Taifa Stars itasubiri sana, wala tusishangae!

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
stardjamena.png

Stars imekuwa ikiendeshwa kiujanja ujanja tu bila kuwepo program yoyote ya maana ambayo inaweza kuwa dira ya soka la Tanzania hasa linapokuja suala la timu ya taifa.

Jambo baya zaidi ni kwamba, wadau mbalimbali, wakiwemo waandishi wa habari na wachambuzi mahiri wa masuala ya michezo, wanapoanza kuchambua na kukosoa (kama ninavyofanya hapa) hubatizwa majina mengi na wengine kuitwa ‘wanafiki’ au ‘hawana uzalendo’.

Kutokana na kukosolewa huko, viongozi wa soka hufunika kila wanapofungua ukurasa kwenye magazeti, ama huzima redio na runinga kila wanapomuona mwandishi fulani anachambua na kuwakosoa.

Badala yake, wamebweteka na taarifa wanazozisoma kwenye magazeti ya michezo kila siku zikipamba na kusifia hata mambo ambayo hayawezekani. Soka limekuwa likichezwa zaidi kwenye magazeti kuliko uwanjani!

Soma zaidi uchambuzi huu hapa=> Taifa Stars itasubiri sana! | Fikra Pevu
 
Back
Top Bottom