TAKUKURU imeamka toka usingizi wa pono wa miaka zaidi ya kumi!

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
18,173
13,776
Ni ukweli usiopingika kuwa sasa TAKUKURU inafanya kazi yake.
Inaelekea ule usingizi wa pono iliyokuwa nao kwa zaidi ya miaka kumi umekwisha kabisa.
Tunaona sasa vigogo wanaitwa mbele ya Pilato kujieleza kwa makosa ambayo wananchi walikuwa wakilaamikia kwa miaka.

Magufuli lazima apewe sifa kwa kuliamsha dude hili, TAKUKURU, ili lifanye kile kinachotegemewa na wananchi.

Maswali ya kujiuliza ni mengi lakini la msingi ni kwa nini chini ya Hosea TAKUKURU waliamua kukalia tuhuma nzito nzito bila kuchukua hatua, walizuiwa au walipewa kitu kidogo ili watazame pembeni?

Ni maswali ambayo wananchi wangependa kujua.
 
Ndiyo maana Magufuli alimtumbua mapema Dr. Hosea. Aliwalea sana mafisadi . Tatizo pia lilikuwa kwa DPP. Alikuwa kama Hosea. Wote walikuwa ni akina ngosha lakini mzee wa hapa kazi hakuangalia hilo.
 
Ni maswali magumu ambayo hakuna kiongozi wa juu aliyeko tayari kuyajibu.Ni ukimya wa kimaslahi ambao hawako tayari kuukiri kwa kuwa ni aibu.Hata hivyo ni heri wakanyamaza maana wakiyajibu,mioyo itapasuka kwa maumivu.

Katika hilo kwa kweli Magufuli ameonekana kuwa yuko focused katika kile anachosema , na kuwa ni cha dhati na si longo longo
 
Mzee wa msog alikuwa ameziweka mafaili aliyopewa toka takukuru na tiss chini ya kiwanda!
 
Kwa kweli nakuombea sana mheshimiwa rais mungu amtangulie kwenye kazi zake,maana wabaya sasa kwake ni upande wa chama chake kwa mtazamo wangu.But washindwe na washindwe kwa uwezo mola.
 
Yaani takukuru ilipewa kilakitu lakini ilibanwa isifanye kazi kikamilifu maana prezidaa nae alikuwa namambo yake na watuwake. Kuibiwa kooote adhabu kubwa aliyotoa kwa wahusika ni kufagia hosp.
Tujifunze watu wa kuwapa kazi na wakuwaacha wacheze drafti na kunywa gahawa
 
Ubongo wako unapoteza kumbukumbu haraka sana. Adhabu ya kufagia Hospital imetolewa wakati Jk kishaacha Urais na kushughulika kuwapatanisha Walibya.
 
Hata hosea angepewa go ahead takukuru ingekuwa kama hii, tatizo wakuu wa nchi ndiyo walikuwa tatizo
 
Ubongo wako unapoteza kumbukumbu haraka sana. Adhabu ya kufagia Hospital imetolewa wakati Jk kishaacha Urais na kushughulika kuwapatanisha Walibya.
Ubongo wako mzito kuelewa,hiyokesi ilishapangwa itavyoisha kaabla kabisa.ilikuwa ni kujionesha tuu kwamba mapambano ni mazito kabla ya uchaguzi
 
Yaani takukuru ilipewa kilakitu lakini ilibanwa isifanye kazi kikamilifu maana prezidaa nae alikuwa namambo yake na watuwake. Kuibiwa kooote adhabu kubwa aliyotoa kwa wahusika ni kufagia hosp.
Tujifunze watu wa kuwapa kazi na wakuwaacha wacheze drafti na kunywa gahawa
Naona hata Pinda alibanwa sana kwenye kazi zake na JK. Ona sasa Majaliwa anavyofanya kazi ya U PM bila ya kuogopa!
 
Ni maswali magumu ambayo hakuna kiongozi wa juu aliyeko tayari kuyajibu.Ni ukimya wa kimaslahi ambao hawako tayari kuukiri kwa kuwa ni aibu.Hata hivyo ni heri wakanyamaza maana wakiyajibu,mioyo itapasuka kwa maumivu.
Tutamkumbuka Mwalimu, alisema ukila vya "wakubwa" kwa njia ya rushwa, utawezaje kumkata kwa kutolipa kodi!
Huyo " mkubwa" ameshakuweka mfukoni.
Ndo hayo sasa.
 
Back
Top Bottom