Kwa wale wenye magari ambao hawapendelei kununua used spair parts kama matairi yaliyotumika na kuchongwa, na kuamua kujikamua kununua tairi mpya toka dukani, kuna haja ya kuwa makini hasa katika kujua tairi hilo jipya lilitengezwa lini. Wenzetu wa magharibi wanaanza kufikiria kuwa "aging" yaani umri wa tairi unaweza kuwa sababu tosha ya kusababisha matairi kujimenya na kusababisha ajali na kupendekeza miaka isizidi sita ya tairi toka kutengenezwa mpaka kununua. Wasiwasi wangu ni kwamba kama sheria hizi zikipita huku kwao basi kuna uwezekano mkubwa na matairi yaliyokaa muda mrefu kutupiwa sisi ili yatumalize.
Je unawezaje kutambua umri wa Tairi toka lilipotengenezwa?
Jibu rahisi sana, kila tairi lina namba na trade mark zake ila kuna namba ambazo ninaamini wengi wetu hatuzijui ni za nini, namba hizo zinaweza kuwa tatu au nne zimezuungushiwa round kila moja. Hizi ndizo namba zinazoonesha tairi limetengenezwa lini japo ni jipya.
Mfano:-
1. namba
519: hii inaonesha tairi limetengenezwa wiki ya
51 mwaka
1999
2. namba
236: hii inaonesha tairi limetengenezwa wiki ya
23 ya mwaka
1996
3. Namba
4107: inaonesha tairi imetengezwa wiki ya
41 ya mwaka
2007
4. Namba
1708: inaonesha tairi imetengenezwa wiki ya
17 ya mwaka
2008.
Kwa hiyo tusisubiri mpaka TBS huenda hawajui haya kutuambia ila unaweza kujiridhisha mwenyewe kuwa unanunua kitu cha lini na kwa thamani bora ya pesa na usalama wa maisha yako.
unaweza kujifunza zaidi toka
HAPA