inayofungishwa,”
  alisema Rugonzibwa.

  Naye Mwakilishi kutoka Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania (Baraza Kuu), Sheikh Kondo Juma Bungo, alisema Waislamu hawaungi mkono utaratibu wa kumtaka mwanaume anayetaka kufunga ndoa ya wake wengi, lazima mke aliyetangulia akubali akisema kwamba, utaratibu huo unapingana na maumbile na mafundisho ya dini ya Kiislamu.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hivi inakuwaje pale talaka mmoja anapokuwa anataka talaka na mwengine hataki hasa pale ambapo mwanaume ana issue talaka lakini mwanamke hataki? Wakifika kwa msajili je mwanamke ataulizwa kama anakubaliana? Na kama ndivyo vipi akikataa?
   
 3. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu ndio maana wanataka kadhi ili kuendeleza TALAKA REJEA.

  Sasa sijui ni chombo gani Tanzania chenye mamlaka ya juu, Religious institutions au Serikali. lol

  Itakuwa patashika watakapo pewa Mahkma ya kadhi. Sawa na Odinga kufukuza kazi KIBAKI kurudisha. Mungu apitishie mbali.
   
 4. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ....well,i hope hii haita-turn into malumbano ya kidini.
  Kikubwa ni kuwa hii inatugusa wote,kwani mara ngapi tumeona watu wanaachana bila kuweka kumbukumbu officially popote pale?na mbaya zaidi ni kuwa baada ya hapo hawajui hata status yao ikoje,kwa hiyo si suala la waislamu au wakristu au wapagani,bali ni swala linalohusu watanzania wote wa kawaida ambao wengi hawajui majukumu wala haki zao kisheria.....!
   
 5. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ahaa!!! Kuna jamaa Muislam ameooa mke ambaye alikuwa mke wa mtu na jamaa hajampa talaka sasa hii inakaaje wandugu. Jamaa alizaa naye alikini ndo hivyo tena na Jamaa hana kumbukumbu yoyote sasa nisaidieni wandugu
   
 6. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,816
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  usaidiwe we ndiye huyo jamaa nini?
   
 7. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hivi nini kinasababisha mpaka mpeane talaka?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...