Taifa Stars Yawakong'oli Waganda! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa Stars Yawakong'oli Waganda!

Discussion in 'Sports' started by Kakalende, May 3, 2008.

 1. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2008
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  [​IMG][​IMG]

  Wadau wa soka week-end yenu itakuwa ya furaha/
   
 2. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  afadhali wametupoza kidogo sio tu machungu ya ufisadi, uchawi bali hata ukichwa wa mwenda...
   
 3. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  tu natoa pongezi zetu kwao, wamejitahidi, tunawatakia mafanikio zaidi
   
 4. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #4
  May 4, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Hongera starz.ila sasa akina makamba,jk,na nchimbi wasiibuke na kudandia tena wadai ni sera zao nzuri.

  Sana sana nilifurahi walipoichaopa Kenya na kuifukuzia mbali nje ya mashindano
   
 5. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  mwenye habari atujuilishe vipi timu yetu imefanikiwa kumuangusa crane?
   
 6. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Kwa mujibu wa bbc swahili, matokeo ni suluhu ya moja moja, hivyo Uganda tumewatoa kwa jumla ya magoli 3 - 1.
   
 7. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hongera kwa wachezaji wetu na Watanzania wote, tunaomba kocha aandae timu vizuri zaidi kwani mechi inayofuata tunakutana na Sudan. Tunakumbuka Sudan ilitutoa kwenye kombe la Kagame. Hivyo tunatakiwa kujisahihisha ili tuibuke na ushindi.
   
 8. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hongera JK boys
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,549
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Kutoka kwa Muhidini wa Michuzi

  BREKING NYUUUUUZZZZZZZZZ
  TAIFA STAAAZ IMEFANIKIWA KUVUKA KIGINNGI CHA KUSAKA TIKETI YA KUSHIRIKI FAINALI ZA KWANZA ZA MATAIFA YA AFRIKA KWA WACHEZAJI WANAOCHEZA LIGI ZA NYUMBANI MAARUFU KAMA CHAN BAADA YA KUILAZIMISHA SARE YA 1-1 TIMU YA UGANDA CRANES UWANJA WA NAKIVUBO HUKO UKWENI.
  GOLI LA STAA LIMEPATIKANA DAKIKA YA 44 MFUNGAJI AKIWA ATHUMANI IDDI 'CHUJI'
  HII NDO KUSEMA STAAZ INAPETA KWA MABAO 3-1 BAADA YA USHINDI WA 1-0 ILIYOPATA IKIWA NYUMBANI WIKI MBILI ZILIZOPITA. SASA TUNAMNGOJA MSHINDI KATI YA SUDAN NA RWANDA AMBAPO TUKIMSHINDA TUNAINGIA FAINALI YA KOMBE HILO ZITAZOFANYIKA IVORY COAST MAPEMA MWAKANI.
   
 10. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #10
  May 17, 2008
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hongera vijana kazi yenu tunaikubali.
   
 11. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2008
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hongereni Staaz!! Sasa tujipange kuwakong'ota waSudani..... Nina amini tukijipanga hawa waSudan tutawapiga bao miiingi tuu!!!!

  Mungu wabariki vijana wa Staaz, Mungu Ibariki Soka ya Tanzania, Mungu Ibariki Tanzania na watu wake!!!
   
 12. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2008
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,272
  Likes Received: 4,256
  Trophy Points: 280
  Congratulation TAIFA STARS
  But bado tuna mechi na SUDAN hawa CAF hawatupendi
  kazi tulioifanya itaonekana bure kama hatutawatoa SUDAN
   
 13. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  mi hao jamaa ningewaona wa maana kama wangewafunga msumbuji...
  kwa kosa lile siwezi kuwasamehe hasilani.
   
