Taja madeni yako unayodaiwa

Dah mkuu uko TPDC nini mimi baada ya kukatwa miwili ya bank nabaki na 345000
Hio nikisema niisambaze kwa wenyewe ni siku mbili tu nabaki na HEWA...vipi wa loans board huna?
Nilipokopa huo mkopo mkubwa nnaokatwa 700k nkaenda kuclear na loan board ilikua kama nadaiwa 1.4m hv. Niliamua kuclear baada ya samia kutoa ile ofa mkopo ukapungua
 
Noncense wenye akili tushajua ni chai. Maana kwa mshahara unaoweza kukopesheka amount yote hiyo ni kama milioni 7 ama 8 sasa 3/4 inayotakiwa kubaki nayo haiwezi kuwa laki7 hata siku moja
Kwan kazini kwenu hakuna saccos??
Mkopo mkubwa nmekopa bank.. hiyo mingine ni saccoss ya kazini... ulizia tanesco saccoss inavofanya kazi.. au cocacola saccoss..
 
Hajui Kuna kitu inaitwa emotional support, yani Kuna muda umekaa mwenyewe unanung'unika huna viatu ghafla unaona mtu kilema anapita mbele yako Hana mguu mmoja au yote, basi unapiga got unamshukuru Mungu unasonga mbele.
Ni kwel chief
 
Chief sio kwamba nastahili pongezi?

faida moja wapo ya madeni ni pamoja na wanaokudai kukesha wanakuombea maisha marefu usife kabla ya kulipa madeni yao. Pil wanakuombea hustle zako milango ifunguke ili upate pesa za kuwalipa. 😂😂
Kaka kweli we mrusi wa mchongo, nili kupigia leo 😃🤣🤒
 
Kuna watu Hawa elewi pesa Ina Jenga uadui.
👉Mkopo ni mzuri mtu aki Elewa misingi yake, ila wengi tuna weka ujamaa na mazoea.
Halafu tatizo la mkopo, mtu hajui atalipaje ila anakuhakikishia kwa maneno tu huku akijua fika hawezi kutimiza ahadi
Yaani mtu unamdai na aliahidi mwisho wa mwezi lakini siku ikifika anapiga kimya mpaka umsemeshe
Na ikivuka mwezi tangu alipoahidi huyo kakutapeli

Mkopaji lazima arudishe siku aliyokuahidi ikipita tu bila ya yeye hata kukupa ile heshima tu ya msaada uliomfanyia na kukuomba radhi kuwa aliahidi ilaimeshindikana sawa

Hivi deni mtu unaweza kusahau kuwa unadaiwa
Halafu cha ajabu aliekopesha ndio anakosa usingizi, lakini aliekopwa anakoroma kabisa kama mali ya baba yake 😄
 
Mimi kuna kipindi ilibid niwe mkali kwa wanaonidai atleast wanipe muda maana niliona nikiwa mnyonge madeni yatanirestisha in peace kabla ya siku zangu,thanks God wengne nimemaliza,wengne wamenipuuza na kusamehe ila kuna hawa HESLB wala hata wasijisumbue maana siwalipi!tusiogope madeni wakuu,ila tuangalie na wapi tunaemkopa!
 
Back
Top Bottom