TAKUKURU ina kazi gani kama Rais na Waziri Mkuu ndio wanaogundua rushwa?

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Habari hapa JF ,

Kutokana na ufisadi mkubwa na rushwa unaogunduliwa sasa hivi, na wanaogundua huu uozo ni Waziri mkuu na Rais, je hii taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (takukuru) ilikua inafanya nini, maana Rais na waziri mkuu ndio anafanya kazi zao.

Mimi naona ingefumuliwa na kuundwa nyingine mpya ambayo itakua huru na wachukue hii momentum ambayo rais na waziri mkuu ameileta,Mnasemaje?
 
Ningekuwa Mimi nisharesign Ila huwa anajitetea kuwa DPP ndo anamwangusha
 
hawajamaa wa takukuru wengi wakweli ila baadhi yao humohumo wala rushwa wakubwa wengi wameuawa na wengi kutishiwa uhai kwa usaliti huo sio wote wachafu ila wachache wamewaangusha
 
Ni zile zilizokuwa zipo kupotezea muda watu wale washibe wajaziane ulafi nao wale pia.
 
Habari hapa JF ,

Kutokana na ufisadi mkubwa na rushwa unaogunduliwa sasa hivi, na wanaogundua huu uozo ni Waziri mkuu na Rais, je hii taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (takukuru) ilikua inafanya nini, maana Rais na waziri mkuu ndio anafanya kazi zao.

Mimi naona ingefumuliwa na kuundwa nyingine mpya ambayo itakua huru na wachukue hii momentum ambayo rais na waziri mkuu ameileta,Mnasemaje?

uliona wapi mwizi kumkamata mwizi?
 
magufuli ni rais wa kila kitu, hana mipaka

rais hawezi kushughulikia kiola kitu, rais hatakiwi eti ndio anafuatilia wala rushwa wa tra, tanesko au bandari , rais anatakiwa awe ana unda sera nzuri nakuwapa watendaji wake na kisha yeye kufuatilia, sasa kuna taasisi ngapi atazifuatilia sasa maana rushwa ipo kila mahali na rais kazi yake sio kupambana na rushwa tu
 
Wengine walikuwa na mipaka ipi?

rais hawezi kushughulikia kila kitu, rais hatakiwi eti ndio anafuatilia wala rushwa wa tra, tanesko au bandari , rais anatakiwa awe ana unda sera nzuri NA MFUMO MZURI, na kuwapa watendaji wake na kisha yeye kufuatilia, sasa kuna taasisi ngapi atazifuatilia sasa maana rushwa ipo kila mahali na rais kazi yake sio kupambana na rushwa tu
 
Dr Magufuli futa kabisa hii taasisi ni wahalalishaji wa rushwa
 
Kwanza me sioni kazi yake bora ifumuliwe tuu imekaa kirushwa rushwa zaidi

Wanashindwa hata kutega mitego rahisi kabisa kwa traffic police ambao kila raia anawaona wakipokea rushwa hadharani huko kwingine si ndiyo kabisaaaa!!! Naafikiana nawe
 
Back
Top Bottom