Takwimu katiba pendekezwa pasua kichwa

Takwimu katiba pendekezwa pasua kichwa

SOTI

Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
79
Reaction score
22
Kwa aliyefuatilia mjadala HotMix EATV ataamini kuwa kuna uchakachuaji wa hali ya juu kuhusu idadi ya wajumbe. Takwimu zilizo kwenye katiba zinaonesha Zanzibar wajumbe 212 na Bara 416 jumla 628. 2/3 ya zanzibar kwa takwimu hizi ni wajumbe 142. Siku ya kutangazwa matokeo tuliambiwa na katibu wa bunge kuwa Zanzibar ni 219 ambapo 2/3 ni 146 wakati bara ilikuwa 411 jumla 630. Kumbuka mwanzoni idadi ilikuwa Zanzibar 210 na Bara 419 jumla 629. Waliopewa jukumu la kudanganya umma wamefanya kosa kubwa sana kushindwa kuweka sawa takwimu. Kwa takwimu hizi hata kama haujui statistics ni dhairi tumedanganywa lakini Mungu Kawaumbua.
 
Haramia Sita na genge lake siku za kueateketeza zinakuja
 
Ngoja aje chabruma apa maana nilimuona pale EATV
 
Kwa aliyefuatilia mjadala HotMix EATV ataamini kuwa kuna uchakachuaji wa hali ya juu kuhusu idadi ya wajumbe. Takwimu zilizo kwenye katiba zinaonesha Zanzibar wajumbe 212 na Bara 416 jumla 628. 2/3 ya zanzibar kwa takwimu hizi ni wajumbe 142. Siku ya kutangazwa matokeo tuliambiwa na katibu wa bunge kuwa Zanzibar ni 219 ambapo 2/3 ni 146 wakati bara ilikuwa 411 jumla 630. Kumbuka mwanzoni idadi ilikuwa Zanzibar 210 na Bara 419 jumla 629. Waliopewa jukumu la kudanganya umma wamefanya kosa kubwa sana kushindwa kuweka sawa takwimu. Kwa takwimu hizi hata kama haujui statistics ni dhairi tumedanganywa lakini Mungu Kawaumbua.
Ni nani hao waliopewa jukumu la kudanganya ndugu yangu?
 
Ukweli uko wazi kwamba takwimu zimechakachuliwa. Tatizo ni kwamba hawa jamaa walidhamiria kupata 2/3 ya Zanzibar kwa namna yoyote ile kiasi kwamba hata hawakujali kwamba watu wataona mkanganyiko huo wa idadi ya wajumbe. Nahisi wameshaona kuwa watanzania wote ni 'viazi'kwa hiyo hawawezi kuona hata jambo la wazi kama hilo. Kifupi inaonyesha kuwa kuna wajumbe kama saba hivi 'wamevuka bahari' kwenda Zanzibar tokea Bara. Mmoja tumeshaambiwa ni Zakia Meighji. Bado tunasubiria wengine, tutawapata tu na majina yao.

na kwa wale wapenda katiba pendekezwa waliozoea kushabikia na kutetea, hoja kama hii wala hauwaoni maana masuala hayo ya mkanganuiko wa takwimu kuna ambao nimeshawauliza lakini wanakimbia mbio kwa sababu ni hoja nzito ambayo uongo uliozoeleka hauwezi kutumika kuitetea.
 
Mzee sita kwa hili kachemka sana.Nimemuona chabruma alivyobanwa hadi kawa mkali
 
Back
Top Bottom