Kuna mambo yaliyo juu zaidi ya ushindi wa mpira. Sisi tuliingia uwanjani kama washindani, si washiriki wa kujaza idadi.
Asiyekubali kushindwa si mshindani wa kweli. Mpira ni mchezo wa wazi, na kila aliyeutazama ameona kilichotokea. Licha ya udogo wa jina letu katika mashindano haya, tumeonyesha wazi kuwa tunaweza kushindana.
Tuliwadhibiti wapinzani kwa kiasi kikubwa na tuliweza kutengeneza nafasi kadhaa, lakini tumeshindwa kuzitumia ipasavyo. Wapinzani walipata nafasi nyingi zaidi, lakini moja tu ndiyo iliyozaa goli.
Tulichezewa rafu mara nyingi, lakini refa alikuwa akipeta tu. Dakika za mwisho kabisa, Nado alisukumwa waziwazi ndani ya boksi la penalti, lakini refa alipuuza tukio hilo kana kwamba tayari kulikuwa na maelekezo—lazima wenyeji washinde.