TAKUKURU Morogoro yaokoa mamilioni ya Fedha

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
2,000
aasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro imetoa taarifa juu ya utendaji kazi kwa majumuisho ya miezi mitatu ambapo wameweza kuokoa zaidi ya shilingi Millioni hamsini zilizokuwa mikononi mwa viongozi wa vyama vya ushirika SACCOS katika wilaya za Mvomero na Gairo.


Akitoa taarifa hiyo naibu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Morogoro Victor Swela amsema kuwa Taasisi hiyo imeweza kuokoa fedha ambazo zilikusanywa na viongozi wa vyama vya saccos na tayari viongozi hao wamefikishwa katika vyombo vya sheria.

Aidha TAKUKURU imetoa wito kwa halmashauri zote ndani ya mkoa wa Morogoro kutumia vyema misaada yote wanayopokea katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 ili zitumike katike katika njia sahihi na si kufanya ubadhirifu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom