Sumbaye
Member
- Apr 26, 2025
- 59
- 77
Kwa miaka ya karibuni zimesikika kauli mbali mbali kutoka kwa viongozi wa serikali juu ya wahitimu wa vyuo vikuu Tanzania kwamba elimu yetu ni ya kukariri, elimu yetu inazalisha graduates wasioendana na soko la ajira, na baadae tukasikia wahitimu wajiajiri. Bado haikutosha, tukasikia hivi karibuni wahitimu wa vyuo vikuu waende VETA ili kujiajiri. Ukiwasikiliza wale wanamajumui wa Africa wao wanalaumu kwamba wazungu wametupatia elimu ya kukariri ili waendelee kututawala. Ukiwauliza swali kwamba tukitaka kubadili mitaala yetu ni lazima tupate ruhusa ya wazungu? Jibu ni hapana, watawala hubadili mitaala kulingana na mahitaji yao na uwezo wa kifedha. Swali la pili ili tuwalaumu Zaidi wazungu kwa kutupatia elimu ya kukariri, ni je bajeti ya wizara ya elimu nayo tunapitisha baada ya kupata ruhusa ya wazungu? Jibu ni hapana. Je tatizo ni wazungu au sisi wenyewe?
Baada ya maswali ya msingi naomba niwarudishe kwenye historia kidogo. Taifa lolote linalopiga hatua popote duniani ni taifa linalothamini elimu ya juu. Elimu ya juu ndio inayotoa Dira na mwelekeo wa kitaifa juu ya maendeleo kupitia tafiti. Ikiwa hufanyi tafiti kutatua matatizo yako huwezi kuendelea. Nchi zinaozopiga hatua kubwa kwa maendeleo sasa, ni nchi zilizofanya mapinduzi makubwa kwenye elimu. Ukiangalia Asia four Tigers kama Singapore, Taiwan, South Korea na China ni nchi zinazopiga hatua kwa kasi sana. Ukirejea hadhi ya elimu ya juu, vyuo vikuu vilivyopo Top ten Asia vinatoka kwenye hizi nchi pia. Ukichunguza kwa undani, miaka 10 iliyopita, list ni ile ile. Ukirudi nyuma miaka 50 iliyopita list inabadilika, vyuo hivi havikuwepo kabisa kwenye Kumi bora.
Ukiangalia North America, vyuo vikuu vyenye ranking ya juu vipo US na Cananda na ndio mataifa yenye uchumi mkubwa. America kusini, vyuo vikuu vyenye hadhi kubwa vipo Brazili ndio taifa lenye uchumi mkubwa likifuatiwa na Argentina. Orodha ni hiyo hiyo ulaya na Australia. Halikadhalika katika Bara la Africa, vyuo vikuu vyenye hadhi kubwa katika kumi bora, vyuo Vinne vya juu vinatokea South Africa na ndio taifa lenye uchumi mkubwa, likifuatiwa na Egypt. Ukirudi Tanzania, UDSM amacho ni chuo cha kwanza Tanzania, inashika nafasi ya 26 Africa ikifuatiwa na SUA ambayo ipo nafasi ya 53 Africa. Hii inaendana kabisa na kasi ya maendeleo yetu though kuna irregularities kidogo.
Hivyo Kuna uhusiano mkubwa sana Kati ya elimu ya juu na maendeleo.
Gunduzi kubwa duniani zenye mchango mkubwa kwenye maendeleo zinafanywa na taasisi za elimu ya juu. Usipowekeza katika elimu, sahau kuhusu maendeleo. Maana hutaweza kutatua matatizoya wananchi wako. Kwa bahati mbaya zaidi wanaotakiwa kuamua hatima ya elimu yetu na Maendeleo na wao wanawalaumu wahitimu. Wahitimu na walimu nao wameingia mtego wa kulaumiwa ili wasimnyooshee kidole anaepaswa kuwajibika.
Wasalaam