DOKEZO TAKUKURU Wakamateni Sheikh, Alhad Mussa Salum, RITA, Mkurugenzi, Ardhi na Polisi kwa kuvunja Msikiti wa Mwenge kwa Mabavu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Salaam Wakuu,

Jamani tunaomba msaada, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum atatutoa roho.

Baada ya rais Samia kuingia Madarakani, wale watu wa pesa inaongea Wamerudi kwa kasi ya ajabu. Mtu mwenye pesa sasa anaweza kufanya chochote na usimfanye kitu.

Katika Mkoa wa Dar Es Salaam kuna Taajiri amewaweka mfukoni Watendaji wote wa Wilaya ya Kinondoni hawa Wakina Gondwe.

Kipindi cha nyumba, kuna Tajiri alitaka kununua Msikiti ili ajenge maduka, Bodi ya Wadhamini ya Msikiti Wakamkatalia. Ikabidi Tajiri huyo amtumie Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ambaye alitetengeneza Bodi mpya ya wadhamni wasio hata waumin wa Msikiti ili Waweze kumuuza Tajiri na Wakafanikiwa. Kumbuka Msikiti unamilikiwa na Taasisi ya Mwenge Mosque & Islamic Centre. Hakuna aliyeshirikishwa kwenye Uteuzi wa Bodi Mpya.

Waumini Walilalamika RITA, Ardhi na kwa Mkurugenzi wa Kinondoni bila mafanikio.
IMG_20220917_113731_761.jpg

Wakashangaa Hati ya jengo wanayo wao lakini wakashangaa Msikiti unavunjwa na kuanza kujengwa Maduka. Walipojaribu kuzuia, Wakaitwa Polisi wa Oysterbay wakawakamata wote walioonekana kulalamika na kuwekwa ndani bila dhamana. Walikaa sana Polisi kwa kosa la kifanya fujo Msikitini. Aliyekua Msimamizi Mkuu wa Msikiti akafa kifo cha gafla kwani aliteswa sana na Polisi wakitaka aoneshe hati ya kiwanja ilipo kwani aliwanyima.

Je, Tajiri aliwezaje kununua sehemu na kujenga bila ya kuwa na hati?

Je, Kwanini Bodi ya Wadhamni iliundwa haraka bila kufuata kanuni?

Kwanini Polisi Wawashikile watu na kuwanyima dhamana hadi uzio uwekwe?

RITA WALIFIKA KUKAGUA MALI ZETU LAKINI HADI LEO HAWATUPI MREJESHO
IMG_20220917_121730_688.jpg

Kwanini RITA pamoja na kuja sehemu ya tukio, mbona hawajasitisha ujenzi?

Je kwanini Mkurugenzi alisimamisha ujenzi, lakini baada ya mhusika mkuu kufariki akaruhusu ujenzi uendelee?

Hawa waumini wanatishiwa kubambikizwa kesi ya Ugaidi.

Hapa chini naweka Ushahidi
IMG_20220917_113321_795.jpg

Hii hapa ni OB ya Polisi waliokamatwa kisa wanazuia Msikiti wao Usibomolewe. Huruma za Polisi ACP Ramadhan Kingai ndo zilifanywa Waachiliwe baada ya kuhoji sababu ya kuwashikilia bila dhamana wala kupelekwa mahakamani. Ni baada ya kuelezwa kilicho nyuma ya pazia.
IMG_20220917_113731_761.jpg

Hii ni barua iliyowataka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA) na BARAZA Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) kufika mbele ya Mkuu wa Wilaya ili atatue mzozo huu lakini hawajatokea kila Walipoitwa.
IMG_20220917_115502_988.jpg

IMG_20220917_115511_080.jpg

Hii ni kibali cha kusimamisha Ujenzi, wiki mbili baada ya alokuwa anatetea Msikiti usibomolewe kufariki, Wakakihuisha
IMG_20220917_120304_169.jpg
IMG_20220917_120259_155.jpg
IMG_20220917_120308_653.jpg

Na hiii ni hati halali waliyopewaTaasisi ya Mwenge Mosque & Islamic Centre ambayo hadi sasa bado wanayo, ila mtu mwingine kaja kabomoa Msikiti na Kujenga Maduka chini ya Usimamizi wa Polisi. Hawana hata Umiliki.
IMG_20220917_120554_577.jpg
IMG_20220917_120601_629.jpg

Na huu ni Uthibitisho wa Serikali za Mtaa kutoelewa kunachoendelea mtaani kwake
IMG_20220917_120831_097.jpg
IMG_20220917_120805_212.jpg

Na haya ndo Maduka yanayojengwa sehemu ulipokuwa Msikiti Mwenge mbele ya Magorofa ya Jeshi barabara ya TRA

Tunaomba Serikali Sikivu ya Mama Samia iingilie Kati swala hili. Bado naamini Godwin Gondwe anao uwezo wa kutatua mgogoro huu japo haoneshi jitihada zozote kuhakikisha hili swala linaisha.

Mkuu wa Mkoa Makalla sababu ni rafiki yake na Sheikh Salum, kila siku anasema yupo busy.
 
Back
Top Bottom