TAKUKURU yaokoa zaidi ya Bil 11.3 kwenye vyama vya Ushirika

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA



TAARIFA KWA UMMA


IMETOLEWA JIJINI DAR ES SALAAM
MEI 15, 2020

  • UCHUNGUZI MATUMIZI YA FEDHA ZA VYAMA VYA USHIRIKA: MPAKA SASA TUMEOKOA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 11.3

Ndugu Waandishi wa Habari,

Nimewaita kwa mara nyingine tena ili kupitia kwenu, tuendelee kuujulisha umma juu ya hatua mbalimbali za utekelezaji wa majukumu tunayoyatekeleza kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Huu ni utaratibu ambao Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa - TAKUKURU tumejiwekea ili Watanzania waweze kufahamu hatua mbali mbali zinazochukuliwa na TAKUKURU katika kutekeleza jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa nchini.

Kwa kufanya hivi, umma wa Watanzania utahamasika kushirikiana na TAKUKURU na Serikali yao kwa ujumla katika jitihada za kuzuia na kupambana na rushwa nchini.

Ndugu Waandishi wa Habari,

Leo tunataka tuendelee kuupatia umma mrejesho wa utekelezaji wa jukumu tulilopewa na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga - Novemba 26, 2019 kutokana na tuhuma mbali mbali kuhusu vitendo vya ubadhirifu na rushwa katika matumizi ya fedha za Vyama vya Ushirika nchini Tanzania.

Ndugu Waandishi wa Habari,

Mtakumbuka kwamba tumekuwa tukitoa taarifa kuhusu uchunguzi dhidi ya tuhuma hii kwa awamu tofauti ambapo awamu ya kwanza tuliitolea taarifa Januari 22, 2020 tulipowaita hapa Upanga jijini Dar Es Salaam na awamu ya pili tuliitolea taarifa Machi 14, 2020 hapahapa PCCB House Jijini Dar Es Salaam. Hivyo leo tunatoa taarifa ya uchunguzi wetu ambao uko katika awamu ya tatu.

Ndugu Waandishi wa Habari,

Mtakumbuka kuwa mnamo Machi 14, 2020 tulipokamilisha awamu ya pili ya uchunguzi huu, tulitoa taarifa ifuatayo:-
  • Kwamba kiasi cha fedha kilichochunguzwa mpaka wakati ule kilikuwa ni Shilingi Bilioni 66,255,488,545.73;


  • Tulieleza kuwa tayari TAKUKURU ilishaokoa kiasi cha Shilingi Bilioni 8,898,661,15.88; na pia

  • Tuliufahamisha umma kwamba tulikuwa tukiendelea na uchunguzi wa Shilingi Bilioni 57,356,827,388.85;
Ndugu Waandishi wa Habari,

Katika awamu hii ya tatu, hadi kufikia leo Mei 15, 2020 tunapotoa taarifa hii ya awamu ya tatu ya uchunguzi huu:
  • TAKUKURU imeshachunguza kiasi cha fedha shilingi Bilioni 103,643,076,623.74.
  • Kiasi cha fedha zilizookolewa hadi kufikia sasa ni shilingi Bilioni 11,314,443,422.31
  • Uchunguzi bado unaendelea dhidi ya shilingi Bilioni 92,328,633,201.43
Kwa mara nyingine tena ninatumia fursa hii kumshukuru Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa utashi wake wa kupambana na rushwa hapa nchini.

Ndugu Waandishi wa Habari,

Ninapenda pia mfahamu kuwa hapo awali TAKUKURU tulijikita zaidi katika kuhakikisha kuwa fedha za Watanzania waliodhulumiwa haki zao zinarejeshwa.

Lakini pamoja na jukumu hilo la kurejesha fedha pia tumefanikiwa kuanzisha uchunguzi kwa kufungua majalada ya uchunguzi pamoja na kufungua kesi mahakamani kwa wale ambao hawakutoa ushirikiano katika kufanya marejesho.



Hii ni kutokana na taarifa mbalimbali zilizopatikana na kubainika wakati tunavyoendelea na zoezi la urejeshaji wa fedha za wakulima katika operesheni hii.



