TAKUKURU: Pinda jiuzulu na Hosea akufuatie!

It not right at all kumkamata Dr Mwakyembe;kisheria TAKUKURU walifanya kosa kubwa la kiufundi la kuwapigia simu wanaotaka kuhojiwa badala ya kuwatumia barua rasmi zenye kuhahakiwa kama wamezipata ili ziingizwe kwenye rekodi za ofisi yao!

!


Huyo mwakyembe mwenye alimwandikia Barua Lowassa ya kumhita kumhoji?



Zito tupo ukurasa pamoja na nawasihi tusitete wizi !

Nashawishika kusema Mwakyembe kamuomba tena Mwanakijiji amtete..na kwa kuwa mwanakijiji alishafanya utetezi kwa kina Nisa swai na sakata lake ,alifanya hivyo Mama Sopha Simba basi aandike utetezi wake mwingine kwa mwakyembe kuwa anaonewa na niko tayari kumjibu kwa hoja kali zaidi.

Go on Cuzn na Pinda ataendelea kuwa Waziri Mkuu na nina Imani kubwa sana na Dr. Hoseah!

Sijaona sehemu ya kumsurubisha hoseah kwa kuwa hata suala la RDC mnajua tatizo lipo wapi

Ahaaa....unajua kwa sababu ni mmoja wao. Kama si mmoja wao sema umejuaje.


Julius unapenda sana sifa..



Julius tatizo lako haumpendi zito na maswali yako ni dharau na kumuabisha Mhe Mbunge..

kama aliwatikisa kwanini bado mnamchukia?muacheni na vijana mpendane..
 

Zitto,ngoja nikukumbushe hapa Takukuru inaongozwa na mtu anayetakiwa kujiuzuru kutokana na mapendekezo ya kamati ya akina Mwakyembe.
Kwanini asiachie ngazi ili kukipa hicho chombo heshima yake?Head of State halioni hili ilia analiona hili la posho mbili za wabunge?
Zitto kuwa mwangalifu pia acha kutu miss lead watanzania,tulitegemea mabaliko chanya toka kwenu hasa ninyi vijana.Nchi hii ikienda siko vijana watawalilia ninyi na ndipo mtakapo kuja jutia kwa nini ulikuwa viongozi zama hizi.
 
mimi nadhani suala la takukuru kuhoji wabunge ni makosa yaliyofanywa na mfumo mzima. mfano mdogo, utamuulizaje william lukuvi kama mkuu wa mkoa kwanini anapokea posho, while ni mbunge?
hapo utakuwa una 'mquestion' rais aliyemchagua kwani hakujua kama ni mbunge?
vivyo hivyo, ni wabunge wengi wenye nyadhifa mbalimbali na wanapokea hizo 'sitting allowances'.
 


Mbona mkuu aliepita hakuhojiwa??? kama kuna baadhi ya watu hawahojiwi kwa nini wengine wahojiwe? na kwa nini iwe sasa ambapo tunasubiria majibu ya msingi kutokana na matukio makubwa ya uhalifu? sometimes i fail to understand u!
 
=jethro;639454
Kaeni mkijua serikali inajua vyema jinsi ya kutuyumbisha muda wote huo
Naamini wale wote wanaojitambulisha kama ni wapiganaji wa ufisadi wangekuwa wasafi ama hata kutubu yale machafu yao yaliyopita na kuacha wanayoyaendeleza sana, msingeweza kuyumbishwa. kukosa MORAL AUTHORITY (mamlaka ya kimaadili) ndiko kunakowayumbisha na sio serikali ambayo nayo pia ina haki ya kutumia mapungufu yetu kulinda maslahi yake pale yanapotishiwa.

tokea 1979 iyo posho 2 ipo al over the suddny wamekuja na iyo issue yao wanadhani sie ni mambumbumbu nini??
Jee hilo linafanya hiyo tabia ama huo utamaduni wa kupokea na wakati mwengine kulazimisha kupewa malaki na mamilioni ya posho za ziada ya zile mlizo na haki nazo kuwa Sawa, halali na sio kukiuka maadili ya uongozi ama utanzania?

