Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,112
Mwandishi wa Habari na Mchambuzi wa Michezo Nchini Wilson Oruma (Mzee wa Jambia ameibua mapya kuhusu mwenendo usioridhisha wa matokeo ya Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) ambayo jana tu, imetoka kupoteza kwa kufungwa goli 2 na Timu ya Taifa ya Guinea Bissau,
Kupitia chapisho lake aliloweka kwenye mitandao yake binafsi ya kijamii ikiwemo Instagram, Mzee wa Jambia amedai kwamba kabla ya kuwalaumu wachezaji wa TAIFA STARS, kwanza ifahamike kuwa wachezaji hao walikaribia kugoma kucheza mchezo wa jana kutokana na kudai malimbikizo ya posho zao za kambi tatu (3) tofauti na kwamba ilifanyika jitihada za 'kuwabembeleza' ndipo wakaridhia kuingia uwanjani kucheza,
Mzee wa Jambia ameenda mbali zaidi na kudai kwamba hata leo, Jumamosi Septemba 26.2026, kabla hawajaanza safari ya kuelekea Morocco wachezaji hao walikuwa mbioni tena kugomea safari hiyo, ikabidi 'wabembelezwe' tena,
Kando na madai hayo aliyoyasema Mzee wa Jambia pia ametumia chapisho hilo kuandika hivi:
"Timu ya Taifa hali ni mbayaaaaaa.....,
Imagine wachezaji wanakaa chini ndani ya Boat, Why? kwa sababu ticket wamekatiwa economy so inabidi waombe kwenda VIP na Royal ambako huko tayari watu wamekaa kwenye siti zao"
"Kama mchezaji hawezi kupata VIP treatment national team, kumbe anaweza kupata wapi?, halafu tukikaa tunasema national team ni nembo ya Taifa. Sio kweli namna hii".