Ndugu Waandishi wa Habari,




Mchanganuo wa taarifa za fedha zilizochunguzwa na kurejeshwa katika ngazi ya mikoa mpaka sasa katika awamu hii ya tatu ni kama ifuatavyo:



JEDWALI:




PROGRESS REPORT KUHUSIANA NA CHUNGUZI ZA UBADHILIFU WA FEDHA ZA
VYAMA VYA USHIRIKA NA SACCOS
[Kwa kipindi cha kufikia 14/05/2020]
NO
MKOA
KIASI CHA FEDHA KINACHOCHUNGUZWA
KIASI CHA FEDHA KILICHOOKOLEWA
KIASI CHA FEDHA KINACHODAIWA
1
RUVUMA
Bil. 5,148,900,947.00​
1,078,027,619.62​
4,070,873,327.38​
2
KILIMANJARO
Bil. 5,819,506,766.00​
108,005,700.00​
5,711,501,066.00​
3
MANYARA
Bil. 1,639,879,842.86​
81,148,617.00​
1,558,731,225.86​
4
KINONDONI
Bil. 5,996,285,089.17​
33,728,000.00​
5,962,557,089.17​
5
KATAVI
Bil. 1,084,157,500.00​
73,172,500.00​
1,010,985,000.00​
6
PWANI
Bil. 1,150,634,608.53​
347,514,550.67​
803,120,057.86​
7
MBEYA
Bil. 7,054,518,950.21​
107,450,790.02​
6,947,068,160.19​
8
IRINGA
Bil. 7,341,088,688.00​
714,417,198.00​
6,626,671,490.00​
9
SINGIDA
Mil. 408,306,119.00​
43,194,500.00​
365,111,619.00​
10
SIMIYU
Bil. 1,635,108,749.00​
83,972,750.00​
1,551,135,999.00​
11
ILALA
Bil. 4,272,321,246.00​
50,610,000.00​
4,221,711,246.00​
12
ARUSHA
Bil. 1,686,463,443.25​
64,435,350.00​
1,622,028,093.25​
13
KIGOMA
Mil. 231,705,214.90​
36,150,400.00​
195,554,814.90​
14
LINDI
Bil. 2,622,900,263.00​
1,361,209,809.90​
1,261,690,453.10​
15
NJOMBE
Bil. 8,129,073,365.04​
4,049,294,856.53​
4,079,778,508.51​
16
TANGA
Mil. 332,993,600.00​
10,842,480.00​
322,151,120.00​
17
TABORA
Bil. 2,932,330,114.71​
250,400,772.87​
2,681,929,341.84​
18
SHINYANGA
Bil. 1,814,720,765.00​
88,224,457.00​
1,726,496,308.00​
19
MARA
Bil. 3,159,944,951.85​
366,451,794.00​
2,793,493,157.85​
20
TEMEKE
Bil. 5,808,400,541.00​
249,743,313.90​
5,558,657,227.10​
21
MWANZA
Bil. 16,514,067,645.00​
43,778,767.00​
16,470,288,878.00​
22
KAGERA
Bil. 7,519,326,201.66​
290,900,845.45​
7,228,425,356.21​
23
GEITA
Mil. 131,400,000.00​
5,020,000.00​
126,380,000.00​
24
SONGWE
Bil. 1,115,916,074.00​
470,830,713.52​
645,085,360.48​
25
RUKWA
Mil. 627,957,588.00​
39,265,876.00​
588,691,712.00​
26
MOROGORO
Bil. 1,278,910,711.46​
42,594,400.00​
1,236,316,311.46​
27
DODOMA
Bil. 3,827,388,730.06​
197,740,844.00​
3,629,647,886.06​
28
MTWARA
Bil. 4,358,868,909.04​
1,026,316,516.83​
3,332,552,392.21​
Bil. 103,643,076,623.74
Bil. 11,314,443,422.31
Bil. 92,328,633,201.43




Ndugu Waandishi wa Habari,




Kupitia operesheni hii tunapenda kufafanua hali ya uchunguzi na mashitaka ilivyo katika mikoa yetu kama ifuatavyo:



Kupitia operesheni hii:


Tumefungua majalada ya uchunguzi 79 katika mikoa mbalimbali nchini;



Zipo kesi 11 zinazoendelea katika mahakama zetu nchini;



Yapo majalada 09 ambayo yapo katika mchakato wa kukamilishwa ili tuweze kufikisha watuhumiwa mahakamani.



Ndugu Waandishi wa Habari,

Vilevile, kupitia operesheni hii yafuatayo yamejitokeza:



Yapo majalada yaliyokamilika na kufungwa baada ya fedha zinazodaiwa kurejeshwa zote au hoja zilizokuwa zikilalamikiwa zimejibiwa zote na pande zote kuridhika;



Yapo majalada yanayoendelea na uchunguzi kwakuwa – japokuwa fedha zilizokuwa zikidaiwa zimeanza kurejeshwa lakini uchunguzi umebaini tuhuma za wizi na ubadhilifu.



Yapo majalada ambayo fedha zilizokuwa zinadaiwa zinaendelea kurejeshwa lakini pia kuna kesi zinazoendelea mahakamani.



Ndugu Waandishi wa Habari,




Kupitia hadhira hii ninataka nivitahadharishe Vyama Vikuu SITA ambayo nitaviita NI SUGU AU NI KOROFI - kwani licha ya vyama hivyo kufahamu kuwa vinadaiwa fedha za wakulima na pia vinafahamu kuwa vimepewa muda wa kurejesha fedha hizo lakini bado havijaanza kufanya marejesho yoyote ya fedha mpaka sasa.



