TAKUKURU yabaini rushwa ya ngono kutawala katika upangaji wa vituo vya kazi vya walimu

Kwa hii nchi ilipofika, inabidi kila mzazi mwenye mtoto wa kike ajitahidi juu ya uwezo wake kumjengea uwezo wa kimawazo na kifedha pia ili kumuepusha na hizi changamoto zilizopo hasahasa kwenye vitu kama rushwa ya ngono
Hata wanaume mbna, au kwa kuwa hawasemi?
 
Mimi kama mwanamke nasema rushwa ya ngono imeletwa na wanawake wenzetu ambao asilimia kubwa wanaona bora watumie miili yao kuliko kutumia akili au kuhangaika kutafuta kazi. Na wanajua wahitaji (wanaume) wapo kibao wanahitaji.

Lakini hata kwenye biashara hata demand iwe kubwa vipi, kama supply haipo basi itabidi wenye demand waangalie njia mbadala. Sasa wanawake asilimia kubwa sana wamejirahisi kiasi kwamba wasiotoa hiyo rushwa wanaumia na wanaume wanakazia palepale maana wana uhakika wa kupata ngono.

Laiti kama silimia kubwa ya wanawake wangeamua kukaza hizo sehemu zao na wakatumia akili kupata kazi haya yote yasingekuwepo. So waomba ngono wasilaumiwe sana. Wanafanya hivo kwakuwa system ya wanawake wengi kujirahisi imewazoesha.
 
Kuna wale madogo wanaitwa maafisa utumishi wanajigongea waalimu wenye misambwanda mpaka nawaonea wivu. Hakuna watu laini kama waalimu wa kike yaani akiwa na shida ni rahisi mno kutoa mzigo 😂
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma imebaini kughubikwa na vitendo vya rushwa ya ngono katika upangaji wa vituo vya kazi kwa waajiriwa wa idara ya elimu.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Sosthness Kibwengo akitoa taarifa kuhusu utendaji wa taasisi hiyo, amesema TAKUKURU imefanya uchambuzi katika mifumo sita ikiwemo mfumo wa elimu na kubaini uwepo wa mianya ya rushwa katika sekta hiyo.

“Tumebaini kuwa maeneo hatarishi ya uwepo wa rushwa ya ngono ni katika upangaji wa vituo vya kazi kwa asilimia 72,” amesema Kibwengo.

Aidha ameeleza kuwa eneo lingine hatarishi kwa uwepo wa rushwa ya ngono ni eneo la uhamisho wa walimu ndani ya halmashauri hiyo ambayo ni kwa asilimia 63.

Hata hivyo ameongeza kuwa taasisi hiyo imefuatilia utekelezaji wa miradi 41 ikiwemo sekta ya ujenzi, afya, maji na elimu yenye thamani ya shilingi bilioni 11.2 na kubaini miradi 10 ina upungufu ikiwemo vifaa viinavyotumika kutokidhi ubora.

Chanzo: Swahili Times
Baada ya kugundua uhalifu chombo cha dola kinachukua hatua gani!!! Kututangazia ktk media badala ya kuwanasa wahalifu!! Gross misuse of taxpayers hard earned monies.
 
Back
Top Bottom