Ni mangapi ambayo tumekuwa tukiyafanya tangia enzi za ujima na sasa tunakubaliana kuwa hayakuwa sawa, haramu na yanakiuka kisingi ya utaifa, uongozi ama ubinadamu?

wanajipotezea muda na kujiwekea maisha ya watoto wao pabaya ni meisha waonya na kuwaambia Rwanda na Burundi ilianza chokochoko kama hizi na viongozi wakapuuzi kilichotokea buuuuuummmmm Vita ndiko huko viongozi wetu wanatupeleka.
Yaani wakati mnashangilia na kutetea uozo wenu hamuaoni kuwa mnayaweka maisha ya watoto wao ama wenu pia hatarini...mnapoumbuliwa katika maslahi yenu basi imeshakuwa chokochoko. Na pia acha kujidanganya, kukiripuka ni wewe na watoto kama unao ama ndugu na jamaa zako pia yatawakuta yaliyowakuta wa Rwanda na Burundi.

Na mojawapo ya sababu ya kuwa hapo ni huu ushabiki hovyohovyo na ubutu wa kufikiria kwa kina nini haswa chanzo cha matatizo yetu. Kukosa maadili kwa baadhi ya wabunge wetu kama viongozi wengine ni moja ya sababu hizo na ubinafsi wa kulinda maslahi binafsi kama ambavyo wabunge wanaopinga TAKUKURU kuendelea na uchunguzi wa kashfa hii ya posho ni sababu pia....
 
Huyu Masiha feki unayemzungumzia hapa ni nani?

Wale wote wanaojidai kuwa wao nido MASIHA wa matatizo yetu na wako mstari wa mbele kuwakomboa watanzania wakati wao wenyewe wamejaa uchafu, uozo, nia mbaya, chuki, ubaguzi, siasa hovyohovyo, ukosefu wa maadili na zaidi tamaa ya wao kufanikisha THEIR TURN TO EAT....

Chagua mwenyewe, mimi ninao wangu wengi tu...na nimekuwa nikiwataja kwa uwazi kabisa...
 

Hili la kusema kuwa hakuna sheria iliyovunjwa ndilo hilohilo linalotumika kuwaacha watuhumiwa lukuki wa UFISADI kuendelea na madaraka na majukumu yao. Watuhumiwa ambao hata badhi yao walivyolazimika kuwajibika kisiasa bado tunashurutisha tena kwa mwamko mkubwa sana kuwa waendelee kuwajibishwa kichama na kisheria hata kama tunajua kuwa kuna uwezekano mkubwa sheria hizohizo zinawapa upenyo mkubwa wa kutokea...

Uongozi ni zaidi ya kufuata sheria tu hata kama zina mapungufu. Uongozi ni suala la maadili. Maadili kaka taifa, chama, serikali, jamii na hata ule upeo wa kibinadamu tu....

Je, kitendo cha kupokea na wakati mwengine kwa moja ka moja ama kwa kificho kulazimisha kupewa posho zaidi ya ile halali wanayopewa na bunge sio ukosefu wa maadili wao kama viongozi?

Je, unadhani ni haki watanzania kuendelea kuaminishwa kuwa ukosefu wa maadili wa aina hiyo ni sawa mradi kwa kuwa hakuna sheria inayokataza.

Je unadhani kuwa hiyo vita ya UFISADI itafanikiwa huku ikiongozwa na watu waliokosa Utimilifu na Mamlaka ya Kimaadili (MORAL AUTHORITY) kama hawa "WAPIGANAJI" wetu/wenu?

Tujisahihishe jamani kabla hatujazama katika janga linalotujongea.....

Kujisafisha wenyewe kwanza na ndiko kutatuwezesha kusafisha mfumo kama ambavyo tunapenda kujiaminisha ndio nia zetu...
 

Nina mtazamo tofauti kidogo juu ya hili. Wabunge au mtu yeyote kuhojiwa sio jambo la ajabu sana, hasa linapofanywa na chombo chenye dhamana si ya kupambana tu, bali pia KUZUIA rushwa. Na kuhoji wakati mwingine ni kujifunza, wala si kutuhumu au kuhukumu. wabunge kwenye hili wanaweza kuhojiwa ili taasisi husika ipate mwanga wa nini hasa kinachotokea. Lakini suala la posho au malipo ya ziada kufanywa kwa mtu mmoja na vyombo au taasisi mbili tofauti linahitaji zaidi ya kuhoji wabunge. Nature ya kazi ya ubunge hailifanyi bunge kuzalisha pesa lenyewe, bali hutegemea pesa zinazotoka serikali kuu. Serikali kuu ndio yenye mawizara na mashirika/taasisi zinazodai kudaiwa na kulipa posho za ziada kwa wabunge, na inasemekana TAKUKURU ikiwa na mojawapo ya taasisi hizi. Katika hali kama hii, ni kutazamwa tu kwa mfumo mzima wa malipo kwa serikali na mashirika yake kutakapopelekea ubadhirifu wa namna hii kutofanyika

