Takwimu haziongopi mwisho umekaribia.

Takwimu haziongopi mwisho umekaribia.

Uchaguzi wa siku mmoja ndiyo utakaoleta viongozi wa miaka mitano na ndiyo watakaoathiri maisha yetu ama kwa njia chanya au kwa njia hasi! Halafu mbona CCM ndiyo wao kila siku wanasema kwamba mwaka 2020 John Magufuli lazima atashinda tena!
Naona kamanda hujakata tamaa na siasa za majitaka zetu za upinzani. Hahahah. Kazi unayo. Hivi unajipangaje kuwatumia watuhumiwa wa ufisadi katika kugombea urais kwa mara nyingine 2020. Umejipanga na ajenda gani this time. Maana ajenda za mafisadi mliziulia mbali kule. Wote tukaambiwa we must SHUT UP mouth.once and forever
 
Hizo takwimu zako siyo za kweli, 1995 Mkapa hakufikisha 85% isitoshe umeweka namba tu kwamba 2015 CCM ilipatata 57% lkn hausemi CCM ilishinda kwa tofauti ya Asilimia ngapi, hiyo ndiyo muhimu, kwa taarifa yako 2015 CCM ilishinda kwa tofauti ya kura Milioni 2 au tofauti ya 20%, sasa hii ni tofauti kubwa sana kuweza kusema ulivyosema kwamba mwisho wa CCM umekaribia, vyama ambavyo husema hivi huwa vinashindwa kwa tofauti ya labda ya kura kama 5000 hivi lkn CCM inashinda kwa tofauti ya kura Milioni 2 hlf unaongelea mwisho wa CCM? Ingekuwa CCM ilishinda kwa tofauti ya < 5% hapo sawa lkn 20% hilo pengo ni kubwa sana kuweza kuzibwa ndani ya miaka 4, unahitaji miaka 20 au chaguzi kuanzia 4 zijazo na Upinzani wamaintain trajectory waliokuwa nayo 2015 ili kuweza kusawazisha hiyo tofauti!

Usisahau chaguzi za Kata kati ya Kata 20 CCM inashinda Kata 19 na hii ni mwaka mmoja baada ya Uchaguzi Mkuu 2015, sasa utaona hakuna dalili kwamba mwisho wa CCM umekaribia,...
Vijana WA Chadema hawatakuelewaaa
 
CCM kupata chini ya 50% hilo halimaanishi wapinzani wataongoza.

Kama wapinzani wapipojipanga kuungana, CCM wanaweza kukosa 50% na wapinzani pia wasipate 50%, mfano, mgawanyikowa 40% CCM, 30% chama kimoja cha upinzani, 20% chamakingine cha upinzani, na vingine vya upinzani vikagawana 10%.

Hapo vipi?
 
Hivi nyie watu wa CCM ni lazima muongope kwenye kila jambo. Ukisikia asilimia maana yake ni kwamba hizo takwimu zinatokana na mia. Sasa 57 inayotokana na mia si lazima inayobakia ni 43? sasa ukitaka kupata tofauti unafanyaje kama si kutoa 57 kwa 43? Sasa 57 toa 43 unapata 20 na siyo 14? Tofauti kati ya CCM na wapinzani wake mwaka 2015 haikuwa 20% bali 14%
Ok hapo kamanda baada ya kurekebisha hiyo, then, whats next.si bado zile zile milioni 2 zinasimama ?
 
Kwanza Babeli mimi hakuna mahali nimesema kwamba CCM haikupewa kura milioni mbili zaidi ya wenzao. Bali Mwenzako Barbarosa alikuja na hoja kwamba CCM ilishinda kwa zaidi ya asilimia ishirini. Nilikuwa namrekebisha asipotoshe watu kama mleta bandiko ambaye ameandika takwimu baadhi zisizo sahihi.

