Taifa limegawanyika kuhusu UKUTA

Taifa limegawanyika kuhusu UKUTA

Matamko mengi na kwa UKUTA, sijasikia matamko juu ya watz wanaouwawa Kagera. Au kwakuwa wao wana Bunduki?
 
Haswaa kama J.P.M angekuwa mjanja angamaliza haya mambo mapema kwa mazungumzo.. sasa angalia now tension ilivokubwa kila mahali
Anasema hajaribiwi.
Binafsi nadhani Urais si ubabe.Urais ni kuleta umoja mahali ambapo kuna utengano.Rais is wa wana-CCM pekee ni Rais wa wananchi wote bila kujali itikadi.Tupime busara za Rais wetu tuone kama atafaulu katika hili.
 
Mkuu;
Huenda hata shule ya upili hukufika ndo maana imekuwa ngumu kwako kunisoma. Tungewekwa kwa kipimo cha ujasiri weye hata robo yangu huna.
Ujasiri unaouongelea wew ni wa jinsia gani? ME au KE?.
Nitarudi tena.
 
You are absolutely right! Jambo dogo limekuzwa saana. Magufuli alikuwa ana support kubwa saana ya wananchi kwa ujumla, pamoja na wapinzani. Angeendelea na azma yake ya kuondoa mafisadi, kuleta viwanda, elimu bure, nk. Sasa wananchi wote, wanao mkubali na wasiomkubali, UKUTA ndio imekua agenda ya nchi. He lost political capital which is hard to get.

wanamchi wa wapi hata huku rombo , amna kitu kama hicho wala watu hawajui kama kuna kitu kama hicho ,labda wa jf ,
 
UKUTA wala usingekuwepo kama si huyu mhujumu amani ya nchi yetu ambaye ameamua kutoiheshimu katiba ya nchi. Wabunge mahiri wa upinzani wasingefukuzwa Bungeni na ile kamati fake ya maadili bungeni chini ya jipu Tulia. Vyama vya upinzani vingekuwa vinafanya mikutano na maandamano yao popote pale nchini bila kujali kama wana mbunge maeneo haya au la na bila kuletewa kero zozote zile na polisiccm. Kauli za vitisho dhidi ya upinzani nchini "msinijaribu" zisingekuwepo.

Taifa limegawanyika na wa kulaumiwa kwa nguvu zote ni mhujumu wa amani na mshikamano wa Watanzania (Magufuli) na nchi iko katika hatari kubwa sana ya machafuko makubwa.

Nilikuwa mapumzikoni kidogo kwa wiki moja, baada ya kazi nzito ya kusukuma gurudumu la maendeleo la Taifa hili la Tanzania.

Katika mapumziko yangu nimetumia muda kujaribu kufuatilia vuguvugu la UKUTA kwenye mitandao ya kijamii na mitaani pia, mwanzoni nilijua UKUTA haina wanachama na ilikuwa ni mbinu ya CHADEMA kuitisha serikali ili wafikie maridhiano, lakini cha kushangaza ni kuwa kuna watu wengi mno, hasa vijana wamehamasika, na kudai kuwa wanasubiria Sept 1 kwa hamu kubwa.

Nimeona jinsi mikakati mingi ya UKUTA ikiendelea kwa upande mmoja na upande mwingine polisi wakifanya mazoezi, ambayo mimi nimeyatafsri kuwa ni njia ya kutoa vitisho kwa wale wanaotaka kuandamana.

Nimeona jinsi kulivyo na tension kubwa katika mitandao ya kijamii kati ya makundi mawili, wanaounga mkono UKUTA na wasiounga, ambao wengi wao wameegemea upande wa serikali na chama tawala.

Nina wasiwasi Sept 1 inaweza kuwa ni siku ya madhara makubwa nchini kuwahi kutokea iwapo pande zote mbili hazitakaa na kufikia mwafaka. Nimepata hofu kuwa nchi inaweza kuingia kwenye vurumai, watu wakafa, tukawekewa vikwazo na kujikuta tunabeba hela kwenye kapu kwenda kununua mkate sokoni kama ilivyokuwa Zimbabwe. Kingine ni wahusika wa sakata kujikuta The Hague.

Habari za UKUTA na maandalizi ya polisi zinazidi kupaa katika anga za kimataifa.

Tensions rise ahead of Ukuta protests

Police ban on political rallies, demonstration lawful

Kwa wasiojua, vita kwenye nchi yoyote ile hasa za kiafrika, ina masilahi makubwa kwa mataifa makubwa hasa USA na Europe.


Mwenye masikio na asikie, naenda zangu.


Kutoka FACEBOOK Page ya Edward Ngoyai Lowassa:

"Leo nimezunguka katika majimbo ya Mbeya Vijijini ,Vwawa na Tunduma nikiwaeleza kuhusu Operation UKUTA,

UKUTA si fujo , UKUTA si machafuko na hatuna haja ya kufanya fujo , tunapiga kelele dhidi ya uvunjwaji wa haki ya kidemokrasia na katiba ya nchi unaofanywa na utawala huu wa awamu ya tano .

