Takukuru - safari hii.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takukuru - safari hii..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tausi Mzalendo, Oct 25, 2012.

 1. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2012
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Je mna visingizio gani tena safari hii?
  Chaguzi zote zilizomalizika na zijazo siyo siri kuwa RUSHWA IMETAWALA NA ITAENDELEA KUTAWALA.
  Mnatuambia nini sisi wananchi?
  Rais mwenyewe alikemea uchaguzi wa UWT ulivyojaa rushwa.Hamkumwelewa?Mnahitai kuvalishwa miwani muweze kutanabahi na kuiona rushwa inayotolewa nje nje?
   
 2. K

  Kishalu JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 852
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  sio rahisi kumkosoa baba yako si atakufukuza, Rushwa kwa ccm sio rushwa si unakumbuka Hosea alivyosema hamna mchezo mchavu kwenye Richmond sasa rushwa iliyo wazi ni ya chaguzi za sasa za ccm alafu aseme chochote si atakua amekiuka maadili ya bosi wake
   
 3. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2012
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kumkosoa baba hakupo hapa.
  NNachotaka kujua ni je, TAKUKURU kama taasis, hawajaona Rushwa kwenye hiyo michakato?
  Au definition ya Rushwa kufuatana na PCCB Act ni nini?
  Je TAKUKURU wanataka kutuambia kuwa rushwa ni pale tu inapotokea "mtu/kikundi fulani cha watu" kukosana na Kundi fulani la jamii, kisha kundi hili kuwasakizia kama unavyosakizia mtu kwa mbwa " bobby..kamata!" ndipo wanapotoka spidi kukamata na kutishia ilhali hawamuumi mhusika?
  Mbona watz wameshachoka na hii "sakizia mbwa" asiye uma!
   
 4. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,643
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  TAKUKURU ivunjwe tu. Hakuna maana ya kuwa na TAKUKURU wakati hawajui job description zao, labda rais bado anazipitia.

  Shame on you Hosea, ondokeni tu humo!
   
Loading...