TAKUKURU Kagera yawafikisha Mahakamani watu 11 kwa uhujumu na utakatishaji wa fedha haramu wa zaidi ya shilingi 900,000,000/=

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA


[TD valign="top"]


TAKUKURU KAGERA YAWAFIKISHA MAHAKAMANI WATU 11 KWA UHUJUMU NA UTAKATISHAJI WA FEDHA HARAMU WA ZAIDI YA SHILINGI 900,000,000/=

TAARIFA KWA UMMA
AGOSTI 3, 2020
[/TD]


Ndugu wanahabari,


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera tumeendelea kutekeleza majukumu yetu kama yalivyoainishwa katika Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sheria namba 11 ya mwaka 2007. Katika utekelezaji wa majukumu yetu tumeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya Rushwa wakiwemo waandishi wa habari, viongozi wa serkali na wananchi kwa ujumla.

Ndugu wanahabari,

TAKUKURU Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na ofisi ya mashitaka ya Taifa Mkoa wa Kagera leo Agosti 3, 2020 inakusudia kuwafikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba watu kumi na moja kujibu mashitaka ya Rushwa, uhujumu uchumi na utakatishaji wa fedha haramu wa zaidi ya shilingi milioni mia tisa (Shs 900,000,000/=).

Ndugu wanahabari,

Watu wanaotarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya leo ni pamoja na;-

Prospery Kashangaki Murungi ambaye ni mkazi wa Karagwe na amewahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya ya Chama Kikuu cha Ushirika cha wilaya ya Karagwe -KDCU LTD

Anna Michael Mlay ambaye ni mkazi wa Kyera- Mbeya aliyekuwa Meneja Utumishi na Utawala KDCU LTD

Sylvery Njagi –Mkazi wa Kaisho-Kyerwa ambaye amewahi kuwa Mkaguzi Mkuu wa ndani KDCU LTD

Justin Tinkaligaile Fidelis – Mkazi wa kata ya Nyakahanga Karagwe

Cyril Tambala Protase-Mkazi wa Rwabere –Kyerwa

Adriani Rwechungura Kabushoke –mkazi wa Rugu Karagwe

Sylvester Joseph Mugishagwe Mkazi wa Dar es Salaam na mfanyakazi wa Kampuni ya DAN CONSTRUCTION (T) LTD

Nestory Tiibaza huyu ni Mhandisi Mhandisi TARURA Nzenga - aliwahi kuwa Mtumishi katika ofisi ya RAS Kagera

Emanuel Ndyamukama huyu ni Mhandisi TARURA DSM - aliwahi kuwa Mtumishi katika ofisi ya RAS Kagera

Desderius Rutakyamirwa Mkazi wa Dar es Salaam na mfanyakazi wa Kampuni ya DAN CONSTRUCTION (T) LTD

Josephati Kinyina –mkazi wa Nyabiyonza Karagwe

Ndugu wanahabari,

Watuhumiwa tajwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma mbalimabali kumi na tano (15) zinazowakabili zikiwemo tuhuma za makosa ya rushwa na makosa mengine ya jinai hususani makosa ya ;-

  • matumizi mabaya ya madardaka kinyume na kifungu cha 31 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na 11/2007,
  • kutoa nyaraka za uongokinyume na kifungu cha 22 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na 11/2007,
  • kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu kinyume na kifungu cha 301 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002,
  • utakatishaji wa fedha haramu kinyume na kifungu cha 3(d), 12(d) na 13(1), vya sheria ya utakatishaji fedha sura namba 12 ya mwaka 2006 kikisomwa pamoja na aya ya 22 ya jedwali la kwanza na kifungu cha 57(10 na 60(2) vya sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002
  • kusababisha hasara kinyume na aya ya 10(1) ya jedwali la kwanza ikisomwa pamoja na kifungu cha 57(1) na kifungu cha 60(1) vya sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 toleo la 2002.

Ndugu wanahabari

TAKUKURU ilianzisha uchunguzi kufuatia kupokelewa kwa taarifa mnamo mwaka 2016 na uchunguzi uliofanyika umeweza kubaini kuwa mnamo mwaka 2008 uongozi uliokuwa wa Chama kikuu cha Ushirika cha Wilaya ya Karagwe (KDCU) uliingia mkataba wa Ukarabati wa HOTEL inayomilikiwa na Chama hicho ijulikanayo kama Coffee Trees mkataba wa mashaka na kutokana na kuingiwa kwa mkataba huo watuhumiwa kwa nyakati tofauti tofauti kuanzia mwaka 2008 hadi 2011 waliweza kutenda makosa tajwa na kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi milioni mia tisa kwa Chama kikuu cha Ushirika cha Wilaya ya Karagwe yaani KDCU

Ndugu wa Habari

Rushwa ni adui wa haki na inaweza kuathiri ubora wa Elimu utolewayo endapo watu wataachiwa kufanya au kuendesha shule au vyuo bila kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi zilizowekwa kwa maslahi mapana ya Taifa. Hivyo nitoe wito kwa Wananchi wote kuchukua hatua mahususi pale wanapoona kuna dalali au ukuikwaji wa sheria zetu za nchi au kuna viashiria vya uwepo wa vitendo vya rushwa. Aidha pia nitoe wito kwa wana Kagera wote katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwani kwa kufanya hivyo ni kufifisha jitihada na kuliletea maendeleo taifa letu na kwamba tusikubali kumchagua kiongozi yeyote anayetoa rushwa au kujuhusisha na vitendo vya aina yoyote vya ruishwa na makosa mengine.

Imetolewa na

Signed

JOHN K.E JOSEPH

MKUU WA TAKUKURU (M)
 
Vyama vya ushirika watu wamekula sana hela. Maisha yalikua matamu sana kwenye vyama vya ushirika.

Kazi ipo mwaka huu.
 
Hao TAKUKURU sina tena imani nao, naona siku hizi wanafanya kazi kwa kutafuta sifa tu, kumfurahisha bosi wao, hivi ule upelelezi dhidi ya Chadema wataendelea nao mpaka mwaka gani?!
 
yaani hapo ujue huku na huku wameshindana kwenye mtonyo kati ya takukuru na watuhumiwa...

ndio unasikia ukimwaga mboga namwaga ugali ...
 
Back
Top Bottom