Tairi zilizokaa muda mrefu zaweza kuwa hatari kwa usalama barabarani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tairi zilizokaa muda mrefu zaweza kuwa hatari kwa usalama barabarani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hofstede, Feb 6, 2009.

 1. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kwa wale wenye magari ambao hawapendelei kununua used spair parts kama matairi yaliyotumika na kuchongwa, na kuamua kujikamua kununua tairi mpya toka dukani, kuna haja ya kuwa makini hasa katika kujua tairi hilo jipya lilitengezwa lini. Wenzetu wa magharibi wanaanza kufikiria kuwa "aging" yaani umri wa tairi unaweza kuwa sababu tosha ya kusababisha matairi kujimenya na kusababisha ajali na kupendekeza miaka isizidi sita ya tairi toka kutengenezwa mpaka kununua. Wasiwasi wangu ni kwamba kama sheria hizi zikipita huku kwao basi kuna uwezekano mkubwa na matairi yaliyokaa muda mrefu kutupiwa sisi ili yatumalize.

  Je unawezaje kutambua umri wa Tairi toka lilipotengenezwa?

  Jibu rahisi sana, kila tairi lina namba na trade mark zake ila kuna namba ambazo ninaamini wengi wetu hatuzijui ni za nini, namba hizo zinaweza kuwa tatu au nne zimezuungushiwa round kila moja. Hizi ndizo namba zinazoonesha tairi limetengenezwa lini japo ni jipya.

  Mfano:-

  1. namba 519: hii inaonesha tairi limetengenezwa wiki ya 51 mwaka 1999

  2. namba 236: hii inaonesha tairi limetengenezwa wiki ya 23 ya mwaka 1996

  3. Namba 4107: inaonesha tairi imetengezwa wiki ya 41 ya mwaka 2007

  4. Namba 1708: inaonesha tairi imetengenezwa wiki ya 17 ya mwaka 2008.

  Kwa hiyo tusisubiri mpaka TBS huenda hawajui haya kutuambia ila unaweza kujiridhisha mwenyewe kuwa unanunua kitu cha lini na kwa thamani bora ya pesa na usalama wa maisha yako.

  unaweza kujifunza zaidi toka HAPA
   
  Last edited: Feb 6, 2009
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu shukrani kwa hii habari, kweli kuna mambo inakuwa vigumu kuyajua. Na wauzaji pia kama wanajua hawawezi wakati fulani sema ukweli ili kulinda biashara zao. Sasa hizi namba ni kwa magari tu, ama pia zipo kwa pikipiki na baiskeli?.
   
 3. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Mkuu, asante sana kwa hii elimu kuhusu matairi maana mimi binafsi nilikuwa siwezi kuchambua kwa kina hivi wakati wa kuyanunua. Nilikuwa naishia kujua namba ya tairi tu!
   
 4. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,896
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Thanks a lot mkuu yaani hii habari imekuja wakati muafaka kwangu kwani am on the way to buy.
   
 5. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Sina uhakika kuhusu tairi za baiskeli na pikipiki ila hiyo code ni kwa mujibu wa tyre manufacturers, kama kwenye tairi za pikipiki na baiskeli zipo zitakuwa na maana moja japo sifahamu zaidi kuhusu pikipiki na baiskeli
   
Loading...