Takukuru kweli wameshindwa kubaini origin ya kadi feki za CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takukuru kweli wameshindwa kubaini origin ya kadi feki za CCM?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Aug 8, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Wadau, hivi hawa Takukuru wameshindwa kazi? Wameshindwa kabisa kubaini chanzo (origin) ya kadi feki za CCM lukuki zilizotumika katika kura za maoni za chama hicho hivi karibuni?

  Inavyoonekana ni kwamba ama hawataki kufanya uchunguzi wa kina kuhusu chanzo cha kadi hizo -- kwa maana ya kubaini kiwanda/viwanda na wamiliki/mmiliki wake -- au wamekatazwa kufanya uchunguzi wa kina.

  Hii inashangaza na kuchekesha -- na hapo ndiyo tunaona kuwa harakati zote za Taasisi hiyo katika zoezi zima la kura za maoni za CCM hazikuwa lolote bali ni kiini macho tu, au changa tu la machoni -- na lengo kuu ni kujaribu kuweka/ku-enforce maadili ndani ya chama hicho, maadili ambayo yanaendelea kutoweka kila siku au tayari yametoweka kabisa.

  Huwezi kutangaza zimekamatwa kadi feki -- huku hufanyi jitihada zozote kujua nani mhusika mkuu wa kadi hizo. Ni rahisi kumuuliza yule aliyekamatwa nazo wapi kazipata, kama ni tawi la CCM, maafisa husika nao waulizwe -- vivyo hivyo hadi kufikia mtu wa mwisho. Ni rahisi tu, unless huyo mhusika (origin) ni mtu mkubwa katika CCM -- na katika nchi pia -- ambaye hatakiwi akaguswa kwani yeye ni Mungu-mtu.

  Na hili ndilo ninalosuspect -- ndiyo maana mtiririko mzima wa ku-trace hizo kadi feki hautakiwi kufanywa.

  Nadhani wadau mnaweza kubaini ni nani au akina nani katika nchi hii wenye sifa hizi za U-Mungu-mtu.

  Inanikumbusha suala la wizi wa EPA uliofanywa na kampuni ya Kagoda. Pamoja na kwamba mabilioni yale yalipitia matawi ya benki za CRDB na kulipwa kwa mwizi/wezi husika, lakini Takukuru haikutaka, au ilikatazwa kufuatilia mtiririko wa wapi fedha hizo ziliishia baada ya kutoka benki. Takukuru wamekuwa mabubu hapo.

  Rafiki yangu kutoka Wilaya ya Nzega kanieleza kuwa Takukuru hawakuonekana kabisa wakifanya kazi yao, bila shaka kwa maelekezo -- kwamba wasiuingilie mchakato wa jimbo hilo la uchaguzi. Anasema siku chache kabla ya kura za maoni katika jimbo hilo maafisa wa Takukuru kutoka mkoani Tabora waliamrishwa kurudia njiani wakati walikuwa wakisafiri kuelekea Nzega.

  Anasema katika jimbo hilo mamia ya kadi feki zilitumika bila pingamizi zozote, kwani kulikuwa hakuna mamlaka ya kuzifuatilia.

  Takukuru, kweli hamna kabisa na uchungu wa nchi hii, katika kusaidia kuleta haki na maadili ili kuepusha farakano katika nchi hii huko baadaye?
   
 2. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Heko kwa post, Takukuru haina mjadala ni moja ya taasisi zilizoundwa kwa ajili ya chama tawala. Iko pale kulinda maslahi ya ccm siyo ya watanzania/kuzuia rushwa.

  Ni moja ya Taasisi za kuanza nazo kuzivunja na kuunda nyingine kama mheshiwa atakayekuja anataka kuiweka Tanzania pazuri. Haiwezekani hata siku moja unasikia watu wanakula rushwa wewe unasema hakuna ushahidi. Aaaaaah, mimi inanikera kwa kweli. Ngoja ninyamaze bana.
   