 14. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  usimsahau jk kwa kutuletea mwalimu
   
 15. Kidzogolae

  Kidzogolae Senior Member

  #15
  May 18, 2008
  Joined: Apr 20, 2008
  Messages: 134
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Acha kujishushia hadhi wewe, utasemaje hao ni vijana wa JK? inamaana sio vijana wa watz wote? acheni kumpa masifa yasiyo na maana huyo JK. Hao ni vijana wetu sisi wote watz, na msiwapachike jina la JK, msije mkatufanya tusiwashangilie ashangilie huyohuyo JK peke yake. period.

  otherwise, NAWAPA HONGERA SANA Taifa stars, watoto watz kwa kutupa furaha ya moyo baada ya kuwafuga the cranes. bora wametupoza moyo kidogo, sio tu kila wakati tunakuwa na machungu ya ufisadi mioyoni mwetu. by the way, waganda na wakenya wamekuwa wateja wetu mda wote. hata wakijitahidi kutapatapa tunawafungaga tu. chao.
   
 16. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #16
  May 19, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280

  Hivi watu kama ninyi bado mpo tu? Upunguani mwingine bwana,duh,ndo maana tunafikiria na kupanga mambo kiswahiliswahili
   
 17. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #17
  May 19, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  duh wenye kuumiA na waumie lkn ndio hivyo JK boys kwa maana yeye amesaidia sana kuisapport timu yetu ya taifa na sasa yeye ndio key ya taifa letu hata huku nje baadhi ya wakati tunataniana watoto wa JK na wa kenya tunawaita watoto wa Kibaki waganda watoto wa Museveni

  chuki na wivu tu
   
 18. Kidzogolae

  Kidzogolae Senior Member

  #18
  May 20, 2008
  Joined: Apr 20, 2008
  Messages: 134
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hahaha, ungejua huyo JK unaemsifia ameajiriwa na wananchi wa Tz, kuanzia mkulima hadi mfanya kazi, usingesema vijana wa JK. Hao ni vijana na watoto wa watz. Usiwe unampa masifa Raisi awaye yote yule kama vile yeye ni mfalme mteule. Kwa miaka ya siku hizi za uelewa, Rais wetu ni Muajiriwa tu ambaye sisi tumemwamini na kumkabidhi majukumu makubwa ya kuongoza nchi. Ndo maana lazima anatakiwa kuwa accountable kwa wananchi wake. bila wananchi huyo JK angepata wapi kibarua?hujui kama kodi zetu ndo zinazomfanya aishi?Kodi anayokatwa hadi mtoto wako kwa VAT akinunua pipi...., ndo inayomfanya yeye apande ndege na kutuwakilisha kufanya yale majukumu ya juu. kuna siku kibarua kitaisha. Kwahiyo, watu wenye Rungu la kupata sifa za nchi yetu, sio mwajiriwa, ni Mwajiri ambae ndo sisi watz wote. Tunatakiwa kuwa proud wote kwa pamoja, sio kumpa sifa mtu mmoja kwavile tu yeye ni rais. Kama uongo, we subiri kinyang'anyiro kijacho, utakavyoona anavyojikomba kwa wananachi ili tumwajiri kwa miaka mingine mitano. hapo ndo utajua kuwa WANANCHI NDO WASHIKA RUNGU. na wananchi ndo wamiliki wa vitu vyote.

  Hongera sana Taifa stars. lakini nawapeni pole, nasikia mmepata shida sana kule uganda, viongozi wa FUFA hawajawatendeeni vyema kama sisi tulivyowafanyia wao hapa. pia, nasikia kuna mashabiki wetu wengine waliumia, na mwanafunzi mmoja wa Kampala mtz. poleni na viongozi pia. Mi nilifikiri Mpira huu kwa waganda ndo ungeonyesha namna gani wao ni watu wanaowajali watz, ili kupromote Huo muungano wanaoulilia. sasa kama hata kukiwa na muungano, MBONA KUTAKUWA NA UUGANDA, UTANZANIA, NA UKENYA, UBURUNDI, NA URWANDA. tusije tukaishia kusuluhisha matatizo kama ya Pemba. Esalaleee...hahaha.
   
Loading...