TAKUKURU ya China | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TAKUKURU ya China

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kilemi, Jan 11, 2011.

 1. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Waajiriwa ni wachache sana na wanawajibika moja kwa moja bungeni. Kazi yao kubwa ni kufanya utafiti wa mambo yanayo sababisha rushwa, sio kuwakamata walarushwa! Walarushwa hukamatwa na Polisi wakishhirikiana mabenki au makampuni makubwa ya biashara! Benk hulinganisha kipato cha mtu, mali alizo nazo pamoja na hela alizotunza benk! kama kuna walakini basi taarifa hutolewa police au TAKUKURU kwenyewe!
  Kwa mfano kumwekea mtu hela bank hata kama ni mwanafunzi ni lazima uache particulars zako zote hapo bank, hii itamsaidia huyo mtu kuelezea zilikopatikana wakati zitakapoonekana ni nyingi kulinganisha na uwezo wake!
  Mwaka jana kamanda wa police wilaya mojawapo alikamatwa baada ya kununua gari! Yeye alikuwa mla rushwa, lakini kwa sababu benki hapafai basi akawa anazificha uvunguni! Aliponunua gari wakati ana mtoto anasoma english medium school (ambayo ni gharama kwa china), kampuni iliyomwuzia gari iliriport takukuru! Takukuru wakariport police, police wakaambush nyumbani kwake na kukkuta mamilioni ya fedha ufunguni; alihukumiwa kunyongwa!

  Kwa mazingira ya namna hiyo rushwa china haina deal, zaidi ya kunyea pombe na vimada, huka kazi yoyote utakayoweza kufanyia hela ya rushwa!

  Source
  China establishes corruption prevention bureau
   
 2. D

  Derimto JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huku kwetu ukifanya hivyo utaonekana sio uhuru wala Demokrasia na unakiuka haki za binadamu maana utakuwa umezuia wakubwa kufanya mambo yao kwa uhuru
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mzuri sana hiyo, hapa kwetu mie naona mtu akishachunguzwa haina haja ya kupelekwa wala kuambiwa polisi ina kwenda squad kum-eliminate, once and for all. Mara mbili tatu, kwisha habari za rushwa.
   
 4. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Tanzania mtu ana miliki gorofa kariakoo na apartment za kupangisha kibao masaki na zote hizo kodi hazilipi na hakuna atakayemchunguza.
  Nchi unapeleka milion 100 bank hakuna wa kukuliza kampuni yako iko wapi wala kujua umezipataje then tuna lalamika kukua kwa bei ya bidhaa na shilingi kushuka thamani!!!
  Ishakula kwetu siku nyingi!!!
   
 5. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  tunahitaji viongozi wenye macho kwa kweli, hawa tunaowasifia kila siku kwa ktabasamu na kuvaa suti! kazi ipo
   
 6. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  China ni nchi ya tofauti duniani ila tukubali kuwa Rushwa bado ipo ingawa ni ya kiwango cha chini sana kiasi kwamba si kero. Ukitaka kupata kazi mpaka utoe rushwa kuanzia ya ngono kwa mabinti mpaka fedha au vitu vidogo vidogo kama chupa ya pombe, matunda kama ndizi n.k hivi china haviitwi rushwa ila ni mahusiano (关系) wakati kwetu ndo tunasema Rushwa mbaya sana. Rushwa Kwa Wachina wenyewe ndugu zetu wanaangalia inayovuruga uchumi wao..... sisi Takukuru ya Tanzania na Hosea wao inaangalia Rushwa za madaktari sh.5,000 wanaachana na rushwa kubwa kama za akina RA za bilioni 185.
   
 7. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hizi rushwa za bia, ndizi au ngono zipo nafikiri kila sehemu duniani! Lakini Tanzania ilikuwa na haja ya kuajiri police marambili? Yaani kuna kuna askari wa TAKUKURU na askari usalama wa raia? Na wote hao wanaachana na rushwa wanapambana na "guanxi"? za manesi na mahakimu wa mahakama za mwanzo?
   
Loading...