TAKUKURU yashikilia wanafunzi 13 wa IRDP kwa rushwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma inawashikilia wanafunzi 13 wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa na udanganyifu wa mitihani ya marudio.

Akitoa taarifa ya utendaji wa taasisi ya robo ya tatu ya mwaka, kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka huu, mkuu wa Takukuru mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo alisema wanafunzi hao wa mwaka wa tatu 2020 wanashikiliwa kwa kufanya udanganyifu katika mtihani wa marudio somo la Applied Statistics II uliyofanyika Novemba mwaka jana kwa mwaka wa tatu.

Uchunguzi wa awali uliofanywa na taasisi hiyo unaonesha kwamba wanafunzi hao walitumia rushwa kupata mitihani hiyo ili warudie nje ya chumba cha mitihani karibu na chuo hicho.

Baada ya kufanya mitihani hiyo nje ya chumba cha mitihani karibu na chuo hicho, wanafunzi hao walijaribu kuingiza katika mfumo rasmi karatasi za matokeo walizotumia kujibia mitihani hiyo ndipo chuo kikabaini ujanja huo na kuripoti Takukuru.

"Wanafunzi hao walitaka kuingiza makaratasi ya mitihani hiyo kwenye mfumo rasmi wa matokeo ya chuo kwa kuchomoa karatasi walizofanya kwanza, ndipo chuo kikabaini na kuripoti Takukuru," alisema Kibwengo.

Kibwengo alisema, kutokana na tuhuma hizo wanazokabiliwa nazo wanafunzi hao, TAKUKURU inawatafuta waliomaliza masomo yao miaka ya nyuma lakini wapo mazingira nje ya chuo. Aliwataja wanafunzi wawili kuwa wanaonekana ndio viunganishi wa mbinu hizo.

Alisema wanafunzi hao wanatakiwa kuripoti mara moja katika ofisi za TAKUKURU mkoani Dodoma kwa ajili ya kusaidia uchunguzi wa nani alitoa mitihani chuoni hapo kwa wanafunzi hao.

Alisema Takukuru inaendelea na uchunguzi kubaini mitihani hiyo waliipataje na kama kuna walimu wanahusika na mbinu hizo.

Alisema uchunguzi ukikamilika TAKUKURU itawafikisha mahakani wahusika wote katika sakata hilo la kufanya udanganyifu katika mitihani vyuoni.

Vile vile, katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka jana, Takukuru ilipokea malalamiko 178 ya rushwa na makosa yanayohusiana na hayo.

Serikali za mitaa zinaongoza kwa kuwa na malalamiko asilimia 23, mikopo umiza na sekta binafsi asilimia 20, ardhi asilimia 14, vyama vya siasa na uchaguzi asilimia sita na afya yote asilimia sita.

Katika kipindi hicho, Takukuru imefanya uchunguzi wa majalada 16 na kukamilisha. Pia mashauri 13 yamefunguliwa mahakamani. Aidha, mahakama ilitoa uamuzi katika mashauri 12 ambayo jamhuri imeshinda 10 na kushindwa mawili.
 
Nilivyoelewa mimi ,walifanya paper tayr zikakusanywa ,wakapata paper baada ya mtihani wakajaza majibu sahihi ,wakataka wachomoe zile walizofanya mwanzo waweke hizi za pili walizofanyia nje ili ndo zisahhishwe
 
Vyuo vingine udandara mtupu.

Issue kama hiyo unaanza kukimbizana na wanafunzi wako Takukuru si ujuha huo
 
Kwenye vyuo serious ukikamatwa na kosa la kuibia mtihani shule inakoma hapo hapo na mara nyingi ni vigumu hiyo mitihani kuvuja. Ni bora vyuo vitafute namna bora ya kuthibiti mitihani ili vilaza ambao wamesheni kila aina ya mbinu kwa sababu wako tupu kichwani wakose mpenyo wa kuingia kwenye sekta muhimu na kuvuruga mambo..
 
Hapo ishu sio wanafunzi kuna ugali wa mtumishi unatafutwa. Nadhani huko aliko atakuwa anajiharishia.

Ila hawa wanafunzi nao vilaza applied statistics inatoa mtu jasho mpaka anaingia na booklet yenye majibu
Mijinga sana hiyo mianafunzi. Paper unasolve nje unaingia na majibu kichwani.

Hicho chuo kimeoza. Kama wanafunzi hata maswali ya Standard Deviation, Range, mode na median hawawezi.
 
Ni mifumo mibovu tu ya vyuo vyetu, na vyuo vingi sana hata Tz vina shida hii, utakuta mwalimu anafelisha kwa makusudi ili atunge mitihani ya marudio kwa sababu tu kuna hela wanalipwa! Kuibiwa mtihani yawezekana kunasababishwa na mifumo ya Professor anatunga mtihani badala ausimamie mwenyewe na kuwapa wanafunzi wake, kinachofanyika mtihani unapelekwa kwenye pool ambapo unashikwa na watu wengi mpaka na wenye tamaa ya kupiga, na mifumo hii ndiyo inayodhoofisha elimu yetu kwenye vyuo vingi nchini
 
Back
Top Bottom