Taikon wa Fasihi awards 2020

Taikon wa Fasihi awards 2020

Kungwi awe Mchagga??? Yewooomii

Namba 5 ulipaswa umtaje Mh. Pascal Mayala

Namba 12 huyo Mkojani ni kelele nyiingi sometimes anakera
 
Kungwi awe Mchagga??? Yewooomii

Namba 5 ulipaswa umtaje Mh. Pascal Mayala

Namba 12 huyo Mkojani ni kelele nyiingi sometimes anakera

Hapa hatuangalii ukabila boss, tunaangalia kazi na impact yake ndani ya Jamii. Dada irene Mbowe amekuwa Kungwi boraa kwa Mwaka huu kwa sababu yeye mwenyewe ni mfano bora wa mwanake bora ndani ya familia yake. Anawafunza wasichana namna ya kuwa mke bora ni kuwa mchapkazi, kujitegemea, utiifu na mahaba. Sasa makungwi wapumbavu wakishaambiwa ukungwi wanachojua ni Kungonoka tuu, mara staili za ngono na upuuzi upuuzi tuu

Kuhusu kutomtaja Mkuu Pascal Mayalla.
Ni kwa sababu Athari ya Pascal Mayalla kwenye jamii ya wasomi ni ndogo sana. Pascal Mayalla athari yake ipo hapa hapa Jf, lakini Ole Mushi athari yake ni kubwa, sio ndani ya jf tuu hata nje, ingia kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Makundi ya WhatsApp, utaona makala nyingi za Ole Mushi kuliko Mayalla.
Sio kwamba Mayalla haandiki vizuri au haitetei vizuri CCM yake, lakini hapa tunaangalia kuandika vizuri na athari yake kwa watu.
Labda ningekuuliza, kwenye makundi ya WhatsApp au Facebook ni mara ngapi umekutana na Makala za Ole mushi, na mara ngapi Umekutana na makala za Kaka Pascal.

Ole mushi anaongelea mambo mchanganyiko, Mayalla kajikita zaidi kwenye siasa na uchumi.
Mayalla siku za hivi karibuni kajikita zaidi kusifia CCM na kuacha jukumu la Kukosoa jambo ambalo linamfanya apoteze athari kwa jamii kubwa, lakini Ole Mushi licha ya kuwa CCM lakini kuna wakati anaikosoa serikali na Chama chake, jambo ambalo linamfanya azidi kupaa kwenye bahari ya uandishi.

Kuhusu Mkojani, sijaona ni wapi umamuona sio bora, kama ni makelele nayo ni mbinu yake ya kuchekesha, kuna wanaochekesha kwa kufanya matendo bila ya sauti, kama kina Charlie Chaplin,Buster Keaton's, Mr Bean, n.k. Hawa walichekesha pasipo kuongea kitu. Lakini wapo wachekeshaji wa kutumia sauti tena kali, Hivyo ulipaswa uulize kwanza kama ule nao ni uchekeshaji au laa
 
Kuna watu wanatangazwa na ubora wa kazi zao. Siyo mtu anajitangaza kila siku yeye kuliko hata kutangaza kazi zake.

Ruge ( RIP) hakuwa hata na account instagram, ila alivyofanya Clouds watu walitaka tu kujua who is behind that.

Kenya tu hapo kuna James Mwangi, kaitia Equity zero kabisa mpaka sasa hivi imekuwa kubwa, kazi yake ndio imemtangaza.

Antony Mtaka ubora wa kazi yake ndio umemtangaza.

USA kuna kina Robert Smith, Zuckerberg, mostly wametangazwa na kazi zao.

Sasa huku kwetu huyo Jokate kwanza hana kazi ya maana zaidi ya mapicha picha mitandaoni. Ukiuuliza any accomplishment HAKUNA. Anazidiwa hata na yuke GERANA somebody dada fulani ni Kiziwi
Mkaruka hii id yako nyengine
 
Ni Tz tu hata wanasiasa au chama cha siasa kinashindanishwa katika tuzo.
 
Mkuu hizo tuzo zimekaa palipo, hapo hakuna upendeleo hapo
Kweli kabisa.Ontario atapewa tuzo bora za MTU ANAYE BLOCK WATU ZAID INSTAGRAM 2019 & 2020.....(jokings)


Mkuuu namba 8 hapo...naomba unisaidie nakipataje kitabu hcho, I mean hard copy.???


Screenshot_20201222-040059.jpg
 
Mkuu, ROBERT HERIEL ninakushukuru sana kwa kutambua mchango wangu humu JF. Ninakaribisha pia Constructive Criticisms zitakazonisaidia katika kunijenga zaidi.

