CHAN 2018: Miaka 9 Baadaye, Sh330 Milioni Zilikwenda Wapi?

CHAN 2018: Miaka 9 Baadaye, Sh330 Milioni Zilikwenda Wapi?

Omu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
414
Reaction score
86
Kenya ilipoteza nafasi ya kuandaa CHAN 2018, lakini miaka tisa baadaye, uchunguzi umeibua swali jingine: Sh330 milioni zilizolipwa kwa maandalizi ya mashindano hayo zilienda wapi?

EACC inadai fedha hizo zilikuwa sehemu ya mkataba wa takribani Sh1.5 bilioni wa kusambaza na kuweka mifumo ya usalama, mawasiliano, audiovisual na taa katika viwanja mbalimbali. Kampuni ya Auditel Kenya ililipwa zaidi ya Sh330 milioni kama malipo ya awali, lakini wachunguzi wanadai hakuna vifaa vilivyowahi kuwasilishwa.

Uchunguzi pia unadai mkataba huo ulitolewa kupitia single sourcing, bila baadhi ya taratibu muhimu za kawaida za ununuzi wa umma, ikiwemo nyaraka za zabuni, bid security na mifumo ya kutosha ya kusimamia utekelezaji.

Sasa DPP ameidhinisha mashtaka dhidi ya aliyekuwa Sports PS Peter Kaberia, maafisa wengine wa zamani wa serikali, wafanyabiashara pamoja na kampuni kadhaa baada ya kupitia ushahidi uliowasilishwa na EACC. Hata hivyo, haya bado ni madai yatakayopimwa mahakamani.

Lakini kwa mwananchi, uchunguzi huu unaacha swali kubwa zaidi:

Inawezekanaje Sh330 milioni za umma zilipwe kabla ya kazi kufanyika, mashindano yasionekane Kenya, vifaa visiletwe—halafu majibu yaje karibu miaka tisa baadaye?
 

Attachments

  • kaberia.jpg
    kaberia.jpg
    37.4 KB · Views: 2
Back
Top Bottom