Rogate
JF-Expert Member
- Sep 29, 2010
- 215
- 45
Madhara ya rushwa ni makubwa zaidi pale yule anayeidai anapochelewesha huduma au kuifanya kwa kiwango cha chini ili tu kusababisha apewe rushwa. Taratibu sheria na kanuni ndio sumu ya kummaliza huyu mdudu aliyewaingia watz. Mfano halisi ni leo ambapo nilikwenda mahakama ya Ilala samora avenue ambayo kwa sasa ipo Lumumba. Imenigharimu masaa 3 kupata mhuri wa mahakama. Wakati huo huo mwengine aliyetaka mhuri kwa sababu kama zangu aliupata kwa dk 30. Mazingira ya rushwa! Sikutakiwa kulipia chochote wakati huyu mwingine alitakiwa kulipia elfu 1 ya file. Utaratibu!