TAKUKURU yawasaka wamiliki wa Kampuni ya MEIS Industries kwa tuhuma za kutoroka na mabilioni

Kwa nini unauhusisha udhalimu mkubwa kiasi hiki, na CCM ?
Umefanya utafiti wowote ?Hata hivyo, mimi napita tu, tungoje wenyewe wanakuja, ikidhibitika kama hayo ni kweli, nitakuheshimu sana.
Kwasababu CCM na upigaji hela ni kama pete na kidole. Na jinsi jiwe ana roho mbaya na wapinzani asingewapa wapinzani. Hao ni CCM 100% ndiyo wamepewa wakamilishe sera yao ya viwonder
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nchini Tanzania inawatafuta wamiliki wa Kampuni ya Meis Industriesltd inayodaiwa kutoroka na mkopo wa fedha kiasi cha Sh46 bilioni kwa ajili ya kujenga kiwanda cha saruji mkoa wa Lindi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Juni 18,2019 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo amesema wamebaini kampuni ya Meis ilikabidhiwa fedha hizo kama mkopo mwaka 2011 kutokana na sehemu ya fedha za uwekezaji zilizotolewa na Serikali ya Libya kwa Serikali ya Tanzania.

"Mwaka 2009 Serikali zote mbili zilisaini mkataba wa nyongeza ambao uliitaja kampuni ya Meis kama kampuni itakayopewa kiasi cha dola 20,000,000 kwaajili ya uwekezaji wa ujenzi wa kiwanda cha saruji eneo la Machole Mkoani Lindi,” amesema Brigedia Mbungo.

Amewataja wahusika wa kampuni ya Meis ambao hawajapatikana na wanaendelea kutafutwa ni Islam Balhabou, Merey Awadh Saleh, Sabri Kuleib na Abdallah Bin Aliya.

Brigedia Mbungo amesema mwenye taarifa ya watuhumiwa hoa awasiliane na Takukuru ili kuweza kuwakamata na kuja kujibu tuhuma zinazowakabili.
Lolote linaweza kusikika huko Lindi kuchele kwenye " mawindo" ya Chadema!
 
Yaani hela zinatolewa kihohela au habari haijakamilika
Unatoa bila insurance au makubaliano yoyote?
Kama zinatoka hivyo naona tutaibiwa sana
 
Kwani wamiliki wa hii kampuni ni wa Tz?....ila all in all pamoja na kumuweka mwanajeshi watu wanakula rushwa bila woga hii hatari sana aisee
Walipewa pesa hiyo mwaka 2011,kipindi hicho unadhani huyu mwanajeshi alikuwa takukuru au?kwa kifupi hii hela ilipigwa enzi za JK
 
WATAFUTWA NA TAKUKURU KWA TUHUMA ZA KUTOKA NA SHILINGI BILIONI 46: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imetangaza kuwatafuta wamiliki wa Kampuni ya MEIS INDUSTRIES LTD inayodaiwa kutoroka na mkopo wa dola za Marekani 20,000,000 sawa na Shilingi za Kitanzania bilioni 46 kwa sasa walizokabidhiwa kwaajili ya kujenga Kiwanda cha Saruji mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa taarifa ya TAKUKURU Kampuni hiyo ya MEIS ilikabidhiwa kiasi hicho cha fedha kama mkopo wa mwaka 2011kutokana na sehemu ya fedha za uwekezaji zilizotolewa na Serikali ya Libya kwa Serikali ya Tanzania.

FB_IMG_1560869020251.jpg
FB_IMG_1560869018429.jpg
FB_IMG_1560869016421.jpg
i
 
WATAFUTWA NA TAKUKURU KWA TUHUMA ZA KUTOKA NA SHILINGI BILIONI 46: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imetangaza kuwatafuta wamiliki wa Kampuni ya MEIS INDUSTRIES LTD inayodaiwa kutoroka na mkopo wa dola za Marekani 20,000,000 sawa na Shilingi za Kitanzania bilioni 46 kwa sasa walizokabidhiwa kwaajili ya kujenga Kiwanda cha Saruji mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa taarifa ya TAKUKURU Kampuni hiyo ya MEIS ilikabidhiwa kiasi hicho cha fedha kama mkopo wa mwaka 2011kutokana na sehemu ya fedha za uwekezaji zilizotolewa na Serikali ya Libya kwa Serikali ya Tanzania.
😬😴
 
Back
Top Bottom