Daaa...kweli nimekumbuka Tarime sec,shule kama jeshi..mwenye nguvu ndo anakula wazembe mtabaki kuona struggle 4 food pembeeni...bwaloni mkono kila siku,wanafunzi 80% wababe na kauzu mbaya,nawakumbuka wapishi wakongwe kama Mzee chris huyu anakupiga uparo(chakula kidogo) ukiomba akuongezee unasikia" karibu kesho"! Mama mariana,mwita na wengine wengi.MSOSI huo ilikuwa ijumaa yaani toka asubuhi unawaza utapateje msosi,so inawabidi kutengeneza team ya mapambano ili atleast kutoka na kitu. Nakumbuka sufuria likibebwa juu na uji,ugali,makande,wali,maharage linashuka chini tupu! Alafu hapo wanafunz wameungua vibaya,ni mwendo wa kuwakimbiza hospital. Mitaa ya buhemba,FDC na mazoez ndo ilikuwa mitaa ya wanajeshi wa tarime sec kujidai,mtaani wakurya wanatuogopa vibaya ukivaa t-shirt ya Tarime sec basi wewe mfalme kila unapopita ni kidole unanyooshewa,NAKUMBUKA form one yetu tuliteswa sana,tulipigwa sana,tulinyanyaswa sana na matokeo yake wanafunzi tukawa tunalala juu ya miti usiku kukwepa kipigo bwenini! Kuna mwezetu alipoteza maisha kwa kipigo,kweli mwanafunz wa tarime sec ni full mwanajesh ni kukosa gwanda tu.