TIQO , I hope your not joking!
Nikitumia simple mathematics naona kama una fanya kichekesho fulani hivi hapa JF!.
Bunge la Tanzania lina jumla ya wabunge 231 na pia Tanzania ina jumla ya madiwani 4,453.
Nikiziangaliaa takwimu zako kama unavyotaka kubainisha kwenye msingi wa hoja yako, Tokea mwaka 1995 mpaka mwaka 2010, CHADEMA imekuwa ikipata wastani wa wabunge 15 kati ya 231 katika chaguzi kuu tatu za Taifa. Huku pia ikipata wastani wa madiwani 156 kati ya madiwani 4,453 wa Tanzania.
Simple equation, kama hiyo idadi utajumlisha na pia ukaangalia multiplier effect utakuwa unaleta kichekesho ukidai kwa takwimu hizi kama CHADEMA itakuwa chama tawala kwa idadi ya wabunge na madiwani.
Kwa takwimu hizi kama zitasimama zilivyo, CHADEMA come 2016 itakuwa na wabunge 63 out of 231 na pia itakuwa na madiwani 623 out of 4,453 but if, takwimu zako unataka zisimame kama upendavyo.
Kwa mtiririko huu, CHADEMA haitapata hata nusu ya wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano la 2016 ili tuanze kufikiria uwezekano wa kuwa na nguvu bungeni katika upitishwaji au kutopitishwa kwa sheria mbali mbali bungeni.
Kwa mtaji huu, CHADEMA has a long walk to ruling party.