Tahadharini LG Tv Workshop usithubutu

Unashangaa kioo kuwa nusu ya bei ya TV nzima? Hiyo ni kawaida kwa simu na TV mkuu. Kawaida sana
 
Pole sana. Mie niliwahi peleka redio ya lg wakaniletea hizo stori. Nkawaambia nalipia 30000 kama mtanipa risiti ya tra.
Jamaa katabasamu akaniambia chukua redio yako
safi sana

sibishanagi na bei,huwa nauliza Risiti napata?

akinijibu ndio nalipa tena nataka ya mashine,ila ajabu ni kwamba

wengi nikiwauliza hili swali wanasusa wanakwambia,nenda kaka 😂
 
Kwa waganda kariakoo tv universal card ni sh 27,000 tu
 
Kioo cha Tv flat kina thamani ya 80% ya Tv nzima
 
Hiyo ni kawaida mkuu. Iliwahi kunitokea. Cha kufanya tafuta namba ya simu ya fundi mmojawapo humo. Kama bei waliokuambia ni 250k mpe 100k huyo fundi atakubadilishia kifaa fasta. Wanaibaga vifaa wakipata dili la nje
 
Daa! Mimi nilipeleka home thierter, ilikuwa na tatizo la kutosoma HDMI pamoja na CD ila ilivyokuja kurudi ikawa afadhari yake maana ikawa na magonjwa kibao ikiwa BT haisomi na redio ukiiwasha inajizima baada ya dk kama 4. Hapo nili force kuichukua baada ya kukaa kwao takribani miezi 3. Hiyo redio niliinua duka la amaizing lipo sinza madukani, na niliwarudishia wao kwa ajili ya kuipeleka kwa agent wa LG
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…