Lakini mh Zitto unalifahamu hili vizuri zaidi kuliko mimi kuwa malipo ya hizi posho kwa wabunge hayafanywi kimakosa, bali ni malipo ya makusudi kabisa yenye lengo maalumu. Malipo haya pamoja na mambo mengine hulenga kuwalainisha wabunge ili taarifa na miswada ya wizara na mashirika ya umma ipite kirahisi kwenye kamati za bunge. Wizara zinafanya sana malipo ya ziada kwa wabunge wakati wa kujadili miswada ya sheria mbalimbali katika kamati za bunge. Mashirika ya umma nayo hivyohivyo pindi yanapowasilisha taarifa zake za utendaji.

Katika hali kama hii, kuhoji wabunge huku muelekeo ukielekezwa kwenye kuifanya jamii idhani kuwa wao ndio wanaoopokea posho zaidi ni kupotosha na kutufanya wajinga

Kibaya zaidi katika haya ni kuwa, yote yanafanywa ili kupata ushawishi wa kisiasa

Takukuru ikitaka tuamini kuwa inafanya kazi yake kama taasisi huru na yenye lengo na uwezo kweli wa kuzuia na kupambana na ufisadi nchini, basi ifanyie kazi chanzo cha wabunge kupewa posho zaidi ya wanazostahili. Na ikifanya ivo kwa dhati, itagundua sio tu kuwa wabunge wanaziomba posho hizo, bali pia watoaji wanazitumia kama malipo ya kupata "mihuri" ya kamati za bunge na wabunge kwa ujumla

"katika nchi hii, nimejifunza kuwa, kwa kila unachoambiwa, anza kifikiri upya kuanzia hapo, na utagundua tunaishi katika uongo wa kutupa"

Nawasilisha
 

Mimi ninaanza na

1. Jakaya Kikwete
2. Zitto Zubeir Kabwe

Na wewe endeleza list
 
Mkuu Mwenzangu Mwanakijiji,

Hizo ni nadharia tu na hii inaonesha ni mapenzi gani uliyonayo na yakiyo kubuhu kwa Mwakyembe.Naomba kukwambia kuwa Unapenda sana ushabiki na hili nilishakuonya muda mrefu na hautaki kuliacha.


Huna uwezo au haki ya kunionya chochote au kwa lolote. Maonyo yako bakia nayo mwenyewe ndugu yangu. Mapenzi yangu hayako kwa mtu yeyote yule isipokuwa kanuni. Na cha kushangaza, watu wanasoma nisichoandika. Hakuna mahali ambapo nimemtaja mtu yeyote isipokuwa watu wanafikiria vile ambavyo wangefikiria.


Sauala la mwakyembe kuhojiwa halina uhusiano wowote na kwamba itafikia stage watu watanyamazishwa.Mwakyembe kachukua posho mara mbili which ni wizi kama anavyosema zito na mimi namuunga mkono zito

nyinyi zungumzeni watu. Kama kuna mbunge kaiba atiwe pingu afikishwe mahakamani na ushahidi wa wizi wake uletwe. Hilo halijalishi kama mwizi ni Mwakyembe, Zitto, Selelii, Lowassa, au Rostam. Lakini hauwezi kuwaletea mashtaka kiholela wakiwa kwenye kikao cha bunge. SHeria inakataza mashtaka ya kihalifu au ya madai kuletwa dhidi ya wabunge wakiwa kwenye kikao na mahakama yoyote ya Tanzania! Hamtaki hilo badilisheni sheria!


Cha msingi ,Mwakyembe ahojiwe na kama vipi afunguliwe mashtaka ya Rushwa.Hatuwezi kuwa na watu ambao hawashikiki eti kisa ni kamamnda wa ufisadi.

well.. I agree.

ukamanda gani huo wakati hata ubunge alioupata aliupata kwa kutoa Rushwa.au ukamanda ni kwa ajili ya watu wachache ambao yey hawapendi?

nawaachieni huo mjadala wenu wa watu. I have refused to get into hata mnivute kwa kamba!


Mpaka sasa naunga Mkono Dr. Edward Hoseah na PCCB kuwa jamaa ahojiwe na afikishwe mahakamani kwa kukika sheria ya Rushwa ya mwaka 2007.

