Taifa Stars Kwenda CHAN: Siasa zisipewe nafasi kabisa

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,798
71,218
Yaliyoipata Taifa Stars ilipofuzu AFCON 2019 hatutaki kuyaona tena yakijirudia.

Safari hii Stars imejishindia safari ya fainali hizo huko Cameroon kwa juhudi zao na hao wanasiasa wakiwa wamesha ikatia tamaa baada ya kuwa imefungwa mechi ya nyumbani.

Kauli za watu kama Makonda kuwa Stars inatekeleza ilani ya CCM ilifanya Wa Tanzania wasio na mapenzi na chama hicho kuona timu imebinafsishwa hivyo hamasa kupotea na kwa kauli hiyo ilifanya Taifa Stars ichukiwe na kundi kubwa la Watanzania hadi kuitolea kejeli mbaya za kuwa nyong'onyeza wachezaji.

Hiyo kamati mnaita ya hamasa ivunjwe na kuundwa mpya ya watu makini wanaoheshimika na jamii ya makundi tofauti na wenye historia na mpira na sio watu wengine ambao hawajui hata wachezaji wako wangapi dimbani.

Siasa iwe mwiko kabisa, mbona nchi zingine hazina siasa michezoni iweje hapa?

Karia kama hawezi kujitoa kwenye makucha ya wanasiasa kama Makonda basi sisi wenye timu (watanzania) tutamtoa yeye.
 
naichukia stars. wakati mwingine naiombea ifungwe ili hawa wapuuzi wanayoitumia kisiasa wakose cha kuongea
Sasa bora kulionya hilo lisitokee tena. Siasa ndio maana hata FIFA wamekataza kuingizwa michezoni kwani inaharibu badala ya kuleta upendo.
Mpira umewahi kutumika hata kwenye nchi zenye vita kuwaunganisha wagomvi. Kuna wakati Savimbi alisimamisha vita Angola kwa vile timu yao ya Taifa ilifuzu michuano ya world cup
 
Nchi ikijaa wananchi kama wewe mleta mada basi inabadilika na kuitwa south sudan.

Wanasiasa ndio wanaoiongoza nchi unayoishi wewe,waziri wa michezo ni mwanasiasa.

Tatizo nchi hii ni pale watu waliokuwa na matarajio makubwa ya upigaji na pia uongozi,walipojikuta wamepoteza.
Halafu aliyeingia akafuta mazowea.sasa hii sumu na mapovu ni wale wooote ambao ndoto zao hazikutimia w015
 
Nahisi hujitambui! Kwako wewe mwanasiasa kusema hadharani kuwa mafanikio ya timu ya taifa ni kutokana na chama Fulani cha Siasa wakati hata timu yenyewe wachezaji wana itikadi tofauti unaona sawa?
Unahitaji kupimwa!
 
Wewe mwenyewe mwanasiasa kwa nini unaongelea michezo?

Huna tija yoyote zaidi ya kutafuta ufitinishi tu,hata kama mwanasiasa alitoa kauli ile je inazuia timu huska kuwakilisha taifa.

Nyinyi ndio wale mnaozomeaga timu za nyumbani zikiwa na mechi za kigeni kisa tu ni mtani wa jadi
 
Usinipe cheo sio changu! Mimi sio mwanasiasa na sipendi siasa ya kuingiza kwenye michezo.
 
Amber Rutty wa Dasilamu lazima ajipitishepitishe au kwakuwa Manula hayumooo
Jamani jamani, ndio nini sasa?
IMG_20190918_165019.jpeg
 
ni kweli hatutaki kusikia mara timu imeitwa bungebi au kamati za uhamasishaji au wasanii wa bongo fleva na bongo movie wanajiandaa kuhamasisha taifa stars wakati timu ikifanya vibaya hakuna hata mmoja anayejitokeza
 
Back
Top Bottom