 3. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  It seems wewe sio mfuatiliaji wa Habari, mtambo wa kutengeneza hizo kadi feki uligunduliwa upo Arusha, na ulikamatwa na TAKUKURU hao hao.
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu mimi nafuatilia habari hiyo nataka nijue kama kweli jamaa watafikishwa kwenye mkono wa sheria. Maana nasikia kadi hizo zimewasaidia baadhi ya watu kupata ushindi wa kishindo.
   
 5. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Teh Teh Am back,
  By the way ngoja niwaambieni wakuu,

  Kwenye kura za maoni hakukuwa na Card za CCM fake zote zilikuwa ni sawa ila kilichofanyika ni urasimu wa hali ya Juu sana na ndilo kosa la Chiligate na wenzake wakubwa huko ccm kutokuwa na mikakati madhubuti katika zoezi hili kwanini nasema haya:-
  1: wakati wanamalizia mkutano wao pale Kizota chiligate akatangaza kuwa Card za ccm zimeisha na zitaletwa mpya kwa ajili ya kuwa wanachama wenu, kwa akili ya kawaida ni kuwa CCM hawakuwa wamejipanga kabisa kuhusu suara la kura za maoni kwani mwanachama wa ccm aandikishwe week mmoja kabla ya kura za maoni kwanini isiwe 2 or 3 Month before kupigwa kura za maoni??

  2: Chakushangaza zaidi walitoa deadline ya Reja ziwe zimerudishwa mapema kutoka kwa makatibu kata lakini zilichelewa kwanini? ni kuwa baada ya chiligate kutangaza card zimeisha na mtaletewa na kweli zilikuja lakini ilikuwa ti too late week hiyo ya kurudisha Reja ndio ilikuwa nayo ya kuandikisha wanachama wapya na je kuna uhakika gani wanachama hawa wapya wa CCM alikuja kwa hializao wenyewe au walipewa Takrima wajiandikishe ili kufanyike ilo zoezi la kupiga kura na hapo ndipo mchezo mchafu ulipo take place, How CCM iwena wanachama wengi kiasi hicho kwa muda mchache? na je walijiandikisha kwa kutangaziwa au kufuatwa na kuambiwa chukua card ya CCM?

  3: tatizo lingine lilikuwa ni kuwa kila katibu wa tawi fulani alipochukua card zake za kutosha tiali alikuwa na majina ya watu wake aliowahaidi na wachache waliokuwa wanataka card mimi hapo ndipo nilishindwa elewa je wanachama wa CCM wapya walikuwa na wazo la kusema huu ndio wakati wa mavuno na wakawa wanazikubali card na kujiandikisha??au ni kujiandikisha kwa mapenzi yao?? na ndipo hapo hawa makatibu walipachika majina mengi kwenye Reja zao. ilinistahajabisha sana hili CCM wao hawakuliona kabisa? au waliamua kufanya makusudi kabisa ili mambo yao yatimilike? kwa Hapo takukuru hawakufua dafu kabisa na haukukua na fake ni kuwa wao wana ccm waliamua kuziita Fake kwani muda ulikuwa umewatupa mkono card hazikuwa na picha za mpiga kura,stamp(mhuri) wa Katibu tawi na zingine zilizo kubaliwa ni card haina stakabadhi ya malipo ya awali wakati wajiandikisha ni wanakuandikisha jina na kupigiwa mhuri wa katibu tawi na hata picha hakuna wewe unaambiwa utapiga kura sasa hapo mwataka kuniambia nini? CCM walikosea kabisa bila hata ya ubishi leo wana CCM wengine wamesema ati ni fake kivipi hili hamkuliona kwanini mlikubali kufanyika wakati muda ulikuwa ni mdogo?
  Takukuru wao watoe statistics zao kwenye rushwa zilipotolewa ila wasijesema kuhusu maswala ya card pale ndipo watu wataleta malalamiko mengi zaidi.

  Kwa haraka haraka tumuulize Makamba atupe takwimu wa wanachama wa CCM Jimbo la Nyamagana, au Ilemela,Arusha Mjini hivi kama anazo yeye hapo alipo Dar?? najua hatotoa takwimu sahihi hata kidogo.
  Mbaya zaidi hizi kura za maoni zilitumiwa na wanafunzi pia walipiga kura kwa baadhi ya wabunge wagombea hii nilikutana nayo kanda ya KATI vijana wadogo sana ati nao wanakadi za CCM hakuna picha wala stakabadhi ni mhuti wa katibu wa tawi.

  Hili Zoezi lilifanyika ila lilikuwa na mapungufu makubwa sana na ndipo mahali palipo kifunuwa chama na kujione madudu ndani yake na pamoja na kuwa na wanachama wasomi
   
 6. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  wajamani kuna moja hiyo ni basi tu sikuwa na Tape Recorder ningewapa live nilikutana na mmoja ya wagombea ubunge mkoa fulani huyo mgombea anapewa Data na mtu wa takukuru kuhusu watu walikutwa au kamatwa na takukuru na huyo dada akawa anamwambia kuwa na watapelekwa mahakamani J3 na kweli nikafuatilia walipelekwa na hakukuwa na ushahidi wa kutosha.

  sasa swala kwangu ni kwanini Takukuru vijana wao walikuwa wanatoa siri kwa wagombea?? Kumbe na wao waklikuwa wanapewa rushwa! haiwezekani wewe unafanya takukuru na unawachunguza wagombea hapo hapo watoa siri na kumpa mmoja ya wagombea hapo nao Takukuru wamekura rushwa pia huu mchakato wa kuwapeleka wagombea wenye kashfa za rushwa pia wafanyakazi wa Takukuru nao wachunguzwe kwa kiasi kikubwa nao walichangiia kufichua siri na kazi kutotendeka vyema katika kamata kamata ya watoa na wapokea rushwa.

  Nampa Tahadhari Mr Hosea(TAKUKURU BOSS) pia nae awachunguze vijana wake wa kazi kuanzia sasa kazi za mashushu ni uumpapo kazi nae umchungeze pia kama anaifanya kazi ipasavyo au!!!
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,772
  Trophy Points: 280
  wao wenyewe wezi ushaona wezi wakikamata wezi wenzao ???
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ivi mna taarifa kwa sasa baadhi wa maofisa wa PCCBB ni mamilionea kwa sasa bse kama umecheza rafu afsa akikohoa tuu lazima umpoze yaani kama trafic akikukuta leseni imexpire.
  Mpaka uchaguzi uishe BAADHI ya maafsa watakuwa mbali sana wangekuwa wanatoa temple ningeamia uko
   
 9. I

  Irizar JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 217
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tatizo liko kwa maboss wa Takukuru, hawa wadogo wakiwakamata wakosaji, kesi ikienda mbele wakubwa wanachukuwa hongo wanawaachia huru, kwa hiyo kunakuwa na uhasama kati ya mkosaji na yule wa chini kutoka Takukuru. Mwishoni sasa hawa wadogo nao hawataki wala hawakamati mtu nao wanachukuwa RUSHWA kwa kwenda mbele sababu wasipochukuwa wao watachukuwa maboss wao kwa hiyo they might as well take the rushwa and life goes on man!!.

  Yaani tuna kazi kweli kweli..
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Yote haya yanasikitisha sana!!! Eti CCM sasa ndiyo imekuwa hivi???? Na bado wanang'ang'ania kupewa nchi kuiendesha!!!!! Na boss wa chama hicho? Kakaa kimya, hajakomment chochote kuhusu uchafu huu uliokuwa unafanyika mbele ya pua yake!!!! Wajameni tumjaribuni Dr Slaa!
   
 11. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2015
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,552
  Likes Received: 1,605
  Trophy Points: 280
  kweli mkuu.
   
 12. Ryaro wa Ryaro

  Ryaro wa Ryaro JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2015
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 2,663
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Origin # source
   
Loading...