Of course! Hana ubavu wa kuwashtaki; believe me. Hakuna kesi yoyote itakayofunguliwa he is on shaky legal ground than a cookie in milk jar!

kuhusu Kinga ya Mbunge,Kinga ipo katika hoja za bunge tu na siyo kwenye tabia ya kula posho mara mbili.

Si kweli. Kasome Haki, Madaraka na Kinga ya Bunge Ibara ya 5 na 11. Usibishe tu ili ubishe.
 
Mheshimiwa Rais amechelewa kumwajibisha Hosea li achunguzwe; that is the cause of all this mess we are experiencing. Kuna kitu hapoooo
 
Mzee mwanakijiji,
Mkuu wangu kuna mbinu kubwa za kuwaangusha Wapiganaji na baadhi ya watu (individuals) toka Chadema.. Hivyo huwezi shinda ubishi huu kwani tayari watu wameisha wekwa makhsusi kuwabwaga watu hawa kabla ya uchaguzi....Na hali inaonyesha wazi kwamba wanafanikiwa!
 

Yes ... Ni bange na sio bangi.
 

- Waliovunja sheria wako rumande na jela mkuu, wezi katika Tanzania huwa hawapigiwi simu kuulizwa kama wameiba huwa wanakamatwa na kwenda kujieleza wakiwa kituo cha polisi au Rumande, huhitaji kuwa Professor kuelewa hilo! ni mambo ya common-sense tu!

- Maneno mengi mazuri na ya kishujaa, lakini hakuna probable course!

Respect.


FMEs!
 
KUmbe hapa kuna tatizo kubwa sana la kikatiba. Kama rais ni mkuu wa mhimili mmoja na wakati huo huo ni mlinzi wa mihimili ile miwili mingine, inapotokea akaegemea ule mhimili ambao yeye ni mkuu wake(serikali), nani atamkemea na kumrekebisha?
Ina maana katiba imeassume kuwa rais ni malaika ambaye hawezi kutenda kosa?
Hiki ndicho kinachotokea sasa hivi. Rais (serikali) ameona bunge linahoji sana mambo yake, anatumia mwanya wa yeye kuwa juu ya mihimili mingine (bunge) ili kuzuia serikali isihojiwe. Ndio maana nchi nyingine rais si mtendaji, yeye anakuwapo kuiangalia mihimili yote mitatu na si pia kuwa kiongozi wa mhimili mmojawapo. Huu ni utaratibu uliopo hata uingereza ambapo kuna malkia na mtendaji ni waziri mkuu; Pia india kuna rais anayeangalia mihimili yote na waziri mkuu akiwa ni kiongozi wa mhimili wa serikali.
Kumbe sisi tumeiga ya uingereza nusu, na hatukuangalia namna checks and balances zitaendaje?
Mfano uliotoa Zitto wa kuunda kamisheni, hautasaidia kwani bado rais anaweza akatumia katiba kuzuia kamisheni isifanye kazi pale atakapoona maslahi ya serikali yanachokonolewa (kama ilivyo kwa tume ya maadili hivi sasa). Katika nchi zenye utaratibu huo., rais anaweza kushtakiwa - hayuko juu ya sheria.
Tubadili katiba ili rais asiwe juu ya mihimili mingine
 
Naomba niulize maswali.

6. Pinda na JK walishapokea kiasi gani wakati wakiwa wabunge?
Siyo walipokuwa wabunge, hata sasa hivi watueleze wanapoenda ziara ziwe za ndani au nje ya nchi serikali haiwalipi posho? Mbona huku tunachangishwa kuwapokea na tunawalaza na kuwalisha - je posho hizo wanazitumia lini?
Wakienda nje, ofisi za ubalozi zinahangaikia malazi na chakula na wakati mwingine aliyewaalika anawalipia kila kitu lakini posho hawarudishi!
Kuna posho nyingine tunayoshuhudia wabunge wakiila bure kila siku ya bunge. Mbunge analipwa posho ya kikao cha bunge halafu hayumo bungeni! Huu si wizi wa dhahiri? Nani alihesabu wabunge waliokuwemo bungeni wakati wa kujadili muswada wa haki za watoto? Hawakufika hata robo - lakini posho ya siku nzima wote wamechukua.
Afadhali anayechukua posho mara mbili akafanya kazi kuliko anayechukua posho moja na asifanye kazi (ingawa wote wana makosa)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…