Vyama hivyo ni vifuatavyo:

Chama cha KYEKU LTD cha Jijini Mbeya. Chama Hiki kinadaiwa zaidi ya Shilingi Milioni 476



Chama cha TANECU LTD cha Korosho kilichopo Mtwara. Hiki kinadaiwa zaidi ya shilingi Milioni 359



Chama cha NEEMA SACCOS LTD ya mkoani Njombe. Hiki kinadaiwa zaidi ya shilingi Milioni 234



Chama cha MAMCU cha Korosho kilichopo Mtwara. Chama hiki kinadaiwa zaidi ya shilingi Bilioni 2.5



Chama cha RUNALI kilichopo Nachingwea. Chama hiki kinadaiwa zaidi ya shilingi Milioni 856



Chama cha SCCULT cha Jijini Dar Es Salaam. Hiki kinadaiwa zaidi ya shilingi Bilioni 4.8



Ninaviagiza vyama hivi kuanza kurejesha fedha wanazodaiwa na wakulima haraka iwezekanavyo, na kwamba baada ya Mwezi huu wa Mei kuisha, hatua za kuwakamata wamiliki na viongozi wa vyama hivyo kwa mujibu wa sheria zitachukuliwa dhidi yao, bila ya kuwa na taarifa nyingine ya tahadhari kwao.

Ndugu Waandishi wa Habari,


Pamoja na majukumu hayo, kupitia Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007, tunalo jukumu la kufanya utafiti wenye lengo la kubaini na kuziba mianya ya rushwa kwenye sekta za umma na binafsi;

HIVYO BASI, kwa kutambua umuhimu wa Vyama vya Ushirika katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii; na ili kuhakikisha kuwa vyama hivyo vinaendeshwa kwa uwazi, uadilifu na kwa kufuata misingi ya sheria, kanuni na taratibu za nchi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iliona kuna haja ya kufanya UTAFITI.

UTAFITI huu umefanyika kwa lengo la kutathmini iwapo kuna mianya ya rushwa katika mfumo wa usimamizi na uendeshaji wa Vyama vya Ushirika na kisha kupendekeza namna bora ya kuimarisha mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa vyama hivyo nchini.

Utafiti huo upo kwenye hatua za uandishi na mara baada ya kuukamilisha, matokeo yake tutayatangaza kwa umma wa Watanzania.

Ndugu Waandishi wa Habari,

UGONJWA WA CORONA – COVID 19


Kupitia hadhira hii tunapenda kutamka kuwa TAKUKURU inaunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali katika kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huu wa CORONA na tunawahimiza wananchi waendelee kufuata na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Serikali kuhusu kinga dhidi ya ugonjwa huu.

Vilevile, tungependa mtambue kwamba TAKUKURU iko macho katika kufuatilia matumizi ya misaada mbalimbali inayotolewa na wadau katika kipindi hiki cha janga la CORONA ili kuhakikisha hakuna vitendo vya Rushwa vinavyojitokeza.

Ndugu Waandishi wa Habari,

Tunaendelea kuwashukuru wananchi na wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakishirikiana nasi katika kufanikisha jukumu hili la kuzuia na kupambana na rushwa nchini.

Tunawasihi waendelee kuiunga mkono TAKUKURU huku tukiizingatia Kauli Mbiu yetu ya mwaka huu isemayo; ‘KUPAMBANA NA RUSHWA NI JUKUMU LANGU’



IMETOLEWA NA:

J.J. MBUNGO, ndc

BRIGEDIA JENERALI

MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU
 

Attachments

  • FINAL PRESS STATEMENT AMCOS III MAY 2020.doc
    351.5 KB · Views: 1
TAKUKURU imulike na rushwa za vyeo na fedha taslimu ambazo zinatumika kuhonga wapinzani.
Laa sivyo TAKUKURU itadharaulika na kubezwa
 
Unaokoa huku halafu unapeleka kwenye ujenzi wa uwanja wa ndege ambao haujaidhinishwa na bunge , hiyo haitosaidia lolote
 
Nitapambana Na Rushwa Bila Kigugumizi Chochote Na Dawa Ya Jipu Ni Kulitumbua
Nipejipa Kazi Ya Mtumbua Jipu!!😀😁😂😅😄
Sitaogopa Kurukiwa Na Usaha. 🙄😎

Na Wale Watumishi Wavivu Wategaji Wajiandae


Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Bahati nzuri ni kuwa wasimamizi wa hivyo vyama ni wanachama kindakindaki wa chama dola, hivyo usitegemee kama kuna kesi zitaendelea
 
Back
Top Bottom