Mkuu hongera sana, napitiaga sana kazi zako,
Unajua wengine wanaweza wasijali, lakini wachache tunajali yanayotujenga, kutufurahisha, kutuelimisha n.k

Kuhusu Constructive Criticisms usijali,, nitakuwa nachangia
 
TUZO ZA TAIKON WA FASIHI 2020

Mwaka umeisha, kama ilivyo ada ifikapo mwisho wa mwaka, tarehe kama za leo, nimekuwa na kawaida kutoa Tuzo kwa Watanzania ambao nimewaona wamefanya vizuri katika fani zao, au Nyanja mbalimbali. Tuzo hizi ni sehemu tuu ya kutambua, kuheshimu, kuzikubali, kutoa moyo kwa Watanzania wenzetu waendelee kufanya kazi nzuri zaidi. Nafahamu wapo Watanzania wengi wanaofanya kazi nzuri zaidi lakini hawa watawawakilisha.

Haya Mabibi na Mabwana, ule wakati wa Kutoa Tuzo umewadia, Nitawaomba pale nitakapo taja mshindi wa Tuzo mshangilie kwa furaha na bashasha.

A. TUZO ZA WANASIASA

1. Kiongozi Bora wa kisiasa wa kiume kwa Mwaka 2020


2. Kiongozi Bora wa Kisiasa wa Kike kwa Mwaka 2020


3. Kiongozi Bora wa vyama vya Upinzani kwa mwaka 2020


4. Kiongozi Bora wa chama tawala CCM kwa mwaka 2020


5. Mwana CCM Bora aliyeitangaza CCM Mtandaoni bila kulipwa chochote na chama chake kwa mwaka 2020


6. Mpinzani bora aliyetangaza CHADEMA Mtandaoni bila kulipwa chochote kwa Mwaka 2020


7. Mwanapropaganda bora kwa mwaka 2020


8. Chama cha Bora cha kisiasa kwa mwaka 2020


9. Mwanasiasa aliyeongoza kwa kusemwa iwe kwa zuri au kwa Baya kwa mwaka 2020



B. TUZO ZA SANAA, MICHEZO NA BURUDANI

1. Mwana muziki Bora kwa mwaka 2020


2. Mwana Muziki Bora wa Kike kwa mwaka 2020


3. Mchoraji Bora kwa mwaka 2020


4. Muigizaji bora wa kiume kwa mwaka 2020


5. Mwigizaji Bora wa Kike kwa mwaka 2020


6. Mchekeshaji Bora wa Stand up comedy kwa Mwaka 2020


7. Kwaya bora kwa mwaka 2020


8. Mwandishi bora wa Fasihi(Riwaya) kwa Mwaka 2020


9. Mchezaji Mpira bora kwa mwaka 2020


10. Mkalimani Bora wa filamu kwa mwaka 2020


11. Producer na Dj bora wa muziki kwa mwaka 2020


12. Mchekeshaji bora kwa mwaka 2020


13. Bondia Bora wa Masumbwi kwa mwaka 2020


C. TUZO ZA KIJAMII, UTAMADUNI NA MEDIA

1. Kungwi Bora kwa mwaka 2020


2. Mhamasishaji bora wa Mtandaoni kuchangia wahitaji kwa mwaka 2020


3. Mtandao Bora wa Kijamii katika Nchi yetu kwa mwaka 2020


4. Mchangiaji Bora wa mitandao ya Kijamii kwa mwaka 2020
> Infantry Soldier wa jamii Forum

5. Kampuni ya Mabasi inayotoa huduma Bora kwa mwaka 2020


6. Kiongozi wa Dini aliyetoa huduma bora kwa mwaka 2020


7. Msomaji bora wa simulizi kwa sauti kwa mwaka 2020


8. Shule bora kwa mwaka 2020


9. Mganga bora wa masuala ya Miti, uganga, ulozi na uchawi kwa mwaka 2020


D. TUZO ZA UCHUMI NA BIASHARA

1. Mfanyabiashara bora kwa mwaka 2020


2. Mtangazaji bora mbunifu kwa mwaka 2020


3. Kijana mwenye kuhamasisha zaidi vijana kujiletea maendeleo kwa vitendo 2020


4. Mhamasishaji bora (Motivational speaker) kwa nadharia 2020


5. Mkulima bora mdogo na mhamasishaji wa kilimo 2020


6. Dalali bora kwa mwaka 2020


7. Mkoa bora wenye fursa nyingi Tanzania kwa mwaka 2020


Niwapongeze wale wote waliopata bahati ya kupata Tuzo hizi. Ni katika jitihada za kutambua kazi za wale waliofanya vizuri.

Muandaaji wa Tuzo,
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji3577][emoji3577][emoji3577][emoji1679][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Back
Top Bottom