Napata uchungu sana ,kwa mtindo huu Demokrasia imeshindwa Tanzania na sasa ili kuwe na uwiano sawa na mgawanyo sawa wa raslimali ni bora kurejea katika mbinu kongwe ya uanamapindui ili sasa tuanzie hapo.Ndiyo maana naendelea kuwaheshimu akina Fidel Castro,Che Guevara,Col.Muamar Gaddaffi,Evo Morales wa Bolivia,Hugo Chavez wa Carcas Venezuela na hata Yoweri Museven.....hawa ni ma-role model wangu kwa kusema kweli. Si mapinduzi yote ni haramu,hwa jamaa wote walifanya mapinduzi ambayo ukifutilia kwa makini uchumi katika nchi zao ulianza kuwa stable,sasa naona CCM watanifanya nibadili muelekeo wangu wa kisiasa.
Siwezi kuvumilia kuona watanzania wakiendelea kuwa maskini huku CCM wakiendelea ku-play Delay tactics zao ili wabakie madarakani huku majirani zetu wakiendelea kutukejeli kila siku,Ni Lazima Heshima ya Mtanzania irudi! Roho inaniuma sana,yaani hata fikra mbadala CCM wanazikemea,hwa ndiyo wanotulazimisha wengine kutumia njia haramu,potelea mbali.Taifa gani ambalo wananchi wake ni maskini,wanakufa kwa maradhi,huku tunakosa mbinu mbadala za kukuza uchumi kwa sababu ya wapuuzi wachache? Hili silo taifa walilopigania babu zetu kama akina Mkwawa,Mirambo,Mangi sina,kimweri au akina Jk Nyerere,Bibi Titi,mzee kizota na wengineo,Mungu awalaze Pema Peponi.Leo hii viongozi wetu wmegeuka kuwa mawakala wa unyonyaji,wanatumiwa na wahindi,wachina na wazungu mliowakataa kututawala.
CCM ILAANIWE! MUNGU IBARIKI TANZANIA.