TAKUKURU yataka mahakama yake

TAKUKURU yataka mahakama yake

Sumasuma

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2011
Posts
342
Reaction score
110
MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Dk. Edward Hoseah, amemuomba Jaji Mkuu, Othman Chande, ili kesi zinazohusiana na rushwa ziwe na mahakama yake.

Dk. Hoseah alisema kuwa kama angekuwa na uwezo angeanzisha mahakama maalumu inayoshughulikia kesi za rushwa pamoja na majaji waliobobea katika masuala hayo ili kumaliza tatizo hilo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika mafunzo ya walezi na wenyeviti wa klabu za wapinga rushwa, alisema kuwa katika maoni yake kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba amependekeza hivyo ili udhaifu unaoonekana kwa TAKUKURU sasa usionekane tena.

"Natamani TAKUKURU iwe na mamlaka ya kushitaki na tukipewa mamlaka hiyo nakuhakikishia rushwa zitapungua lakini sasa mwenye mamlaka ni DPP (Mkurugenzi wa Mashitaka)," alisema.

Dk. Hoseah pia alisema kuwa kuna haja ya kuangalia mfumo uliopo na kuuboresha ili uwafaidishe Watanzania katika uchukuaji wa hatua.

"Kubadilisha mfumo na kuuboresha si dhambi, unajua wenzetu wanatuzidi kwa sababu ya mfumo wao wa kiutawala, hasa katika haya masuala ya rushwa kila nchi ina namna inavyojiendesha," alieleza.

Pia alisema kuwa kwa sasa Tanzania ipo katika nafasi ya pili kwa nchi za Afrika Mashariki na kwa Afrika inakamata nafasi ya 12 katika mapambano dhidi ya rushwa.

Akizungumzia lawama zinazoikumba TAKUKURU kwa baadhi ya maofisa wake kutokuwa waaminifu, Dk. Hoseah alitaka Bunge au Ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) kuichunguza TAKUKURU kama ina watu wachafu, alidai kuwa anachoamini ina watu wasafi.


[TD="bgcolor: #ffffff"]
na Happiness Mnale

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][/TD]
source: Tanzaniadaima
 
kwa nini anaogopa kusema mkurugenzi wa takukuru asiteuliwe na rais naofisi isiwe chini ya ikulu?tatizo la katiba ya sasa rais anaogopwa kama Mungu.
 
Hili ni pendekezo la kwanza la maana kabisa ambalo Dk. Hoseah amepata kulitoa tangu akiwa kwenye nafasi hiyo. Mahakama aliyopendekeza ni muhimu sana.

manyerere
 
Hili ni pendekezo la kwanza la maana kabisa ambalo Dk. Hoseah amepata kulitoa tangu akiwa kwenye nafasi hiyo. Mahakama aliyopendekeza ni muhimu sana.

manyerere

Hiyo ni geresha tu na danganya toto...

Hawa jamaa wanongoza kwa kushindwa kesi mahakamani maana wanachukua rushwa hadi kwa watu waliowashtaki wao wenyewe halafu wanaharibu ushahidi makusudi
 
Kwa hiyo Hosea anataka kuwaambia Watanzania tatizo la rushwa au/na utendaji mbovu wa TAKUKURU ni kwa sababu TAKUKURU haina mahakama yake?

Bwana Hosea anakumbuka nukuu zake Wikileaks?
 
Back
Top Bottom