Taifa Stars yaendelea na mazoezi kuelekea CHAN

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Sep 11, 2020
69
104
20210104_124033.jpg
Kikosi cha Timu ya taifa "Taifa Stars" kimeendelea na mazoezi leo katika uwanja wa Gymkhana kwa ajili ya kujiandaa na michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya DR Congo na mashindano ya CHAN yatakayofanyika Cameroon.

Mashindano ya CHAN awali ilikuwa yafanyike kuanzia tarehe 4 hadi 25 mwezi Aprili 2020 nchini Cameroon lakini CAF ilitangaza kuahirisha mashindano hayo hadi Januari 16, 2021 kutokana na janga la COVID-19.

Awali Ethiopia ilipewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo lakini Shirikisho la soka nchini humo, EFF lilikiri kwamba haikuwa tayari kuandaa mashindano hayo na nafasi yake kupewa Cameroon kuwa mwenyeji wa michuano hiyo.

CHAN, tofauti na Kombe la Mataifa ya Afrika, timu za kitaifa zinazoshindana lazima ziwe na wachezaji wanaocheza ligi yao ya nyumbani pekee.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom