Nilikuwa mapumzikoni kidogo kwa wiki moja, baada ya kazi nzito ya kusukuma gurudumu la maendeleo la Taifa hili la Tanzania.
Katika mapumziko yangu nimetumia muda kujaribu kufuatilia vuguvugu la UKUTA kwenye mitandao ya kijamii na mitaani pia, mwanzoni nilijua UKUTA haina wanachama na ilikuwa ni mbinu ya CHADEMA kuitisha serikali ili wafikie maridhiano, lakini cha kushangaza ni kuwa kuna watu wengi mno, hasa vijana wamehamasika, na kudai kuwa wanasubiria Sept 1 kwa hamu kubwa.
Nimeona jinsi mikakati mingi ya UKUTA ikiendelea kwa upande mmoja na upande mwingine polisi wakifanya mazoezi, ambayo mimi nimeyatafsri kuwa ni njia ya kutoa vitisho kwa wale wanaotaka kuandamana.
Nimeona jinsi kulivyo na tension kubwa katika mitandao ya kijamii kati ya makundi mawili, wanaounga mkono UKUTA na wasiounga, ambao wengi wao wameegemea upande wa serikali na chama tawala.
Nina wasiwasi Sept 1 inaweza kuwa ni siku ya madhara makubwa nchini kuwahi kutokea iwapo pande zote mbili hazitakaa na kufikia mwafaka. Nimepata hofu kuwa nchi inaweza kuingia kwenye vurumai, watu wakafa, tukawekewa vikwazo na kujikuta tunabeba hela kwenye kapu kwenda kununua mkate sokoni kama ilivyokuwa Zimbabwe. Kingine ni wahusika wa sakata kujikuta The Hague.
Habari za UKUTA na maandalizi ya polisi zinazidi kupaa katika anga za kimataifa.
Tensions rise ahead of Ukuta protests
Police ban on political rallies, demonstration lawful
Kwa wasiojua, vita kwenye nchi yoyote ile hasa za kiafrika, ina masilahi makubwa kwa mataifa makubwa hasa USA na Europe.
Mwenye masikio na asikie, naenda zangu.
Kutoka FACEBOOK Page ya Edward Ngoyai Lowassa:
"Leo nimezunguka katika majimbo ya Mbeya Vijijini ,Vwawa na Tunduma nikiwaeleza kuhusu Operation UKUTA,
UKUTA si fujo , UKUTA si machafuko na hatuna haja ya kufanya fujo , tunapiga kelele dhidi ya uvunjwaji wa haki ya kidemokrasia na katiba ya nchi unaofanywa na utawala huu wa awamu ya tano .
CHADEMA ni nani wakapambane na polisi ,polisi ambao ni watoto wetu ,ndugu zetu na hata wake na waume zetu ila tuwahakikishie hatutorudi nyuma pale katiba na haki ya kidemokrasia ikichezewa au kuwa chini ya mtu fulani . Najua polisi watapiga watu ,wataumiza watu na hata kuua ila niwahakikishie wao na walio na mamlaka wataishia katika mahakama ya Kimataifa .
Siasi ni mazungumzo ,lazima tuzungumze milango yetu iko wazi kufanya mazungumzo ila kwa kuwa hawahitaji na sisi hatutorudi nyuma September Mosi ,tumejiandaa vya kutosha na sasa tuko ngazi ya kaya na wajumbe wetu wanakamilisha kazi katika kaya ili tarehe mosi sauti ya kutosha ipazwe kwa maandamano na mikutano kama tulivyokubaliana katika kata zetu na majimbo nchi nzima . Haiwezekani hata kidogo mtu mmoja azuie kila kitu ,nchi hii ni mali yetu sote na inaongozwa na Katiba na sheria.
Kamati kuu ilipo amua katika suala la UKUTA haikukurupuka , kamati kuu yetu inaundwa na mchanganyiko wa wasomi wa kada mbalimbali ,wazee wenye busara na vijana machachari kamwe hawawezi kukukurupuka na UKUTA ni haki ya watanzania wote.
Pili naomba niwape siri ya ushindi 2020 ndugu zangu na wanachama wenzangu , tutashinda uchaguzi Mkuu 2020 kama tutafanya yafuatayo na kuyasimamia
Kwanza; Umoja ndani ya Chama na wanachama ,tuheshimiane ,tusameheane na tuimarishe chama chetu
"Chama ndani ya Chama , chama nje ya chama na chama ndani ya Umma ""