mtendaji wa kijiji
JF-Expert Member
- Jul 3, 2012
- 533
- 115
Wapendwa wana JF natumaini mpo salama.
Katika hali isiyo ya kawaida Tembo wanane wameonekana wakirandaranda mitaani katika vijiji vya wilaya ya Same na kuendelea kuharibu mazao ya wananchi pamoja na Miti.
Tembo hao wanaosadikiwa wapo Zaidi ya 30 ambao wametoroka Kutoka Msitu Wa Tembo wameonekana Tangu tarehe 18/05/2016 Katika Kijiji Cha Ishinde Kata Ya Njoro na Siku Moja Baadae yan tarehe 19/05/2016 walionekana katika kijiji cha Saweni. Tarehe 20/05/2016 Walionekana kijiji cha Mng'ende na Leo Jumamosi tare 21/05/2016 Wameonekana katika Milima Ya Kijiji Cha Gonjanza Suji.
Licha ya kuenea kwa taarifa za uwepo wa Tembo hao Bado wananchi hawajaona Jitihada za TANAPA kuwaswaga na kuwarejesha tembo hao mahala walipotoka
Nimeambatanisha picha ya baadhi ya tembo hao kama walivyoonekana katika kijiji cha Gonjanza Suji