TALA yakimbia Tanzania, yafunga ofisi zake

DAR ES SALAAM,TANZANIA.


Kampuni ya TALA inayokopesha kwa njia ya mtandao wa simu za kiganjani, imetangaza kufunga shughuli zake Tanzania.
Imetoa taarifa hiyo leo Jumanne Septemba 17, 2019 na kubainisha kuwa maelezo ya kina kuhusu uamuzi huo yatatolewa hivi karibuni.
Kampuni hiyo inayoendeshwa na teknolojia ambayo kwa sasa inafanya kazi nchini Kenya, Mexico, India na Ufilipino hutoa mikopo ya haraka, na binafsi kwa wakopaji na kuvutia zaidi ya watu milioni 27 duniani.
"Tunakujulisha kuwa kwa sasa TALA haitoi mikopo nchini Tanzania. Tunathamini nafasi ya kukutumikia na tunatamani wateja wetu waaminifu waendelee na mafanikio katika safari yao ya kifedha, "inasomeka taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo.
Akizungumza na Mwananchi kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Facebook, mmoja wa maofisa wa kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Kelly amesema, "Ndio, hatujatoa mikopo tena nchini Tanzania. Kwa bahati mbaya, kwa sababu za kisheria hatuwezi kusambaza habari nyingine yoyote isipokuwa ile iliyosambazwa kwenye mtandao wa kijamii.”
Ripoti ya kampuni hiyo mwaka 2018 inaonyesha kuwa katika nchi za Afrika Mashariki asilimia 78 ya mikopo hutumiwa kwa biashara, asilimia 32 ya wateja wake wakiwa wanawake na wanaume, kati yao asilimia 68 wana umri chini ya miaka 34.


Credit : Mwananchi
 
Attitude za wateja zimetufikisha hapa. Some of us had no reason to face such consequence.
 
Hakuna shaka nafasi yao imechukuliwa na wachina , walianza kwa kishindo kugawa hela uwanja wa Taifa , wala hawataki riba
 


... katika nchi za Afrika Mashariki asilimia 78 ya mikopo hutumiwa kwa biashara, asilimia 32 ya wateja wake wakiwa wanawake na wanaume, kati yao asilimia 68 wana umri chini ya miaka 34.

Chanzo: Mwananchi

"Asilimia 32 ya wateja ni wanawake na wanaume"

Kwa hiyo asimilia 68 ya wateja ni watu wa jinsia mseto, transgender.
 
Na hivi tunaelekea kwenye uchaguzi wasitubugudhi na sms zao za vitisho haya makampuni ya wanyonyaji tutawashitaki kwa baba awachinjie baharini.....;););)
 
Back
Top Bottom