Taifa Stars tafuteni kipa mahiri na siyo Manula

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Leo nimeshuhudia mtanange baina ya Taifa Stars na Benin kupitia luninga. Kusema ukweli Taifa Stars wamecheza vizuri kuliko wapinzani wao aliyewaangusha ni kipa Manula.

Namshauri Kocha wa Taifa Stars kutafuta kipa mahiri badala ya Manula. Kipa gani anashindwa kudaka mpira uliopigwa mita 30 kama ya leo.

Wapo akina Kakolanya, Metacha, Mgore n.k. Kwa nini kila uchaguzi wa Taifa Stars kipa ni Manula?. Achaneni na Manula. Leo lawama lazima zimwendee kutokana na goli lililofungwa na Benin.
 
Hahaha,angalia tena kwa makini marudio ya lile goli mkuu,umemuona yule mpigaji alivyopiga ile kitu? na jinsi beki zetu zilivyojipanga pale lile goli kwa mazingira Yale kipa yoyote duniani anafungwa goli la aina ya ile,lile pigaji la ule mpira ni liuaji haswaaa...
 
Afu uwe unaongea kimpira na sio kiushabiki!Kwa lile goli hamna wa kumlaumu,ni uwezo binafsi wa mchezaji aysee.
Na ndiyo wakati huo huo na golikipa nae alitakiwa aoneshe uwezo wake binafsi. Ila kwa bahati mbaya ndiyo hivyo tena! Huyo Manula kutunguliwa magoli ya mbali, ni kawaida yake.

Mfano Yanga mara nyingi akutanapo na Mo fc, huutumia udhaifu wa huyu golikipa wake kumtungua wakiwa nje ya 18 na kujipatia point 3 muhimu kiulaini.
 
Na ndiyo wakati huo huo na golikipa nae alitakiwa aoneshe uwezo wake binafsi. Ila kwa bahati mbaya ndiyo hivyo tena! Huyo Manula kutunguliwa magoli ya mbali, ni kawaida yake.

Mfano Yanga mara nyingi akutanapo na Mo fc, huutumia udhaifu wa huyu golikipa wake kumtungua wakiwa nje ya 18 na kujipatia point 3 muhimu kiulaini.
Yule Kapumbu aliwafanyaje mwananchi day
 
Leo nimeshuhudia mtanange baina ya Taifa Stars na Benin kupitia luninga. Kusema ukweli Taifa Stars wamecheza vizuri kuliko wapinzani wao aliyewaangusha ni kipa Manula...
mtu yeyote anayecheza na watz huwa anawajua udhaifu wao, wanatumia sana minguvu, hawatumii akili.

wameuchezeaa mpira hadi wakachoka, jamaa wamechukua tu mara moja hadi golini wakarudi kulinda goli.

sisi tumekosakosa magoli rundo. leo kama tungekuwa na wafungaji tungefunga magoli 5, lakini wote hamna kitu.
 
mtu yeyote anayecheza na watz huwa anawajua udhaifu wao, wanatumia sana minguvu, hawatumii akili. wameuchezeaa mpira hadi wakachoka, jamaa wamechukua tu mara moja hadi golini wakarudi kulinda goli. sisi tumekosakosa magoli rundo. leo kama tungekuwa na wafungaji tungefunga magoli 5, lakini wote hamna kitu.
Huo ndio utofauti wa ndondo na proffesionals!!sana sana mtakimbilia bahati haikuwa kwetu!!mpira ni sayansi sio kwenda kwa kubahatisha, matokeo yake ndio hayo timu inakuwa kama homa ya vipindi!!kutoa draw na DRC, na kuifunga Madagascar tu, mlikuwa mnajiona level nyingine kabisa!!WAZEE WA KUTIANA HAMASA, badala ya kuangalia uwezo wenu.
 
Hakukuwa na mipango katika finishing. Mimi huamini mkicheza na timu mliyoizidi possession kwa muda mwingi na kushindwa kuifunga lazima majanga au lawama zitawageukia tu. Maana kulinda goli ugenini pia ni akili kubwa ya mchezo!
 
Goli gumu sana kudaka yule jamaa amefunga goli la akili sana kama mzungu wa hispania.
Manula halaumiwi mabeki ni misukule pia kina samata hawana ari ya kulazimisha matokeo...uwendawazimu unaendelea kututafuna.
 
Leo nimeshuhudia mtanange baina ya Taifa Stars na Benin kupitia luninga. Kusema ukweli Taifa Stars wamecheza vizuri kuliko wapinzani wao aliyewaangusha ni kipa Manula. Namshauri Kocha wa Taifa Stars kutafuta kipa mahiri badala ya Manula. Kipa gani anashindwa kudaka mpira uliopigwa mita 30 kama ya leo. Wapo akina Kakolanya, Metacha, Mgore n.k. Kwa nini kila uchaguzi wa Taifa Stars kipa ni Manula?. Achaneni na Manula. Leo lawama lazima zimwendee kutokana na goli lililofungwa na Benin.
Hapana japimo mie ni yabga hilo goli sio kosa la manula

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Ilo goli linatofauti gan na goli la Messi juzi dhidi ya Man city kwaio kipa wa city amna kitu anachojua?upande ni uleule makosa ya beki yaleyale mguu wa shoto uleule ngoja niattach ilo goli urudie kuangalia vzur
 
Back
Top Bottom