Kinachonishangaza eti Barbarosa anasema tofauti hiyo ni kati ya UKAWA na CCM kama vile ni vyama hivyo tu ndivyo vilipigiwa kura kwenye uchaguzi wa Mwaka 2015. Huwezi kusema CM ilishinda kwa zaidi ya asilimia 20, labda angesema CCM iliizidi UKAWA asilimia 20 na siyo kusema kwamba CCM ilishinda kwa asilimia zaidi ya 20.

Halafu mimi bwana Babeli sina siasa za maji taka. Hizo wanazo CCM na msemo huo ulianzishwa na Marehemu Samuel Sitta dhidi ya wana CCM wenzake. Yule aliyesema kwamba watu wana wivu wa kike unajua alikuwa anawaambia wana CCM wenzake? Nyie watu mna maneno kama wazaramo!!
 
Habari wanajamvi!
Naam! Ndivyo unavyo weza kuhitimisha kusema mwisho wa enzi wa CCM kutawala umekaribia kama ukitafsiri takwimu hizi mwelekeo wake. Hakika muda siyo mrefu matarajio ya watanzania yatatimia.Angalia kwa makini ninacho maanisha nikiziangalia takimu hizi toka uchaguzi wa vyama Vingi unipolar anza mwaka1995!
. 1995 CCM ilipata asilimia 85 ya kura zote za urais
. 2000 CCM ikapata asilimia 80 ya kura zote za urais
. 2005 CCM ikapata asilimia 75 ya kura zote za urais
. 2010 CCM ikapata asilimia 64 ya kura zote za urais
.2015 CCM ikapata asilimia 57 ya kura zote za urais.
Ukiangalia takwimu hizi ni dhahiri upinzani unazidi kuimarika kisiasa, kiuchumi, kiuzoefu na kimbinu.Uchaguzi wa mwaka 2020 upinzani hususan UKAWA mtu yeyote atakae pambana na Mheshimiwa Magufuli lazima UKAWA WASHINDE! Sababu ni nyingi sana lakini kubwa ni hizi zifuatazo.
Kwa kipindi kifupi alicho tawala Magufuli hakika wananchi wamekatishwa tamaa na namna anavyo endesha Nchi. Uchumi umeyumba sana kiasi kwamba watu wa chini wamekutana na ugumu wa maisha usio wa kawaida.Akiendelea hivi mpaka 2020, upinzani wanachukua Nchi saa nne asubihi.
Magufuli ni mbinafu na mwenye upendeleo ulio wakera watu wengi. Hakika unaweza kusema hii ni zama ya wakristo! Katika teuzi zake, katika kila kumi anao wateua watu 7-9 ni wao! Mbaya zaidi ni wasukuma au kabila jingine lakini wa kanda ile pendwa. Jambo hili pia limewaudhi wengi hata wakristo wenyewe.
Magufuli hashauriki! Anacho taka yeye ndicho hufanyika hata kama kitaleta madhara kwa Chama, serikali au Nchi kwa ujumla.mfano mpango wake wa kutaka kuzuia vyuo vikuu vya binafsi na vya mashiriika ya kidini siyo tu utapunguza ajira lakini pia una Malengo yenye mashaka.Mpango huu utainyima CCM kura nyingi.
Mipango mingi miovu hajapata kuikemea hivyo kuzua minong'ono kwa huenda ina baraka zake.Lipumba kupewa fedha ya CUF wakati siyo kiongozi na hajashitakiwa inaleta maswali mengi kuliko majibu. Kupotea kwa Ben Saanane na serikali kukataa kuleta wataalamu waliobobea kuja kumtafuta pia kunaacha viulizo vingi.
Binafsi naomba aendelee hivi hivi ili mpango wa Mungu utimie 2020
Hoja ya kipumbavu na kilofa sana. UKAWA washinde 2020 kwa Mgombea gani waliyenaye?
 
Fanya kazi unawaza uchaguzi wa siku moja ,siasa afrika kweli ni hasara baada ya kujenga nchi wewe 2017 unaota uchaguzi
nchi gani ya kujenga labda bangi ccm si mulikuwa pekeyenu na hamukufamya lolote la maana
 
Back
Top Bottom