CHADEMA ni nani wakapambane na polisi ,polisi ambao ni watoto wetu ,ndugu zetu na hata wake na waume zetu ila tuwahakikishie hatutorudi nyuma pale katiba na haki ya kidemokrasia ikichezewa au kuwa chini ya mtu fulani . Najua polisi watapiga watu ,wataumiza watu na hata kuua ila niwahakikishie wao na walio na mamlaka wataishia katika mahakama ya Kimataifa .

Siasi ni mazungumzo ,lazima tuzungumze milango yetu iko wazi kufanya mazungumzo ila kwa kuwa hawahitaji na sisi hatutorudi nyuma September Mosi ,tumejiandaa vya kutosha na sasa tuko ngazi ya kaya na wajumbe wetu wanakamilisha kazi katika kaya ili tarehe mosi sauti ya kutosha ipazwe kwa maandamano na mikutano kama tulivyokubaliana katika kata zetu na majimbo nchi nzima . Haiwezekani hata kidogo mtu mmoja azuie kila kitu ,nchi hii ni mali yetu sote na inaongozwa na Katiba na sheria.

Kamati kuu ilipo amua katika suala la UKUTA haikukurupuka , kamati kuu yetu inaundwa na mchanganyiko wa wasomi wa kada mbalimbali ,wazee wenye busara na vijana machachari kamwe hawawezi kukukurupuka na UKUTA ni haki ya watanzania wote.

Pili naomba niwape siri ya ushindi 2020 ndugu zangu na wanachama wenzangu , tutashinda uchaguzi Mkuu 2020 kama tutafanya yafuatayo na kuyasimamia
Kwanza; Umoja ndani ya Chama na wanachama ,tuheshimiane ,tusameheane na tuimarishe chama chetu
"Chama ndani ya Chama , chama nje ya chama na chama ndani ya Umma ""
 
Habari wana jf, hizi habari za UKUTA ni habari zinazo trend sana kwenye vyombo vya habari kama vile magazeti,television mbalimbali na hata kwenye mitandao ya kijamii. Ukizisoma vizuri habari zinazohusu huu mpango mkakati wa kukomesha udikteta uchwara kwa wenyewe walengwa wanavyomaanisha utaona ni kwa namna gani watu wanajinasibu kwenda balabalani siku ya tarehe 1 sept humu mitandaoni.

Tatizo linakuja nimejaribu kuongea na watu wengi mitaani kwetu na maeneo ya kazi kila ninayeongea naye kuhusu inshu hii naona hayupo pamoja kabisa na hawa watu wa UKUTA sasa nawaza mbona mitandaoni naona watu ni wengi waliohamasika lakini nikija kiuhalisia mtaani hakuna watu waliohamasika hivyo.

Nilichokigundua...

Watu wanaopost mitandaoni kuhusu kuhamasika juu ya UKUTA na kuapia kuingiya barabarani tarehe 1 sept ndio hao hao tunaokutana nao mitaani na tukizungumzia suala la ukuta wanatoka nduki hawataki hata kusikia. Ni unafiki umetujaa ni wepesi kwenye kuongea lakini ni waoga kutenda.

Ushauri kwa vijana wenzangu...

Usidanganyike na thread na michango ya watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wengi ni wanafiki.
Unaweza ukawaona wapo wengi lakini cha kushangaza tarehe 1 Sept ukawa peke yako barabarani ukiambulia kula virungu vya polisi kipuuzi tu. Watanzania tumejawa unafiki mwingi.

NB: Akili za kuambiwa please changanya na za kwako.
 
Unataka kusema hakutakuwa na watu wakitembea siku hiyo?! Mpaka wewe mmoja tu ndiye uwe pekee barabarani!
 
images
 
Dalili zinasema tarehe moja lazima kitaumana.

Mjiandae kuona JF na mitandao mingine ya kijamii inazimwa tarehe 1 ili kuzuia mawasiliano kusambaa.
 
Serikali imekuza mambo. Wangewapuuza chadema yasingefika huku yalipo.
Kikwete aliweza ila kwa John hapana.
Yani hamna cha ukuta wala matofali let us wait and see! Watanzania lazoma wafuate sehria na haman aliye juu ya sheria. Mleta mada amesema Lowas anazunguka huko sasa je kama Mh. Rias angekuwa amekataza Lowasa angewezaje zunguruka huko alipo?
 
Ukuta karibu tuheshimiane, tumejiandaa vya kutosha
 
Nimeiona sehemu

"Ccm mbele kwa mbele. TUMEWAVUMILIA MNO, MMETUTUKANA MNO, MMETUDHIHAKI MNO. SASA NGOJA TUWAONESHE, MKISHINDA SAWA TUKISHINDA MTUHESHIMU"
 
Back
Top Bottom