Kabla ya kumponda kocha tujiulize tulishafanya nini kimataifa?CECAFA mara 2,CAF mara 1.Simba na Yanga wamefanya nini kimataifa?
Je kuna mchezaji hata mmoja wa Kitanzania aliyewahi kung'aa kwenye ligi ngumu? Hatuna mfumo wa soka, hatuna viongozi makini. Vimashindano vya vijana ni utani mtupu.
Ok,tunasema kocha wa bei rahisi,kocha gani wa kiwango cha juu atakuja kuharibu Cv yake hapa,Maximo ametoka hapa amekosa timu kabisa kwa sababu hakufanya lolote.
Hao wazawa wanaolilia kupewa timu wamefanya nini? Kama hawawezi hata kuvuka mipaka na kufundisha klabu za CECAFA Watawezaje Taifa stars?Kwanza wakasome, wengi wao hata leseni A za CAF hawana.