Takukuru ni kinga ya watoaji na wapokeaji rushwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takukuru ni kinga ya watoaji na wapokeaji rushwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tankthinker, May 10, 2011.

 1. Tankthinker

  Tankthinker Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TAKUKURU NI KINGA YA WATOAJI NA WAPOKEAJI RUSHWA?

  Ndugu wana JF, mimi hawa TAKUKURU kwa kweri wana niudhi sana. Wanataka wananchi watoe ushirikiano kwa kuwapatia taarifa za rushwa. Cha kushangaza ni kwamba taarifa walizo nazo za rushwa kubwa kubwa zote hakuna hata moja waliokwisha kuifanyia kazi na kuitolea taarifa yenye tija kwa taifa letu. Sasa wanaleta mambo ya siasa, eti kuwa wananchi wenye taarifa za rushwa wawapelekee. Hiki chombo kwa mtazamo wangu ni kuwa kiliundwa kwa makusudi haya yafuatayo:

  1. Kuyandanganya mataifa kuwa Tanzania iko mstari wa mbele katika vita zidi ya rushwa. Hii ni kwa kusudi nchi zinazotoa misaada ziendelee kutoa huku zikidhani kuwa nchi ina viongozi waadilifu na misaada hiyo inatumika vizuri.
  2. Kuwabana na kuwatisha tisha wote wenye kuonesha upinzani dhidi ya uongozi mbaya wa kifisadi. Kwa mfano; Hivi karibuni tuliletewa hapa jamvini issue ya Askofu ambaye anasemekana amekuwa akikemea ufisadi hadharani na hivyo akatumiwa TAKUKURU wamchunguze. Hapa kuana rushwa gani huyu Askofu kachukuwa au katoa kama sio tu hayo malengo yao. Wakati wa kula za maoni za chama tawala rushwa ilikuwa kama kawaida, hakuna aliyefuatiliwa ila yule aliyekuwa hatakiwi na chama hicho. Kama rushwa ingefanywa na chama chochote cha upinzani basi hayo makucha ya TAKUKURU ndiyo yaneonekana na hata hukumu inge kuwa imeshatolewa kitambo kwa muhusika.
  3. Kukilinda chama tawala na viongozi wake wakati wowote wanatakapo tuhumiwa au julikana kuwa wametoa au kupokea rushwa. Haya maoni yangu ni kutokana na jinsi taarifa za rushwa zenye uhakika ambacho hiki chombo kinafahamu na wala hakuna chochote kinachotekelezwa kwa lengo la kutokomeza rushwa au kuwa chukulia hatua wahusika, tunona jitihada za kimakusudi za kuufumba umma kuwa watuhumiwa wanatuhumiwa kwa taarifa zisizo za kweri. Ukweri huu unthibitishwa na wao wenyewe katika habari iliyo andikwa na gazeti la Mwananchi yenye kichwa cha habari; TAKUKURU:Mwananchi Unaweza kuzuia rushwa kwa kutoa taarifa. Monday, 09 May 2011 21:25
  Naomba hiki chombo tukikatea na wala tusikipe ushirikiano wowote. Maana hakina dhamili ya thati ya kushughulikia ruswa Tanzania. Ni chombo kwa ajili ya masilahi ya watu wachache tu.
   
Loading...